Kwanini wazazi wengi bado wako 'obsessed' na As na Bs za matokeo ya mitihani?

Leo Baraza la mitihani limetangaza matokeo ya kidato cha 2,4 na mitihani ya ufahamu kwa wanafunzi wote waliofanya hiyo mitihani mwaka 2021.

Mwezi june 2022 itatutangazia matokeo ya form 6 pia kama kawaida ya miaka yote, kila mwaka ni matokeo ya ulinganifu wa nani kafanya vizuri na nani kafanya vibaya.

Kinachonisikitisha ni kwamba pamoja na udhaifu mkubwa sana wa huu mfumo wa elimu tulionao ambao bado unawaandaa wanafunzi kua waajiriwa, bado wazazi wengi kama sio wote wako na tamaa ya kuona watoto wao wanapata A ama B au Div 1 au 2.

Wote tunakubaliana kwamba huu mfumo wa kupima watu uelewa ama ufahamu wa kukabiliana na changamoto zinazowazunguka ni wa hovyo lakini bado wazazi wako very much obsessed na As. Pamoja na kwamba huu mfumo wa mitihani ni mbovu, unaua ubunifu, ugunduzi, uvumbuzi na uchambuzi wa masuala muhimu kwenye jamii lakini bado Tanzania yunaikumbatia na kuushadadia kwa kila hali.

Tujiulize, hao top 10 wa kitaifa wa kila mwaka, yaani Tanzania kila mwaka tunapata watu wenye akili kuliko wote 20, je hao ma genius hua wanasaidia nini taifa? Je wanakua na mchango gani kwa nchi? Utashangaa hao brainy ama geniuses 20 wa kila mwaka huishia kupewa kazi serikalini, kuajiriwa eitha kua waalimu vyuo vikuu ama maafisa wa kawaida wa serikali.

Dhana ya elimu ni kumpa mtu ufahamu, uelewa na ujuzi wa kukabiliana na changamoto na mazingira yanayomzunguka. Sasa hnajiuliza toka lini kupata elimu ikawa mashindano? Kwamba hata kutatua changamoto zinazotuzunguka tunazitatua kwa mashindano? Ama mtu akipata A basi yeye atatatua changamoto haraka zaidi na kwa ufanisi kuliko aliepata D? Mbona hatuoni faida za A ama Div 1 kwenye jamii?

Hivi 1 zilivyo nyingi kila mwaka sitegemei Tanzania bado tungekua na changamoto yoyote inayotuzunguka maana tuna geniuses wa kutosha.

Hii mada inaendelea.
Wewe ulitaka watangaze nini sasa.Binadqmu tuna kazi sana Kusolve matatizo au kutokusolve ka mtu na definition yake na uwezi kulinganisha
 
Tatizo Tz siasa nyingi.Tusilaumu TOs wakati mfumo wa elimu ni mbovu hivyo wao wameongoza kwa kukariri tu.Vilevile kuna watu kila siku wanakuwa creative hapa bongo ingawa hawana elimu ya kutosha.Ila wanaishia wapi mkuu zaidi ya kupewa pongezi hatimaye hasikiki tena.Wawe wamefaulu au wamefeli mitihani suala la kufanikiwa kimaisha hapa bongo ni zari tu au kanjanja zako.Hiyo elimu inaweza isitumike kabisa.
#UKIRITIMBA NI ADUI WA MAENDELEO.
Nipe mfano wa hzo problems ambazo zimesoviwa na hao genius!!

Nchi inatangaza magenious kila mwaka afu nch hyo hyo inaenda kujenga stand kuu ya kimataifa kwny swamp area kabisa,,,, like WTF are those u call dem genious
 
Tanzania One/genius akifika chuo anaitwa best student, akifika mtaani anapanga foleni na kuzunguka na bahasha huko wanamuita jobless.

Nafikiri Tanzania kuna matatizo ya kimaadili kuanzia katika ngazi ya familia haya yanapelekea matatizo makubwa ya kimfumo.
 
Tuna upuuzi mwingi kufikiria best student ni yule anayefanya vizuri darasani na tunashindwa kuwatambua watu kwenye holistic education
 
Hilo ni swala lingine na ni tatizo la nchi kiujumla, lkn bado ukweli unabakia kuwa ukweli kwamba mtoto anayefaulu vizuri ( sana) ana nafasi kubwa ya kufanikiwa maishani kuliko yule wa wastani .
Unaposema mtu kafanikiwa uweke waz ktk nyanja ipi kimaisha......kiujumla sote tunalenga kufaninikuwa kiuchumi zaid kuliko nyanja nyingnezo......ktk list (top 10) ya matajir dunian au hata Tanzania hakuna kipanga (As au dv 1) wanaosadikika kama ndio ma*genius kwa kipimo cha ufaulu......fikir sana mwananchi.....binafsi nimepta huku na nimepambania sana hzo A kama si mungu na background ya utafutaj ya familia yang bas nadhan utajir ungekuwa muujiza kwangu
 
Back
Top Bottom