Kwanini Waumini wengi tukitoka Kanisani tunasahau Injili ya siku?

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Jul 13, 2013
59,949
119,214
Ni jambao la kushangaza sana na ambalo sasa linaota ' mizizi ' ambapo unaweza kuwakuta ' Waumini ' wakiwa makini kabisa Makanisani wanasikiliza neno la Mungu ( Injili ) tena wakiwa ' wanamkodolea ' kabisa Mchungaji au Baba Paroko lakini cha ajabu mkiwa mmemaliza Ibada na mnatoka nje ukimuuliza Mtu yule yule kuwa ' Injili ' ilikuwa nini anakuambia amesahau.

Sasa nawaulizeni hivi humu Makanisani huwa tunaenda kweli Kusali na kusikiliza neno ' Injili ' au tunaenda tu kupoteza muda na kusindikiza Waumini wa kweli?

Nitashukuru nikijibiwa.
 
Wengi wetu tumefanya ibada kama kamtindo ka kila jumapili, hatutafakari neno b4 ya jumapili na siku ya jumapili hatuko tayari kutafakari zaidi ya kufata utaratibu wa ibada na kuondoka
 
Wengi tunaenda ili kuonekana kuwa tunaenda church.......kuna wakati mpaka niliona noma nimeenda church na mwimbieni bwana ya zamani kumbe vimeshabadilishwa...
 
Usione watu wanamkodolea macho mchungaji kwa umakini wengi wanakua mbali kimawazo,
Kama ungekua na uwezo wa kuona yale binadamu awazayo
Wengi ungekuta wapo bar, gesti, ofisini n.k
 
Ni jambao la kushangaza sana na ambalo sasa linaota ' mizizi ' ambapo unaweza kuwakuta ' Waumini ' wakiwa makini kabisa Makanisani wanasikiliza neno la Mungu ( Injili ) tena wakiwa ' wanamkodolea ' kabisa Mchungaji au Baba Paroko lakini cha ajabu mkiwa mmemaliza Ibada na mnatoka nje ukimuuliza Mtu yule yule kuwa ' Injili ' ilikuwa nini anakuambia amesahau.

Sasa nawaulizeni hivi humu Makanisani huwa tunaenda kweli Kusali na kusikiliza neno ' Injili ' au tunaenda tu kupoteza muda na kusindikiza Waumini wa kweli?

Nitashukuru nikijibiwa.

Kwa sababu Tanzania wanaojiita Wakristo zaidi ya 80% ni Wakristo jina tu, hawaelewi chochote kuhusu Ukristo, na wengi wao wanakwenda Kanisani kama kutimiza wajibu tu ili waonekane walikuwa Kanisani, na ndiyo maana zaidi ya 90% ukisimama mlangoni na kuwauliza Misa ya leo ilihusu nini au hata tu ni Jumapili ya ngapi ya mwaka hakuna atakayekupa jibu ingawaje ndiyo kwanza Misa imeisha!!
 
Wengi wanaenda kutimiza tu utaratibu wa jumapili
wapo makanisani ili waonekane wamo tu
Wengi hawazingatii neno,
 
Kanisa zuri mtu anatoka hata usoni anaonekana kufurahi ana uchangamfu na anatamani arudi. Mengine mtu anaingia anatoka na stress zaidi kwasababu kilichosisitizwa ni Michango tu
 
Ni jambao la kushangaza sana na ambalo sasa linaota ' mizizi ' ambapo unaweza kuwakuta ' Waumini ' wakiwa makini kabisa Makanisani wanasikiliza neno la Mungu ( Injili ) tena wakiwa ' wanamkodolea ' kabisa Mchungaji au Baba Paroko lakini cha ajabu mkiwa mmemaliza Ibada na mnatoka nje ukimuuliza Mtu yule yule kuwa ' Injili ' ilikuwa nini anakuambia amesahau.

Sasa nawaulizeni hivi humu Makanisani huwa tunaenda kweli Kusali na kusikiliza neno ' Injili ' au tunaenda tu kupoteza muda na kusindikiza Waumini wa kweli?

Nitashukuru nikijibiwa.

Kitu ambacho wakristo wengi hawajakijua ni kuwa falme mbili kati ya MUNGU na Shetani wangombea utawala wa ulimwengu, Mungu kupitia watumishi wake anajaribu kuleta kweli machoni kwa wakristo lakini shetani anatumia mbinu zisizomithilika kuzuia kweli isije ikawazukia na wakatawala ulimwengu. Wakristo wenye kweli ya MUNGUwakitawala ulimwengu MUNGU ametawala, na wakiristo legelege+wasiomcha MUNGU wakitawala sawa na kuwashetani ametwala ulimwengu.
Na ndiyo maana ni rahisi tu mtu kulala kanisani, au kuchat na wakati mwingine kutongozana na nk. hebu jiulize kweli siku moja yesu asimamae madhabahuni yeye mwenyewe anaongea ana kwa ana tutapata muda wa kufanya upumbavu kama huo?, lakini shetani anatudanganya kuwa anaeongea madhabahuni ni mtu wa kawaida tuu na tunaamini, lakini MUNGU anasema akiongea mtumishi wake yeye ndio kaongea. Hivyo hutupati maarifa ya KIMUNGU kwa sababu tunadharau waongeayo watumishi.

Kusikiliza au kusoma neneo la Mungu ni vita kali kuliko bomu la nyuklia, Dunia imeumbwa watu waishi kwa kusikia Neno la MUNGU maana ndilo lenye maelekezo na mipango yote ya maisha yako. Hivyo kumzuia mtu kumsikiliza MUNGU anachoongea ni kumtawala kabisa milele na ndicho shetania anachofanya.Matayo 13.19 Mtu anaposikia neno la Ufalme na asilielewe, yule mwovu huja na kunyakua kile kilichopandwa moyoni mwake; hii ndio mbegu iliyopandwa njiani.
Hii ndiyo sababu kubwa inayofanya watu kusahahau kile walichojifunza, lakini matukio mwengine wanayakumbuka sana ndani ya ibaada hiyohiyo, na ndiyo maana ukipaanga ratiba ya kusoma bible usipokoma utafanya siku tatu za kwanza kisha unasahau kimoja.

Kwa asili kila unaposoma au kusikia neno la MUNGU unakuwa informed, nuru inaongezeka rohoni unapta nguvu sana, unapata nguvu ya kuucontrol mwili kufuata mapenzi ya Mungu pia unaanza kujua siri za MUNGU juu ya Maisha yako na kuna level ukifika ni ngumu sna shetani kukushinda hivyo anapambana kukuzuia mapema kabla hujkiti mizizi ili uwe wake na akuongoze milele.

Na ndiyo maana mkristo usiridhike kwenda kanisani, chunga umesikia nini na umedaka vingapi ilikukuvusha maisha yako. ukiona umekwenda kanisani halafu huoni hamu mabadiliko ya rohoni jichunguze sana unajaribu kucheza ngoma na muziki wa shetani ndani ya ukuta wa kanisa la MUNGU
 
Usione watu wanamkodolea macho mchungaji kwa umakini wengi wanakua mbali kimawazo,
Kama ungekua na uwezo wa kuona yale binadamu awazayo
Wengi ungekuta wapo bar, gesti, ofisini n.k

Mkuu post yako hii imenifanya nicheke sana. Akhsante kwa kuniongezea siku za kuishi kwa kunifanya nifurahi.
 
Kanisa zuri mtu anatoka hata usoni anaonekana kufurahi ana uchangamfu na anatamani arudi. Mengine mtu anaingia anatoka na stress zaidi kwasababu kilichosisitizwa ni Michango tu

Jamani basi mtaniua huku kwa Kucheka na hizi posts zenu. Kuna Watu humu JF mna vituko sana hadi raha.
 
Mtu anaenda kanisani kama ana enda disco Hana biblia wala kijitabu cha kuandikia neno...sa hapo mkuu unategemea nn?
 
Back
Top Bottom