Kwanini watu wengi wakistaafu hurudi kwao japo huko waliondoka siku nyingi?

Nadhani kikubwa ni shughuli ya kiuchumi au kijamii uliyokuwa unaifanya muda ambao hauko ofisini

kama hukuwa na lolote mtaani lazma urudi bush walau ukaoshe macho su kupunguza gharama za maisha

sio siri ni muhimu sana kujishughulisha na kazi ama biashara flani flani nje ya maofisi
 
Jiulize Kwanini wazungu walikuja kuvuna kwetu wakapeleka kwao wakaijenga ulaya.Jiulize Kwanini mzungu akifa huku anapelekwa kwao kuzikwa.
Ukiona kabila lolote hawapendi kwao basi na maendeleo yao ni duni sana.Sanasana ni wachawi anaogopa akijenga akipiga bati tu halali.Nimeshafika mkoa mmoja nikaona gari nje la mil260.Nyumba nzuri ya tofali juu dishi lakini imeezekwa kwa majani.
Hawa wachaga sio wajinga wajinga ni sisi tunaowacheka.Mkoa pekee wenye barabara za lami baada ya Uhuru ni kilimanjaro.Ujinga wao tunavyoona ndio maendeleo yao.
Ila la maana kwa sasa sababu Nyerere alifuta ukabila Tanzania imekuwa moja iko miaka let say miaka 500 ijayo lugha zote za makabila tunazoongea zitakufa kama ilivyo kwa Marekani na Wingereza.hivyo ule ulazima wa kuzikwa kijijini kwenu utakufa wachaga watabadilika

Sent using Jamii Forums mobile app
Wati wengine mnavofikiri bana

Ss hio baada ya uhuru walijenga wananchi na greda zao hizo barabara au ni pesa za serikali ndo zilipelekwa na zimejenga hizo lami?..


lami saivi nchini ni ishu tena?.

labda kabila lenu wangewahi kupata wamishenari mapema mkaenda shule mngekua viongozi serikalini mapema mkapeleka lami kwenu kwanzA kabla ya mikoa mingine
 
Wadau wa JF hongereni kwa sikukuu ya Christmas.

Mada hapo juu yajifafanua vizuri. Watu wengi ikiwa ni pamoja na watumishi, wanasiasa nk wakistaafu shughuli zao hurudi kwao. Huko warudipo walishaondoka siku nyingi sana na hurudi wakati wa likizo na dharura mbalimbali. Sasa cha kujiuliza mtu amejenga mahekalu maeneo mbalimbali lakini huyaacha na kurudi Nyumbani kwao kijijijini au mjini kisa huwa nini?

Wanamuduje mfumo mpya wa maisha na jamii mpya tofauti?
Mkuu si ungejipa tu homework hapo hapo homen kwenu ukamwuliza Mzee wako?
 
sheria ya utumishi ukistaafu unapewa nauli ya kurudi kwenu pamoja na kusafirisha mizigo yako na familia na hivyo uliporipoti kazini ulilipwa nauli na pesa ya kujikimu wewe na familia yako mwisho ukimaliza utumishi unarudi kule ulikosema unatokea nadhani mwajiri anaamini kuwa inabidi akugharimie urudi kule alikokutoa ulipokuja kazini labda ndiyo sababu kubwa watumishi wengi huwaza kurudi kwao .
Has a polisi na majeshi mengine
 
Amerudi Nyumbani ndiyo nikawaza hivi kwanini wastaafu hurudi kwenye maisha hayo ambayo ni mapya
Ndiyo maana mkuu nikasema ungejipa homework ukamhoji vizuri kwa nini aliamua kuondoka town kwenda kuanza maisha mapya kijijini? Huenda kuna sababu za msingi!
 
Hivi kwani lazima uzikwe kijijini kwenu?
Si uzikwe hapo hapo unapoishi sasa hivi(mjini or kijijini) ...ili kuepusha gharama na kama umejenga nyumba ndo utazikiwa kwa hiyo(kwa hiyo concept ya kujenga utapozikwa)

Sent using Jamii Forums mobile app
Makaburi mengi ya mjini yanafukuliwa mkuu, maendeleo ya binadamu yanafanya maiti zisiwe na thamani tena,
Ni bora mtu ukizikwe kwenu, mfano bibi yangu tulimzika mjini ila mpk hii leo pale walitanua barabara hivyo kaburi halipo tena

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wadau wa JF hongereni kwa sikukuu ya Christmas.

Mada hapo juu yajifafanua vizuri. Watu wengi ikiwa ni pamoja na watumishi, wanasiasa nk wakistaafu shughuli zao hurudi kwao. Huko warudipo walishaondoka siku nyingi sana na hurudi wakati wa likizo na dharura mbalimbali. Sasa cha kujiuliza mtu amejenga mahekalu maeneo mbalimbali lakini huyaacha na kurudi Nyumbani kwao kijijijini au mjini kisa huwa nini?

Wanamuduje mfumo mpya wa maisha na jamii mpya tofauti?
Anakuwa amebakiza 20% yakutumia nguvu zake. Na ndio maana anahisi bora akazitumikie kwao. Hata kwa kuuza nyanya na biringani.
 
Na m
mnavyojitengaga ama kujubagua kikabila mpaka huko huko Moshi mnaanza kubaguana Mara huyu mmarangu akaweka wamarangu wote kwa hii sekta mbona hakuna wakibosho,wauru,wamachame,wa old Moshi, wa uru, wakishumundu,yaani wilaya moja INA makabila karibia nane, mmeshindwa kwa kubaguana mkiwa huko huko.
Aliyekula nyama ya MTU haijawahi muacha salama.
Mkuu mbona unaweweseka, hao watu wamekufanyaje?

Ulichokiandika kiko nje ya mada kabisa.
 
Yaani hao , huwa hawajielewi tu utaendaje nyumbani tena ???wakati unaenda kuonekana mgeni wote uliokuwa nao hawapo

Hizo mambo za kizamani tena mm nimepanga nikipata kiinua mgongo changu naenda kuishi kwenye jiji moja nalipenda sana

Lkn si kwa kuniambia nirudi nyumban kufanya nn sasa huko !!!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Makaburi mengi ya mjini yanafukuliwa mkuu, maendeleo ya binadamu yanafanya maiti zisiwe na thamani tena,
Ni bora mtu ukizikwe kwenu, mfano bibi yangu tulimzika mjini ila mpk hii leo pale walitanua barabara hivyo kaburi halipo tena

Sent using Jamii Forums mobile app
Sio ishu,hata uzikiwe kijijini,baada ya miaka 100,kaburi halipo
 
Mimi ni mmoja wa watu walio na mpango wa kurudi kijijini kwao baada ya kustaafu. Kama kufanya hivyo ni ushamba niiteni vyovyote mtakavyoniita na wala sitojali.

Kwanini nimepanga kurudi nyumbani (kijijini) baada ya kustaafu?

1.Wengi tunajua kuwa mtu anapozeeka kumbukumbu za zamani, utotoni humrejea kwa kasi sana. Ndo maana kuna nyakati wazee hu-act childishly. Sasa nataka nikare-experience maisha hayo ya utotoni kwenye mazingira halisi nilipoishi nikiwa mtoto. Uzeeni mtu hu-flash back mwanzo wa maisha, kumbukumbu za wazazi wako, marafiki wa utotoni, majirani na village life as a whole hurejea kwa kasi kichwani. Narudi nyumbani...

2.Binafsi huwa najisikia vyema nirudipo likizo nyumbani. Na watu husema 'jambo unalopenda kufanya ukiwa likizoni ndo unalotakiwa kulifanya baada ya kustaafu'. Ndio maana huwa napenda kwenda likizo kijijini kwetu.

3.Nikifa napenda nizikwe karibu na wazazi wangu, na likely by 60 nitakuwa nimekaribia 'kurudisha mpira kwa kipa', death becomes real. Ndio maana kila likizo lazima nitembelee mahala ancestors wangu walizikwa na kupafanyia usafi inapobidi.

4.Village life is cheap! na kama mstaafu nitatakiwa kuwa makini na matumizi yangu. Vitu vingi ni bei chee! Fikiria bei za matunda, mboga mboga na nafaka kule Mbeya,n.k. Uzeeni natakiwa kula mlo wenye afya (matunda na mboga mboga kwa wingi), nikienda kuishi Mbeya, Njombe, Tarime, Kilimanjaro,n.k nitavipata kwa bei cheee kabisa!

5.Uzee unahitaji utulivu bwana! Hizi kelele za magari na kumbi za starehe si vitu wazee tunapenda. Purukushani za vijana wa mjini nazo ni taabu kwetu wazee. Halafu above 60 ni vigumu kwa mzee kuendana na hustle za mjini, believe it or not. Inatuwia vigumu sana sisi wazee kwenda sambamba na mabadiliko ya haraka ya mjini (lifestyles, language za vijana, etc).

Hadi sasa maandalizi yangu ya kuanza maisha ya kustaafu kijijini yakoje?

- Nitastaafu miaka 10+ ijayo. Sikutaka kujenga kwenye viwanja vya familia, ambavyo ni vingi tu, bali nilinunua uwanja wa almost ekari 2. Humo nimejenga nyumba yangu na nimepanda miti ya matunda kidogo na ya vivuli. Hivi karibuni nitamtuma gardener akanitengenezee bustani. Sipendi maisha ya mjini ya kujibanabana kwa space ndogo. Nataka niishi kwenye Village paradise kama Le Grand Villa.

-Nina ekari 78 kwa ajili ya kilimo cha mpunga na mazao mengine, bila kusahau ufugaji wa kuku wa kienyeji.

MWISHO! Kama kuna wimbo unanivutia basi ni ule uitwao 'NARUDI NYUMBANI' ulioimbwa na Hayati Dr.REMMY ONGALA wenye kibwagizo:

"🎼 I want to home, I need to go back home.
The place that is our home,
Good hopes are still home...

Narudi Matimila, Remmy Oooh narudi Kinshasa.
Eeeeh, narudi Songea. Oooh narudi Majimaji..🎼🎹🎻"
 
Wadau wa JF hongereni kwa sikukuu ya Christmas.

Mada hapo juu yajifafanua vizuri. Watu wengi ikiwa ni pamoja na watumishi, wanasiasa nk wakistaafu shughuli zao hurudi kwao. Huko warudipo walishaondoka siku nyingi sana na hurudi wakati wa likizo na dharura mbalimbali. Sasa cha kujiuliza mtu amejenga mahekalu maeneo mbalimbali lakini huyaacha na kurudi Nyumbani kwao kijijijini au mjini kisa huwa nini?

Wanamuduje mfumo mpya wa maisha na jamii mpya tofauti?
Pamoja na kujenga nyumba nzuri kama huna kipato cha kueleweka unaweza kuadhirika mjini. Bora urudi kijijini ambako maisha no rahisi.
 
Sio ishu,hata uzikiwe kijijini,baada ya miaka 100,kaburi halipo
Nashanga wale watafiti kule Egypt wamefukua miili iliyozikwa miaka elfu sita iliyopita na bado imefunikwa sanda huku majeneza yakiwa imara kabisa
 
Back
Top Bottom