matunduizi
JF-Expert Member
- Aug 20, 2018
- 6,571
- 15,321
Wakuu nimefanya utafii uchwara nimegundua
Watu wenye viherehere, wanaojiongeza nje ya majukumu yao, wanaoongea kwa ujasiri na kujiamini mambo ambayo hawayafahamu vizuri ni rahisi kufanikiwa.
Nimeona watu wa namba hii katika mazingira tofauti zaidi ya watu kumi.
USHAURI NINI UFANYE.
1:Usiwe na aibu za kijinga, jiongeze kuwa mwepesi wa kupata habari na taarifa sahihi zieleze kwa watu wenye ushawishi, Wenye vyeo, wenye pesa kwa ujasiri mkuu kana kwamba wewe ulikuwepo.
2: Usiwaamrishe wape kama mapendekezo nini kifanyike. Wakipata majanga na matatizo kuwa wa kwanza kuwapa pole, Shiriki katika mazishi, kuchimba makaburi, kubeba majeneza.
3: Kama unauweza pendeza sana unapokutana na watu wenye ushawishi. au unapotaka kufanikiwa katikati ya watu wa kawaida ili uaminike. Siku zote napanda mabus jamaa wanakusanya sadaka wa (wahubiri kwenye mabasi), Ila Juzi kapanda jamaa mmoja mchaga kapiga suti kali, kaongea kwa kujiamini sana kana kwamba hana shida, alipokusanya sadaka alikomba za kutosha basi zima.
4: Uwe makini katika kiherehere na kujiongeza usichongee watu au kuwasema vibaya sana maana unaweza kweli kufanikiwa lakn kwa Mta mfupi utafeli.
5: Ufurahie watu. Yaani ukikutana na mtu mfurahie mchangamkie kana kwamba mnamiaka mingi mnafahamiana japo hamjuani. Utakokota maelfu.
6: Ongea maneno yatamkike na kusikika kila herufi. Pia Ongea kwa mtazamo wa kutoa suluhisho hata kama ni la uongo.
7: Kuna watu wanaakili za kizamani eti kama ni Muhasibu basi hataki kujua kinachoendelea engineering, sheria, etc. utakufa Muhasibu. Ila sifa ya kiongozi ni kujua mambo hata kwa kupapasa kutoka katika almost kila tasnia. Mtu anayejiongeza nje ya eneo lake huaminiwa mapema kuwa kiongozi mahali popote.
hizi mbinu na za ziada ukijaribu huwezi kulala njaa...
ongeza na zako