Kwanini wazazi wa kambo wanawekwa pembeni katika shughuli muhimu za watoto wa kambo? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kwanini wazazi wa kambo wanawekwa pembeni katika shughuli muhimu za watoto wa kambo?

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Quemu, Jul 1, 2011.

 1. Quemu

  Quemu JF-Expert Member

  #1
  Jul 1, 2011
  Joined: Jun 27, 2007
  Messages: 986
  Likes Received: 69
  Trophy Points: 145
  Jana nilihudhuria mazishi ya binamu yangu wa karibu.

  Binamu yangu huyu alilelewa na mama wakambo karibu maisha yake yote.

  Kilichonishangaza na kunisikitisha ni kuona kuwa mama yake wakambo alivyowekwa kando wakati wa mazishi. Ninachomaanisha ni kuwa, wakati wa kumwaga udongo na kuweka mashada kaburini, waliitwa mume wa marehemu, baba mzazi na mama mzazi, wadogo wa marehemu, na mpaka shangazi na wajomba zake. Lakini mama wakambo akarukwa!!

  Hivi ni katika hatua gani mchango wa wazazi wakambo katika malezi ya watoto huanza kuthaminiwa? Binamu yangu amelelewa na mama wakambo toka akiwa mdogo. Lakini leo hii amefariki, ndugu hawaoni umuhimu wa kumhusisha mama huyu kwenye matukio muhimu ya kumwaga udongo na kuweka mashada. Kulikuwa kuna ugumu gani kuwashirikisha wote mama mzazi na wakambo?

  Au ni mpaka pale mama mzazi anapokuwa hayupo (amefariki, nk), ndipo mama wakambo anapopewa heshima yake?

  Na kwenye shughul za harusi mambo yanakuwa hivi hivi....kama mama mzazi yu hai, basi mama wakambo hakai kwenye meza ya wazazi, hatambulishwi, halishwi keki, hanyweshwi shampeni????

  Inasikitisha kuona kuwa mpaka leo hii bado tunaendelea kuwabeza wazazi wakambo
   
 2. King'asti

  King'asti JF-Expert Member

  #2
  Jul 1, 2011
  Joined: Nov 26, 2009
  Messages: 27,508
  Likes Received: 2,249
  Trophy Points: 280
  ni kitu kinachoweza kuumiza hisia za watu. cha muhimu ni uhusiano wa marehemu na mama yake mlezi (sio wa kambo huyo, ni wa karibu). wakati mwingine anayepewa kazi ya u-mc anakuwa haelewi vizuri uhusiano uliopo. Ilitokea wakati wa harusi ya step-brother wangu, ambaye mama alimchukua kabla hata hajaolewa na mzee.

  Kwenye sendoff mama hakutajwa bali mama yake mzazi pekee,japo mama ndo alikuwa high table. lakini mama hakukasirika,manake cha muhimu kwake ilikuwa uhusiano wake na mwanae ambaye yeye kwakwe sio wa kambo, ni mambo ya kidunia tu, yanayopaswa kuangalia kwa uzito wake (mdogo,sio issue sana).

  Aendelee ku-celebrate maisha aliyoishi na mwane huyo, yatosha! akijiskia kukosa amani, amuombe Mungu ampe amana,kwani kazi tunayofanya hapa duniani ni kwa ajili ya Mungu na si kwa wanadamu per ce!
   
 3. Nyamayao

  Nyamayao JF-Expert Member

  #3
  Jul 1, 2011
  Joined: Jan 22, 2009
  Messages: 6,980
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 0
  tunavumilia mengi King'asti, wacha tu...hata ufanyaje utaonekena bado kuna utofauti, don knw y kwa kweli.
   
 4. Zurie

  Zurie JF-Expert Member

  #4
  Sep 14, 2016
  Joined: Jul 6, 2014
  Messages: 961
  Likes Received: 1,621
  Trophy Points: 180
  Waswahili wanasema "Cha mtu naniliuuu".....
   
 5. G

  Gololi One JF-Expert Member

  #5
  Sep 14, 2016
  Joined: Oct 23, 2014
  Messages: 580
  Likes Received: 283
  Trophy Points: 80
  Acheni tu unaweza kulia ukiwa na akili fupi.
   
 6. m

  mnkola Member

  #6
  Sep 14, 2016
  Joined: Aug 18, 2016
  Messages: 91
  Likes Received: 52
  Trophy Points: 25
  Wazazi wa kambo wana mitihani sana...na hilo jina lao ndo kabisaa wanaonekana wabaya mweee
   
 7. n

  nyamwinuka Member

  #7
  Sep 14, 2016
  Joined: Aug 10, 2016
  Messages: 93
  Likes Received: 70
  Trophy Points: 25
  Yaani nyie acheni mmenitonesha roho yangu... Mimi ni mama wa kambo... Nimewakuta watoto wapo primary... Mmoja Kumaliza chuo kuolewa send off niihangaika mpk kufanikisha kwakua baba yao yupo busy sana.. Ila kilichokuja kutokea ukumbini sintosahau maisha ni... Of coz mama yao alifariki siku nyingi sana kabla Sijaelewa na bahati mbaya kwangu sijuwahi kumjua zaidi ya kumuona kwenye picha a.. Siku ya sendoff bint kabla ya kutanbukisha ndg zake alituomba tusimame dakika moja ili tukumbuke marehemu mama yake kwa sala fupi.. Si kuona vibaya ila kilichonitesa na kuniumiza ni msiba ulioibuka gafla pale ukumbini... Ndg wa mwanamke walilia Sana kiasi kwamba gumzo likaanza... Baadhi ya watu wengi walikuwa hawajui kama Hao si wanangu wa kuwazaa... Rafiki zangu na majira ni wengi walijua ni mwanangu... Imagine km wewe ungejisikiaje.. Sijuwahi kuwabagua wala kuwatenga nikijisika vibaya sana.. Na siku wahi kuwaona et wanalia au wanahuzuni wanamkumbuka mama yao ila siku hiyo nilishangaa sana... Najiuliza wamebaki wawili mmoja anamaliza fm four mwaka huu je nitaenda kwenye sherehe yake??

  Mwingine Amemaliza chuo kikuu mwaka huu je nitaanzaje kwenda kwenye graduation yake.. Yani heka heka zote nilizozifanya nyuma kumbe ilikua ziro??? Sina HAMU nashukuru Mungu sana wamekuwa wamejitambua nimewatoa mbali sana nisingependa penda kuja kuumia tena km siku hiyo.. Hata ikitokea mwingine akafunga ndoa kiu kweli nitasafiri kwa Muda... Kwakua mama wa kubwa na Wadogo wapo nitawaachia wakamilishe Hilo.. Lawama nilizozipata sintosahau kamwe
   
 8. Zurie

  Zurie JF-Expert Member

  #8
  Sep 14, 2016
  Joined: Jul 6, 2014
  Messages: 961
  Likes Received: 1,621
  Trophy Points: 180
  Mimi naomba kutofautiana na wewe. Sidhani kama alifanya vibaya, wala sidhani kama ni vibaya mtu kumlilia mzazi wake aliyefariki. Wewe una nafasi yako na marehemu ana yake. Hata ungewafanyia wema upi huwezi kuwa mama yao mzazi, na wana haki ya kumlilia hata kwa mayowe.

  Kwakweli naona ulipanick tu....hujawahi kuwabagua na wao sidhani km kumkumbuka mama yao ni kukubagua. Siamini unataka kuacha kwenda kwenye sherehe za watu unaowaita "wanao" kwa sababu tu watu walizua gumzo kujua kuwa si wanao. Unatakiwa uwe proud uliwalea vema bila ubaguzi hata watu hawakunotice ila usitegemee malipo ya kugeuzwa mama mzazi...wewe si mama yao mzazi na huwezi kuwa!
   
Loading...