Kwanini Watumishi na ldara ya Usalama wa Taifa Wanaogopwa SANA?

Status
Not open for further replies.

Sumbalawinyo

JF-Expert Member
Sep 22, 2009
1,282
247
Watanzania wanawaogopa sana watumishi wa ldara ya usalama wa taifa.
mkikaa kwenye vikao vya pombe, mtu akinyoosha kidole kuwa yule fulani ni afisa usalama, amani inatoweka, mazungumzo yanabadilika na hofu inatanda.
nasikia hapa Jamii Forums watu wanaogopa kutumia majina na wasifu wao kamili kwa kuwahofia wana Usalama wa taifa.
Je kwanini usalama wataifa waogopwe kiasi hiki?
 
kwa sababu ya ushahidi uliopo wa wao kuwalinda viongozi hata kama ni wachafu kiasi gani na vile vile wakishakujua kuwa unaisema serikali (ikifanya madudu) wanakufuatilia mpaka unatamani kuuvua uraia wako.

Hii TISS mie nina mashaka nayo sana kama wanaenda sawa na viapo vyao vya kulinda ustawi wa taifa letu. Wanapaswa kuboreshwa zaidi waende na wakati kwani zama za makaburu na wahujumu zimepita sasa ni mafisadi na wauza nchi. huko marekani CIA wanaweza kumtoa rais madarakani (kupitia bunge) endapo atakwenda kinyume na ustawi wa taifa lao kimaadili hivyo wataanika ushahidi dhidi yake peupee ili awajibike au awajibishwe.

Kukubali kuwa kiongozi si fadhila ni dhamana na lazima UWAJIBIKE ukienda jojo
 
kwa taarifa yako
walipowakamata baadhi ya staff wa JF miaka miwili nyuma walikuwa na lengo la kupata data za members wa JF ili iweje? Suala lenye ushahidi la DEEP Green, meremeta na taka taka zinginezo kwa nini wanazifumbia macho ilhali ni kodi zetu halali?

Tupo macho. kama wao walienda mafunzo ya kiushushushu sisi wengine tumezaliwa na vipaji vya kiushushushu ingawa kareti zao ni value added .
 
Watanzania wanawaogopa sana watumishi wa ldara ya usalama wa taifa.
mkikaa kwenye vikao vya pombe, mtu akinyoosha kidole kuwa yule fulani ni afisa usalama, amani inatoweka, mazungumzo yanabadilika na hofu inatanda.
nasikia hapa Jamii Forums watu wanaogopa kutumia majina na wasifu wao kamili kwa kuwahofia wana Usalama wa taifa.
Je kwanini usalama wataifa waogopwe kiasi hiki?

Uzuri mmoja hata wewe Sumbalawinyo umeogopa kutumia jina lako halisi!!!!! Kwa nini unawaogopa wana usalama wa Taifa kiasi hiki?? Hebu tupe jibu la hili nasi tutajitahidi kujitutumua kutoa majibu ya swali lako!!
 
Kuna sehemu ambazo hao usalama wa taifa hawapo, kuna sungusungu, mgambo na polisi.
Lakini majeshi hayo yana mamlaka makubwa sana ambapo huwa wanapiga watu, wanapora mali za watu, wanatesa na kusulubu.
Majeshi haya yanatisha sana, raia wanawaogopa sana.
Taifa letu limeundwa kwenye misingi ya nidhamu ya woga ndio maana kuendelea kwetu ni ndoto.
Watu ni waoga hata kuulizia haki zao za msingi.
 
uzuri mmoja hata wewe sumbalawinyo umeogopa kutumia jina lako halisi!!!!! Kwa nini unawaogopa wana usalama wa taifa kiasi hiki?? Hebu tupe jibu la hili nasi tutajitahidi kujitutumua kutoa majibu ya swali lako!!

sumbalawinyo ni jina langu halisi,
wanaonifahamu tangu nikiwa mdogo wanaiita sumba.
Ila nilipofikia ile miaka ya kujitambua nikawa naliona kama limekaa kilugaluga sana,
nikaanza kujiita cool boy sumba,
jina kool boy lilivuma sana.
Ni hayo tu kaka.
 
nani anapendelea ghasia za watu wambeya wambeya? Lol
Anyway mi natumia jina langu halisi
 
Usalama wamejivunjia hadhi yao siku hizi baada ya kufanya kazi binafsi za watawala badala ya maslahi ya nchi. Unapoona mafisadi wanaogopwa na kuendelea kupewa vyeo serikalini, then ujue kuwa usalama wa taifa umekufa.
 
Tatizo la intelligencia yetu ni kwamba hakuna kitengo cha economic intelligence ndiyo maana ktk hilo tumekwama. Kuhusu kuogopwa, siyo kweli kwamba wananchi wote wanawaogopa wafanyakazi wa idara ya usalama wa taifa, tatizo ni kwamba hawa watu wanatishia sana wananchi tena kwa bunduki ambazo wamepewa kufanyia kazi.

Kioja cha ajabu ni kwamba hawa jamaa ni waoga sana; mwaka 2005 majambazi wa kutumia silaha walivamia baa moja hivi wakaua na nilikuwa nimekaa na kijana mmoja mtu mzima kiasi na namjua ni afisa ktk idara yetu ya usalama lakini wote tulifanikiwa kutimua mbiyo kwa nguvu za MUNGU na ilihali yeye alikuwa na bastola mfukoni.
 
kioja cha ajabu ni kwamba hawa jamaa ni waoga sana; mwaka 2005 majambazi wa kutumia silaha walivamia baa moja hivi wakaua na nilikuwa nimekaa na kijana mmoja mtu mzima kiasi na namjua ni afisa ktk idara yetu ya usalama lakini wote tulifanikiwa kutimua mbiyo kwa nguvu za mungu na ilihali yeye alikuwa na bastola mfukoni.

kweli wanajeshi shupavu tunao. Dah!!
 
Watanzania wanawaogopa sana watumishi wa ldara ya usalama wa taifa.
mkikaa kwenye vikao vya pombe, mtu akinyoosha kidole kuwa yule fulani ni afisa usalama, amani inatoweka, mazungumzo yanabadilika na hofu inatanda.
nasikia hapa Jamii Forums watu wanaogopa kutumia majina na wasifu wao kamili kwa kuwahofia wana Usalama wa taifa.
Je kwanini usalama wataifa waogopwe kiasi hiki?

Kwa sababu hawa jamaa ili kujionyesha kama ni Watendaji wazuri wa kazi zao wanaweza kukubambikia lolote lile la kuonyesha kwamba unataka kuharibu usalama wa Taifa. Na hapo maisha yako yote watakuwa wameyaharibu kabisa maana unaweza kusoteshwa mpaka ukajuta kuzaliwa.
 
Watanzania wanawaogopa sana watumishi wa ldara ya usalama wa taifa.
mkikaa kwenye vikao vya pombe, mtu akinyoosha kidole kuwa yule fulani ni afisa usalama, amani inatoweka, mazungumzo yanabadilika na hofu inatanda.
nasikia hapa Jamii Forums watu wanaogopa kutumia majina na wasifu wao kamili kwa kuwahofia wana Usalama wa taifa.
Je kwanini usalama wataifa waogopwe kiasi hiki?

Hapana sio kweli....Wapo wengi tu wana JF ambao ni usalama wa Taifa, sasa wana JF tukitumia majina yetu halisi tutashindwa kumwaga Nyanga za kutosha kiulaini...
 
Kioja kingine ilikuwa kukiwa na migomo pale UDSM hawa jamaa walikuwa wanatumia nafasi ile kupata posho kwa kudanganya wakubwa wao kuwa kuna wanafunzi wanaandaa mabomu na hiyo wanatidhia usalama wa nchi kumbe ni maskini watoto wa wakulima wana njaa.
 
Kioja cha ajabu ni kwamba hawa jamaa ni waoga sana; mwaka 2005 majambazi wa kutumia silaha walivamia baa moja hivi wakaua na nilikuwa nimekaa na kijana mmoja mtu mzima kiasi na namjua ni afisa ktk idara yetu ya usalama lakini wote tulifanikiwa kutimua mbiyo kwa nguvu za MUNGU na ilihali yeye alikuwa na bastola mfukoni.

Mkuu huyo jamaa alikuwa sahihi sana, kwa kawaida majambazi wanapovamia sehemu inabidi ujue kwanza wana silaha za aina gani. sasa watu wamekuja na AK 47 unataka kupambananao na kibastola chako cha mrusi cha mwaka 1947. hapo ni kutimua mbio tu...
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom