Kwanini watu wengi wakistaafu hurudi kwao japo huko waliondoka siku nyingi?

Freed Freed

JF-Expert Member
Jun 27, 2017
6,221
6,461
Wadau wa JF hongereni kwa sikukuu ya Christmas.

Mada hapo juu yajifafanua vizuri. Watu wengi ikiwa ni pamoja na watumishi, wanasiasa nk wakistaafu shughuli zao hurudi kwao. Huko warudipo walishaondoka siku nyingi sana na hurudi wakati wa likizo na dharura mbalimbali. Sasa cha kujiuliza mtu amejenga mahekalu maeneo mbalimbali lakini huyaacha na kurudi Nyumbani kwao kijijijini au mjini kisa huwa nini?

Wanamuduje mfumo mpya wa maisha na jamii mpya tofauti?
 
Ondoa kabila la wachagga...haa sasa hv enzi hizi za ujana wetu tupo mgomabni!
 
Huwa ni maandalizi ya kukipokeavifo vyao,hivyo wanapunguza gharama za usafirishaji Wa mwili pindi tamati zao hapa duniani zikishafika
 
Marais Nyrere, kikwete na wafanyakazi mbalimbali serikalini na sekta binafsi.
Wanarudi makwao kwa sababu muda wao wa utumishi wa umma umeisha, hana tena majukumu ya kila siku ofisini. Hii ni kutokana na kuwa hawezi kuwa Rais, waziri, mkurugenzi, meneja au katibu mkuu wa chama cha siasa akafanyia kazi kijijini kwao ni lazima awe eneo la kazi hivyo baada ya ukomo wa kazi wengi huamua kurudi makwao kuwa pamoja na jamii zao.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wanamudu vp mfumo mpya wa maisha ktk mazingira hayo mapya?
 
Kwa wale ambao kipindi chote wakiwa wanafanya kazi hawakuwahi kuwekeza huko kijijini, wala hawakua na utaratibu wa kwenda kusalimia na kukaa huko kipindi cha likizo, lazima watapata tabu sana wakistaafu. Ila kwa waliojipanga tangu mwanzo wakijua kabisa siku wakistaafu wataenda kuishi kijijini, naona hua wanaishi kawaida tuu. Wengine unakuta wameshajenga huko na wameweka vimiradi vya kuwa keep busy kwahiyo maisha yanakua sio mabaya.
 
Wengi inasemekana wanarudi kufia kwao , japo kiukweli wanajikuta wanafia Muhimbili ama nchi za watu .

Natoa wito kwao kwamba wasirudi tena mjini wakiondoka , maana walishindwa kuelewa tulipowaambia watengeneze sera za kuboresha hospitali za mikoa walitupuuza

True tena unakuta mtu anamiliki mahekalu,magari lkn ajawahi hata nunua pencil akawakumbuka watoto wa kijijini kwake.
 
Wengi inasemekana wanarudi kufia kwao , japo kiukweli wanajikuta wanafia Muhimbili ama nchi za watu .

Natoa wito kwao kwamba wasirudi tena mjini wakiondoka , maana walishindwa kuelewa tulipowaambia watengeneze sera za kuboresha hospitali za mikoa walitupuuza

Kwa sababu wewe hufahamu tu, wengi wanarudi kwa sababu baada ya kupata pension Maisha ni rahisi zaidi wakirudi Tanzania. Mfano nyumba UK 3brmd unalipa £2000 (London) kwa mwezi wakati nyumba kama hiyo Tanzania inaweza kuwa ya kwako hivyo hulipi chochote. Gharama ya maisha UK ukiwa na familia ndogo usafiri chakula nk kwa mwezi £1000. Hivyo basi wastani ni £3000 kwa mwezi, kwa mwaka £36,000 ukiondoa nyumba. Akiwa Tanzania hawezi kutumia zaidi ya £1000 kwa mwezi ukitilia maanani kwamba ana gari yake mwenyewe na ana pension isiyopungua £500,000.(half a million) Huo ni wastani kwa mtu anayelipa pension kwa miaka 20. Mshahara usiopungua £40,000 - £60,000 kwa mwezi yaani proffesional sio wafagia vyoo au wafanyakazi kwenye homes nk.
 
Wadau wa JF hongereni kwa sikukuu ya Christmas.

Mada hapo juu yajifafanua vizuri. Watu wengi ikiwa ni pamoja na watumishi, wanasiasa nk wakistaafu shughuli zao hurudi kwao. Huko warudipo walishaondoka siku nyingi sana na hurudi wakati wa likizo na dharura mbalimbali. Sasa cha kujiuliza mtu amejenga mahekalu maeneo mbalimbali lakini huyaacha na kurudi Nyumbani kwao kijijijini au mjini kisa huwa nini?

Wanamuduje mfumo mpya wa maisha na jamii mpya tofauti?
Siku hizi hakuna kitu kama hicho. Asilimia kubwa wanabaki mahali walipostaafia kazi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom