Kwanini watumishi wa ambulance wasafirishapo mgonjwa hukaa mbele wamepiga vishoka?

tutafikatu

JF-Expert Member
Dec 17, 2011
3,198
4,376
Kwa uelewa wangu mdogo, ambulance (nazungumizia gari) ni gari lenye vifaa vya matibabu ambalo hutumika na watumishi wa afya kusafirisha wagonjwa kwenda kwenye vituo vya matibabu vinavyoweza toa huduma za juu ukilinganisha na huduma inayoweza tolewa mgonjwa anapohamishwa.

Kawaida mgonjwa aliyepo kwenye ambulance huwa anapaswa kupata uangalizi wa karibu na hata matibabu ndani ya gari wakiwa njiani kupelekwa kwenye kituo cha juu. Jambo la ajabu sana, mara nyingi hapa Tanzania mgonjwa anaposafirishwa ndugu za mgonjwa ambao hupewa lifti hukaa nyuma na mgonjwa, huku dereva na mhudumu mwingine mwenye uelewa zaidi ya dereva wakiwa mbele amepiga kishoka.

Nadhani hili jambo linapaswa lirekebishwe kwa sababu huhitaji rocket science kutambua makosa kama haya.


p1100138.jpg

Picha haina uhusiano na bandiko
 
Weka picha...wewe umezoea kuyaona magari ya wagonjwa yakienda kuchukua wagonjwa au wakiwa wanatoka kuwapeleka wagonjwa vinginevyo mhudumju anakuwa karibu na mgonjwa! Period.
 
Tuna mgonjwa home ambaye anabebwa na hizo gari mara kwa mara,sijaona mhudumu akikaa na dereva ilihali kuna mgonjwa, lazima akae na mgonjwa
 
2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom