Kwanini watu wengi wa Kanda ya ziwa hasa Wakurya ni Wasabato?

Director D

Senior Member
Feb 24, 2016
192
229
Habari zenu wakuu,

Katika pitapita zangu za hapa na pale nimebahatika kutambua kitu ambacho nilkuwa sikijui nacho ni kuwa waumini wengi wa dhehebu la wasabato ni watu wa Kanda ya ziwa hasa wakurya mfano kwa hapa Dar maeneo ya Gongo la Mboto, Kitunda, Lugalo, Mabibo n.k ambako kunaaminika kuwa na idadi kubwa ya wakurya wengi wao husali sabato kwa kifupi hapa mjini ni vigumu kukuta kanisa la wasabato bila wakurya.

Naomba kujuzwa kuhusu jambo hili ni kwa nini wakurya wengi ni wasabato?
 
sasa unaweza kuja kuuliza ni kwa nini watu wa Pwani na Zanzibar ni waisilamu? kamahuwezi basi tumia mantiki hiyo hiyo kujua ni kwa nini hao uliowataja ni wa kundi hilo...
 
Wamissionary wakwanza wa Kisabato waliingia Tanzania tokea Kaskazini(hasa Upareni) baadaye wakaeneza ujumbe Ukanda huo Kaskazini Magharibi hadi kanda ya ziwa.
 
Hao
Habari zenu wakuu,

Katika pitapita zangu za hapa na pale nimebahatika kutambua kitu ambacho nilkuwa sikijui nacho ni kuwa waumini wengi wa dhehebu la wasabato ni watu wa Kanda ya ziwa hasa wakurya mfano kwa hapa Dar maeneo ya Gongo la Mboto, Kitunda, Lugalo, Mabibo n.k ambako kunaaminika kuwa na idadi kubwa ya wakurya wengi wao husali sabato kwa kifupi hapa mjini ni vigumu kukuta kanisa la wasabato bila wakurya.

Naomba kujuzwa kuhusu jambo hili ni kwa nini wakurya wengi ni wasabato?
Hao Wakurya wanajitambua ndio maana wanasali Sabato. Nijuavyo mimi kusali Sabato ni kutimiza amri ya nne ya Mungu kama ilivyotolewa kwenye Kutoka 20:8. Ikumbukwe pia kuwa Yesu alikuwa Msabato kasome Luka 4:16, Paulo na mitume wote walikuwa Wasabato kasome Matendo ya Mitume 17:2, tukienda Mbinguni kwa watakaoshinda dhambi za dunia hii watatunza Sabato kasome Isaya 66:23. Tuwapo hapa duniani wote tunatakiwa kutunza Sabato kasome Waebrania 4:9. Huo ndio ukweli wenyewe. Kama unabisha lete ushahidi wa maandiko kuhalalisha msimamo wako.
 
Kwanini MOSHI wengi ni Walutheri(KKKT) afu KAGERA ni RC?
Moshi RC ndio wengi sio KKKT!

KKKT ipo Machame na Marangu kidogo na Old Moshi.

Ukienda Kibosho hakuna kanisa la KKKT, Ukienda Rombo Hakuna kanisa la KKKT, Ukienda Uru robo ni KKKT, Marangu nusu nusu, Old Moshi KKKT WENGI NA MACHAME.

Inasadikiwa 64% ya wachaga ni ROMAN CATHOLIC
 
Usiseme wa kanda ya ziwa sema watu wa mkoa wa Mara. Huko usabato umetawala sana ila mikoa mingine hasa kagera ni wakatoliki na walutheran sanasana
 
Kwasabau ya wamissionari wa kisabato walianza kuingia mapema maeneo hayo
Kwanza walianzia upareni, usukumani hasa maeneo ya Bariadi , Mara musoma na walijenga mashule ya kimissionari huko kama vile Ikizu,Nyasincha na kadhalika kiujumla mkoa wa mara una wasobato wengi hasa Wajita,Wakurya , Waikizu,wazanaki na kadhalika, pia wamissionari wa kisabato waliendelea kueneza injili Kigoma- Kasulu-Heri Mission ,
Mbeya-Tukuyu na sehemu zote hizo walifungua mashule yao ya misheni
Kwa ufupi ndiyo hivyo
 
Kwa kifupi hii research haijakaa sawa, watu wanaoitwa wakurya wengi wanashindwa kuelewa ni watu wanaoishi maeneo gani huko kanda ya ziwa. Mimi ninavyojua wakurya huko kanda ya ziwa wanapatikana wilaya ya Tarime na SERENGETI, lakini pia wako kwa kiasi wilaya zingine huko. Sasa ukienda wilaya RORYA ukiacha shirati amabako kuna kanisa kubwa la menonite walio wengi ni RC. Si kwamba shirati menonite wako wengi ila ndiyo kuna kanisa kubwa la menonite rorya nzima. Ila dhehebu kubwa MARA AU HATA HUKO KWA WAKURYA NI RC, labda ndiyo sabato wanafuata halafu ROHO , na makanisa mengine madogo
 
Back
Top Bottom