blackcrow
Member
- Sep 24, 2020
- 21
- 43
Kweli leo nimeamini maneno ya mwanamziki wa kizazi kipya BANDO MC kwamba "ata chuo kuna wajinga ndiyo maana kuna mtihani" ni sahihi kabisa. Wazazi wengi wakitanzania wanaosomesha watoto zao vyuo vikuu huwa wana mtindo wa kuwapa watoto zao pesa za ada wakalipe wao wenyewe. Kwa asilimia kubwa mimi naona wanakosea kwani asilimia nyingi ya watoto hupewa ada na wazazi wao na kufanyia mambo mengine. Japo siyo wote kwani tunatofautiana kimalezi lakini wengi huwa na tabia hiyo.
Hii inapelekea wanafunzi kulimbikiza deni la ada na pindi inapofika kipindi cha mtihani anakuwa na jukumu la kuitafuta ile ada ili aweze kufanya mtihani wa kumalizia chuo au kufunga muhula na kama atakosa kufanya mtihani itabidi arudie mwaka. Hatua hii hupelekea wanafunzi wengi kuuza vitu vyao vya thamani kwa gharama ya bei ya chini sana. Unaweza kukuta mwanafunzi alinunuliwa na baba yake PC ya laki 9 anakuja kuiuza laki 1 na nusu au laki 2 ili tuu alipe pesa ya ada aliyotumia. Siyo PC tuuu wengine huuza mpaka vitu vyote alivyonavyo mpaka nguo ili alipe deni la ada asije kukosa mtihani.
Sasa hiyo ni kwa watoto wa kiume vipi kuhusu hawa dada zetu. Kwao huwa ni hatari zaidi kwani wao huamini kuwa miili yao inatosha kabisa kuweza kumaliza tatizo hilo na ndiyo maana ukiingia mjini wanawake wengi wanaojiuza huwa wanafunzi wa chuo na huwa hawajali atatembea hata na lecture ili asije kukosa kufanya mtiani bila kujali kuwa kuna magonjwa.
Wazazi wanapaswa kulitathmini hili kweli unaweza kusema mwangu anajielewa lakini kumbuka mazingira pia humbadilisha mtu anaweza kufika chuo akakutana na mazingira tofauti mwishowe akabadilika kwani vishawishi pia chuo ni vingi.
Hivyo ni muhimu wazazi kwenda kulipa ada wao kama wao na kuwakabidhi watoto zao slip kuliko kumpa ada mtoto akalipe kama kweli unampenda na unataka amalize chuo kama alivyomaliza lasaba, form4, na form 6.
USHAURI WA BURE TUUU.