Kwanini watu wenye roho nzuri huwa hawatajiriki?

OMOYOGWANE

JF-Expert Member
Dec 30, 2016
3,602
9,066
NB: Dhumuni la maada hii sio kufundisha watu roho mbaya bali ni swali ambalo nakuuliza kwa lengo la kupata maarifa,

Wakuu mwenye jibu atuwekee hapa,

Kwanini watu wenye roho nzuri wengi wao hufa masikini, na huwa hawatajiriki kabisa tofauti na wale wenye roho mbaya ?
 
Utajiri unaoungalea wewe ni upi?

Wenye roho nzuri ni matajiri wa imani, upendo na watu zaidi ya utajiri wengi wanaouthamini wa pesa na mali
Wakati wale wasio na roho nzuri huthamini vitu peke yake na utajiri walio nao ni utajiri wa vitu, wanaweza kuwa na utajiri wa watu ila sio kwa upendo bali kwa maslahi yao binafsi
 
Utajiri wa mali (ukwasi)

Haya jibu swali kama hutojali
 
Kwa sababu huwa tunagawa vitu vingi vya thamani kubwa bure wakati wengine huviuza.. Nilishawahi kwenda kwa mwanasheria mmoja kumuomba anigongee muhuri kwa sh elf tatu akakataa kata kata hadi niwe na elfu tano.. Unaona sasa, mtu anakunyima tu wino kisa umepungukiwa buku mbili je ni kitu gani kingine anaweza kukupa bure?
 
Back
Top Bottom