Elections 2010 Kwanini watu wengi hawakujitokeza kupiga kura?

babayah67

JF-Expert Member
Mar 28, 2008
493
79
Sio siri uchaguzi mkuu wa wabunge na Rais wa mwaka huu 2010, umeacha maswali mengi na maeneo kadhaa ya Political analyst na Political Scientist kuyafanyia kazi. Moja ya eneo hilo ni IDADI NDOGO YA WAPIGA KURA ILIYOJITOKEZA.

Katika vituo karibu vyote vya Tanzania Bara, watu waliojitokeza ni chini ya asilimia 50. Ukiangalia watu waliokuwa wakihudhuria mikutano ya wagombea urais, na ukiangalia idadi ya watu waliokuja piga kura mtu unajiuliza kulikoni?

Hali hii inanifanya nikubaliane na hofu aliyokuwa nayo Prof Baregu juu ya uhakika wa hizo data za wapiga kura. Nafikiri kuna haja ya utafiti wa hali ya juu ufanyike ili kujua hasa nini kimefanyika kilichopelekea idadi ya watu waliojitokeza kuwa ndogo kiasi hiki.
 
Kuna nadharia nyingi zinazoweza kutumika katika kuelezea dhana hiyo:

Mmoja ni kwamba watu wengi walijiandikisha ili kupata kitambulisho ambacho kinatumika katika mambo mengi kama kufungulia a/c nk

Pili majina ya watu wengi hayakuonekana katika vituo vya kupigia kura na mengina yalikuwa misplacec

Tatu hofu ya wizi wa kura katika utafiti wangu wa haha na pale watu wengi wamekuwa wakisema hawapigi kura kwa sababu wanajua zitaibiwa tu of which is narrow view and ignorance (to some extent ina ukweli ndani yake)

Nne watu wengi kuhama makazi hivyo kuwa mbali na maeneo yao waliyojiandikishia kupiga kura
nawakilisha wakuu.
 
Nafikiri ishu ya watu kuhama na kutokuwa na ktk vituo vyao siku ya kura imechangia sana. Nafikiri tunatakiwa kufanya kitu kwa chaguzi za mbele
 
Baadhi ya vyama viliridhika na umati kwenye mikutano wasijue kuwa walikuwa ni mashabiki tu waliokuwa wakifuata mkumbo.
CCM walijua wapiga kura wao waliko na kuwafuata huko huko - ndo maana tulikuwa tunasikia suala la mikutano ya ndani na kampeni za nyumba kwa nyumba na kitanda kwa kitanda.
Aidha jumuia mbali mbali za chama tawala kama vijana, wanawake, wazee nk zilitumiwa kikamilifu.
Pengine hili ni somo kwa vyama vinavyochipukia kama Chadema.
 
Elimu ya uraia inahitajika iwe endelevu, wengi walijiandikisha ili wapate vitambulisho vya kusajili simu!
huwezi kuamini nilimkuta jamaa mmoja anakunywa pombe tarehe 31/10/2010 saa 9 bado hajapiga kura na wala hakumbuki!:doh:
 
Sio siri uchaguzi mkuu wa wabunge na Rais wa mwaka huu 2010, umeacha maswali mengi na maeneo kadhaa ya Political analyst na Political Scientist kuyafanyia kazi. Moja ya eneo hilo ni IDADI NDOGO YA WAPIGA KURA ILIYOJITOKEZA. Katika vituo karibu vyote vya Tanzania Bara, watu waliojitokeza ni chini ya asilimia 50. Ukiangalia watu waliokuwa wakihudhuria mikutano ya wagombea urais, na ukiangalia idadi ya watu waliokuja piga kura mtu unajiuliza kulikoni??? Hali hii inanifanya nikubaliane na hofu aliyokuwa nayo Prof Baregu juu ya uhakika wa hizo data za wapiga kura. Nafikiri kuna haja ya utafiti wa hali ya juu ufanyike ili kujua hasa nini kimefanyika kilichopelekea idadi ya watu waliojitokeza kuwa ndogo kiasi hiki.

Very simple, waliaminishwa kuwa hata wakienda kupiga kura hawataweza kuleta mabadiliko kwani eti CCM wataiba kura......
 
kuna nadharia nyingi zinazoweza kutumika katika kuelezea dhana hiyo:
Moja ni kwamba watu wengi walijiandikisha ili kupata kitambulisho ambacho kinatumika katika mambo mengi kama kufungulia a/c nk
pili majina ya watu wengi hayakuonekana katika vituo vya kupigia kura na mengina yalikuwa misplacec
tatu hofu ya wizi wa kura katika utafiti wangu wa haha na pale watu wengi wamekuwa wakisema hawapigi kura kwa sababu wanajua zitaibiwa tu of which is narrow view and ignorance (to some extent ina ukweli ndani yake)
nne watu wengi kuhama makazi hivyo kuwa mbali na maeneo yao waliyojiandikishia kupiga kura
nawakilisha wakuu.

it does make sense
 
Elimu ya uraia inahitajika iwe endelevu, wengi walijiandikisha ili wapate vitambulisho vya kusajili simu!
huwezi kuamini nilimkuta jamaa mmoja anakunywa pombe tarehe 31/10/2010 saa 9 bado hajapiga kura na wala hakumbuki!:doh:

Watu watapewa elimu ya uraia hadi lini kama mtu unakunywa pombe hadi saa tisa usiku kesho yake unashindwa hata kuamka kwenda kupiga kura unataka elimu ipi ya uraia hapo
 
Tunaweza kuhusisha hii na mahesabu yaliyotiliwa shaka ya NEC kuwa jumla ya wapiga kura ni milioni 19? Manake tofauti ni kubwa mno mpaka inatia shaka...Inawezekana pia daftari halikuwa updated ipasavyo likawa na majina mengine ya waliofariki etc...
 
STrategy ya UWT ni kuwatch yale maeneo korofi kama dar,mbeya, mwanza, musoma arusha moshi bukoba etc kununua vitambulisha 20,000 na 15000 then wanawarudishia after uchaguzi

Hii nimeiona pale mwenge kwa waendesha bajaji walikuwa wananunuliwa kwa 20,000 per ID
 
idadi ya wapiga kura haikuwa ya kweli Ilipikwa ili kusaidia uchakachuaji kwenda mbele Nyambala alishasema hapa ila bahati mbaya hatukumuelewa. Soma:Takwimu hii ni sahihi? - Idadi ya wapiga kura TZ

Huo ulikuwa ni uzshi kwani tangia miaka mitatu iliyopita vyama vyote vilikuwa vinakubaliana kuwa 2010 kutakuwa na wapiga kura wengine wapya wapatao Milioni 5 ambayo ndiyo idadi iliyongezeka. Lakini pia kwa mujibu wa ripoti ya STATE OF WORLD POPULATION 2010 ya United Nations iliyozinduliwa tarehe 22 October 2010, Tanzania inakadiriwa kuwa na watu Milioni 45 hivi sasa......
 
Baadhi ya vyama viliridhika na umati kwenye mikutano wasijue kuwa walikuwa ni mashabiki tu waliokuwa wakifuata mkumbo.
CCM walijua wapiga kura wao waliko na kuwafuata huko huko - ndo maana tulikuwa tunasikia suala la mikutano ya ndani na kampeni za nyumba kwa nyumba na kitanda kwa kitanda.
Aidha jumuia mbali mbali za chama tawala kama vijana, wanawake, wazee nk zilitumiwa kikamilifu.
Pengine hili ni somo kwa vyama vinavyochipukia kama Chadema.

Mbona Batilda kashindwa wakati alipiga kampeni za kitanda kwa kitanda; guest kwa guest?
 
kuna nadharia nyingi zinazoweza kutumika katika kuelezea dhana hiyo:
moja ni kwamba watu wengi walijiandikisha ili kupata kitambulisho ambacho kinatumika katika mambo mengi kama kufungulia a/c nk
pili majina ya watu wengi hayakuonekana katika vituo vya kupigia kura na mengina yalikuwa misplacec
tatu hofu ya wizi wa kura katika utafiti wangu wa haha na pale watu wengi wamekuwa wakisema hawapigi kura kwa sababu wanajua zitaibiwa tu of which is narrow view and ignorance (to some extent ina ukweli ndani yake)
nne watu wengi kuhama makazi hivyo kuwa mbali na maeneo yao waliyojiandikishia kupiga kura
nawakilisha wakuu.

Nakubaliana na hoja za Mishemishe. Hiyo inaakisi ukweli kuwa bado elimu ya uraia inahitajika sana, si vijijini tu bali hadi mjini. Lakini takwimu zikoje roughly?
 
Nakubaliana na hoja za Mishemishe. Hiyo inaakisi ukweli kuwa bado elimu ya uraia inahitajika sana, si vijijini tu bali hadi mjini. Lakini takwimu zikoje roughly?

Jamani elimu ya uraia imefanyika vya kutosha na msitegemee kuwa itafika wakati eti watu wote watakuwa na mtazamo wa aina moja katika suala hili. Kuna tatizo kubwa la imani ya wananchi kwa kila kitu kinachohusiana na siasa. Hili ni tatizo kubwa ambalo kwa Tanzania linaendana sambamba na hali ya ktokuaminiana kati ya mtu na mtu kama ambavyo ripoti zinavyoonyesha kuwa kati ya watu 8 ni mmoja tu mwenye kumuamini mwenzake.

Lakini pia wanasiasa wanaotokana na mfumo kandamizi uliogubikwa na ubinafsi na ufisadi wana sehemu kubwa ya kujenga hali hii ya wananchi kutokuamini kila kitu kinachohusiana na siasa...

Kwa hili pia uvivu wa wananchi katika kufuatilia mambo hata kwa wale wanaojiona ni wasomi nalo ni tatizo linalopelekea hii hali ya kutokuwa na imani na masuala ya kisiasa...

Na pia hizi siasa za naming and shaming zilizoibuka miaka ya karibuni kwa upande mmoja zinawapandisha watu hasira dhidi ya watawala wao lakini kwa upande mwengine zinawafanya wengi wadi-test everything to do with politics....

Vilevile zile propaganda kuwa ni lazima CCM wataiba ushindi wa wapinzani nazo zimewafanya watu wengi haswa vijana kutokuona umuhimu wa kuhangaika kupiga kura

Yote haya kwa pamoja yamepelekea watu kutokuona umuhimu wa kupiga kura
 
Sio siri uchaguzi mkuu wa wabunge na Rais wa mwaka huu 2010, umeacha maswali mengi na maeneo kadhaa ya Political analyst na Political Scientist kuyafanyia kazi. Moja ya eneo hilo ni IDADI NDOGO YA WAPIGA KURA ILIYOJITOKEZA. Katika vituo karibu vyote vya Tanzania Bara, watu waliojitokeza ni chini ya asilimia 50. Ukiangalia watu waliokuwa wakihudhuria mikutano ya wagombea urais, na ukiangalia idadi ya watu waliokuja piga kura mtu unajiuliza kulikoni??? Hali hii inanifanya nikubaliane na hofu aliyokuwa nayo Prof Baregu juu ya uhakika wa hizo data za wapiga kura. Nafikiri kuna haja ya utafiti wa hali ya juu ufanyike ili kujua hasa nini kimefanyika kilichopelekea idadi ya watu waliojitokeza kuwa ndogo kiasi hiki.

ndugu babayah67, kwanza nakshukuru kwa thread hii. mimi nilipost thread kama hii yenye kichwa tofauti "Redet na Synovet wafanye utafiti katika eneo hili". Nilieleza masikitiko yangu ambapo katika kata niliyokuwepo yanjimbo la kinondoni waliopiga kura walikuwa kama 32%! Nikasema hata kama kuna sababu nyingi vipi, hiyo inatisha!. Mbaya zaidi tatizo hili ni kubwa zaidi Bara (Tanganyika) zanzibar wao ni nafuu. Je katika hali kama hii, tutaweza kuiamini tume ya Uchaguzi?

Nadhani mbali na makampuni hayo, hata wale wanaotafuta PhD wanaweza kuangaliua sehemu hii. Itaweza kutusaidia kupata ufumbuzi wa tatizo hili. La sivyo tutaendelea kuwa na matatizo makubwa kuliko ilivyo sasa.
 
kwaheshima na taadhima naomba watanzania wenzangu mnisaidie mawazo yenu katika uhalisia wa jambo hilo...
 
kwaheshima na taadhima naomba watanzania wenzangu mnisaidie mawazo yenu katika uhalisia wa jambo hilo...

Haiingii akilini, wananchi wengi sana safari hii walipiga kura, hizo takwimu zinazoonyesha wananchi hawakupiga kura zimechakachuliwa......pia kumbuka kabla ya hapo CCM walinunua shahada nyingi sana katika kila kona ya JMT ili kudhoofisha vyama vya upinzani.

Na kubwa zaidi ni uchakachuaji wa matokeo na lile daftari la wapiga kura ili kuonyesha kwamba watu waliojitokeza kupiga kura ni wachache wakati hali halisi vituoni ni kuwa watu wengi sana walienda kupiga kura.

Tusubiri, tutasikia madudu mengi yaliyofanyika wakati wa uchaguzi...
 
Back
Top Bottom