Kwanini watu wengi wanaoishi Dar, hawapendi ndugu zao wanaoishi mikoani?

Mkuu samahani wewe una ndugu wa ngap huko Dar ambao wameonyesha kutokupenda
 
Sio kwamba hawawapendi ila hali zao hapa mjini ni ngumu na nyie mkoani mkijua mtu yupo dar mnahisi tu ni mambo safi
Mtu akiwa dar hawezi kutamani hata ndugu yake uje umtembelee kwahiyo lazima utahisi ana roho mbaya au hakupendi kumbe ni hali tu ya maisha

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Maisha yanabadilika na hivyo jifunze kubadilika pia mambo ya kujenga chuki na majungu kwa ndugu yako hayakusaidii kitu
 
Ni wewe na ndugu zako ndiyo hampendani.

Wenzio tunapendana na ndugu, jamaa na marafiki zetu walio mikoani.

I moved your cheese!
 
Nyie wenyewe hamtupendi wa Dar. Sema mnataka kujisogeza ili mje huku.
 
Kila mtu ana ndugu dar

Kila mtu anaishi au alishawahi kuishi dar

Kila mtu anaenda au anasafiri dar maisha mikoani yakimpiga

Ametia mimba mwanafunzi huku misungwi mwanza kakimbilia dar

Bodaboda mtaani wamekata watu mapanga wamekimbia dar kuepuka msala

Shule zimefungwa au chuo eti naenda dar kwa sister

Mwanangu hauna kazi unajishindwa hata kwenda kuwa mwizi dar "utawaskia wazee wakisema

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sababu zaweza kuwa nyingi:

Mfano;

Choyo,

Wengine wanakwepa husuda na maneno Maneno yatakayosambaa kwa ndugu na watu bali

Ndugu Wengine wachawi au mama zao wakijua mna Neema nyumbani wanatafuta kukuharibia

Kuishi na watu au mgeni kuna udhia mwingi.

Cha msingi maisha ni popote yanawwza kuchanua bora kufanya kazi kwa bidii.

Kuna watu wanalima lakini maisha yao mazuri wanabadilisha milo na mboga wakiwa vijijini na hawamlaumu ndugu yeyote aliepo Dar

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wewe achana na watu wa Dar, utaonana nao December wakija huko mikoani! Fanya kazi kwa bidii mpaka watu wa Dar wakutafute wenyewe
 
Kila mtu ana ndugu dar

Kila mtu anaishi au alishawahi kuishi dar

Kila mtu anaenda au anasafiri dar maisha mikoani yakimpiga

Ametia mimba mwanafunzi huku misungwi mwanza kakimbilia dar

Bodaboda mtaani wamekata watu mapanga wamekimbia dar kuepuka msala

Shule zimefungwa au chuo eti naenda dar kwa sister

Mwanangu hauna kazi unajishindwa hata kwenda kuwa mwizi dar "utawaskia wazee wakisema

Sent using Jamii Forums mobile app
Hakuna mzee anayeweza kusema hivyo.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom