Kwanini wazanzibari wengi weusi na machotara wanaikana asili yao

sky soldier

JF-Expert Member
Mar 30, 2020
5,408
19,032
Katika sehemu mbali mbali nimeona wazanzibar weusi na machotara wakikataa asili yao ya kutokea huku bara, sasa sijajua wanaukataa ukweli kwanini.

Hapo zamani wafanya biashara wa watumwa walifika visiwa vya zanzibar na kulikuwa na watu wenye asili ya kibantu wachache kwenye visiwa hivyo, hawa wafanya biashara wakaanza kuwatumia machifu na mamwinyi kuwauzia watumwa katika jamii zao na kisha kuwasafirisha kwenda nchi nyingine,

Kwa kuwa idadi yao ilikuwa ni ndogo, ikabidi wafanya biashara hao waje huku bara kutafuta soko jipya la kununua watumwa.

Sasa huku kwetu kulikuwa na makabila yalikuwa madogo ama hayana majeshi yenye nguvu, haya makabila mara nyingi yalikuwa yakipigwa basi mateka wa vita na wakimbizi waliokamatwa walikuwa wakiuzwa kwa wafanya biashara wa watumwa, Hata pale makabila makubwa yenye nguvu yalipopigana basi mateka na wakimbizi waliuzwa kwa wafanya biashara hawa.

Baada ya kuuzwa kwa wafanya biashara hawa, walisafirishwa kwenda zanzibar lilipokuwa soko mojawapo maarufu la watumwa walionunuliwa kwa bei ya juu na kupelekwa kufanya kazi amerika ya kusini, afrika ya kaskazini, n.k

Sasa kuna kipindi kilifika, kukawa na mashamba ya karafuu hapo zanzibar na ikaonekana ni vyema kutumia watumwa hao waliofika hapo zanzibar na kuwatumikisha katika mashamba badala ya kuwauza wote, Kwa hio baadhi wakifika zanzibar waliendelea kuuzwa kwenda nchi nyingine ila wengine walibaki katika mashamba ya karafuu.

Walikuwa ni ma elfu waliotumikishwa kwenye mashamba hayo, mazingira ya kazi yalikuwa magumu sana. Kazi zilifanywa kwa mijeredi, Watu walitukanwa, wengine kuuawa, wanawake walibakwa na kuzaa machotara, matibabu yalikuwa ya hali ya chini, n.k

Hata lugha zao asili walizotoka nazo huku , wengi wakaacha kutumia kabisa na kugeukia kiswahili na pia wengi waliacha kutumia majina yao ya ukoo waliyotoka nayo huku ikabidi waanza kutumia majina ya huko zanzibar, Wengi lugha yao ni kiswahili, lugha za kikabila ni shughuli pevu kuzikuta

Ni miaka mingi ilipita ya manyanyaso haya, ila kufikia mwisho ya miaka ya 1800, Muingereza alishinikiza kukoma kwa biashara hio haramu na hapa ndipo pakawa na nafuu,
 
So unaamini kabisa kabla ya waarabu zanzibar kulikua na kima tu hakukua na watu?

Unajua kwanin waarabu walipaita hapo Zanzibar

Back to your point wanakataa kuhusishwa na bara sababu wanataka kujitenga na hilo likifanikiwa majority watalia na kusaga meno huku wakimkumbuka kocha nyerere na minority wenye miziz mascut wataishi kama paradiso
 
Nyama ikigeuzwa kuwa supu sio nyama tena

Historia hii inauma sana hasa kwa hawa wenzetu wa pwani

Hawataki kusikia au kufundishwa kuhusu biashara za utumwa zilizofanywa na waarabu
 
Nyama ikigeuzwa kuwa supu sio nyama tena

Historia hii inauma sana hasa kwa hawa wenzetu wa pwani

Hawataki kusikia au kufundishwa kuhusu biashara za utumwa zilizofanywa na waarabu
wanakuambia mwarabu hakuhuska na biashara ya utumwa, kile kinachojulikana na wengi kuwa mwarabu alihuska ni ya uwongo uliotungwa na Westerners kuwafitnisha na ndugu zao katika Iman ya mnyazi mungu.
 
Yaani mtu mweusi tii, ana pua pana, lips pana na nywele fupi ngumu anajiita Mwarabu kama huyu FaizaFoxy wa humu

Kisa wameletewa Uislam na kuwa Waislam wanajiona sio watu weusi tena
Definition ya sasa ya Uarabu haiangalii rangi, Sudan kuna watu weusi tii na ni Waarabu. Kwa sasa ukiongea Kiarabu na kuwa na mila na tamaduni za kiarabu wewe ni mwarabu.
 
zanzibar = unguja + pemba., mimi binafsi naunga hoja yao ya kuwa na taifa lao huru.......then walioko huku bara warudi kwao, waje upya kama wawekezaji :cool: .........
 
Kitu kimoja ambacho hamtaki kukisema, mkiwapiga hao wazanzibari na kuwachagulia viongozi, mkiwaua na kuwanyima huduma zao za kimsingi wakikimbilia oman wanapokelewa na hawabaguliwi kama huku.

Oman Mzanzibari ana status kubwa kuliko huku,

Kabla ya kuwalaumu hao wapendeni kwanza nyie, msiwabague, msiwaite maneno mabaya, wapeni opportunity na mengine mengi.
 
Maada inahusu asili, fungua uzi mwengine

Acha kutuvunja mbavu aisee, Oman mzanzibar ana status kubwa kwa kipi 😂😂
 
Wana kitu gani kibaya au cha ajabu paka wabaguliwe mkuu??
 
Nyama ikigeuzwa kuwa supu sio nyama tena

Historia hii inauma sana hasa kwa hawa wenzetu wa pwani

Hawataki kusikia au kufundishwa kuhusu biashara za utumwa zilizofanywa na waarabu
Wth? wapi kulikuwa na afadhali?

Sijui kwanini nyie watu mko full of Condescendence.
 
Wana kitu gani kibaya au cha ajabu paka wabaguliwe mkuu??
Mkuu wapinzani bara wakiandamana watakuja tu FFU mabomu ya machozi ya aidha, Zanzibar wakiandamana watakodiwa hadi wanajeshi, si mabomu ya machozi tu yatakayotumika bali risasi za moto kuuana na kudhalilishana...

Angalia historia mkuu wanavyokuwa treated ni sawa?
 
wanakuambia mwarabu hakuhuska na biashara ya utumwa, kile kinachojulikana na wengi kuwa mwarabu alihuska ni ya uwongo uliotungwa na Westerners kuwafitnisha na ndugu zao katika Iman ya mnyazi mungu.
Mimi sio mtu wa dini but I gotta say tatizo liko wapi?

Nyie christians mnatetea wazungu vilevile, ninachokiona hapa ni kila mtumwa anatetea bwana wake.
huku kundi A likipinga kwamba bwana wake hakuhusika na utumwa na mwengine wazi'wazi akijua kwamba bwana wake amehusika na utumwa hivyo hili kundi B linaumia kwanini wanakataa wakati sisi bwana wetu alihusishwa na utumwa na hatukatai, ni lazima tuwe sawa.

while mimi nawaona wote ni bunch of braindeads and uncivilized idiots.
 
Maada inahusu asili, fungua uzi mwengine

Acha kutuvunja mbavu aisee, Oman mzanzibar ana status kubwa kwa kipi 😂😂
Ndo hio asili Muangalie tu GSM yeye ni Chotara wa kiarabu na mbongo hata asili yake ukimuangalia anaonekana kabisa ni mbantu, ila akitajwa wengi wana husisha na muarabu.

Waarabu wanajali damu zao, ila Bongo hawajali,

Na oman wazanzibari na weusi kibao wapo na wana status kubwa tu kama hujui uliza utaoneshwa na kuambiwa.
 
Back
Top Bottom