Kwanini watu wengi hasa wanawake hawapendi majina ya kibantu? Ubaya wake uko wapi?

Mshinga

JF-Expert Member
Feb 5, 2013
3,532
1,124
NIKIWA NIMETULIA LEO TAREHE 02/01/2014 wazo la matumizi ya majina linanijia wakati nafikiria niweke topiki ipi ya kwanza ndani ya mwaka huu.
ni mada nyingi zinakuja kichwani lakini nimeona ni muhimu leo tujadili matumizi ya majina kwa namna tofauti tofauti.

IMANI JUU YA MAJINA YA WATU
1.kuna majina yanahusishwa na upole
2.kuna majina yanahusishwa na uzuri
3.kuna majina yanahusishwa na ukarimu
4.kuna majina yanahusishwa ufalme/utawala
5.kuna majina yanahusishwa na umalaya
6.kuna majina yanahusishwa na ukatiri
7.kuna majina yanahusishwa na uchoyo nk nk


UKWELI NI KWAMBA MAJINA PIA YANA MAANA ZAKE
1.kuna majina yanamaana ya upendo
2.kuna majina yana maana ya uzuri
3.kuna majina yana maana ya upole
4.kuna majina yana maana ya unyenyekevu
5.kuna majina yana maana ya vitu mbalimbali kama wanyama,miti,miamba nk


UKWELI MWINGINE.
kila kabila lina majina yenye maana mbalimbali karibu kila kundi.


CHA KUSHANGAZA.
watu wengi hawapendi kutumia majina ya kibantu hata kama yana maana nzuri kuliko yale ya watu weupe wanayotumia.
na ni-ukweli usiopingika kuwa wanawake ndio wanaongoza kuchukia majina ya kibantu na huwa hawapendi kuyasema hadharani majina hayo na kuna wakati mwingine wanayakana ama kukataa kuwa wao hawana majina ya kienyeji pamoja na ukweli kwamba majina wanayo na walipewa toka utotoni.
KWA SAMPULI YA HARAKAHARAKA hata hapa MMU ugonjwa huu upo kwa kiasi kikubwa na ninaomba nitumie MMU kama sampuli ya harakaharaka kwa ninachokisema.


binafsi natumia jina la kibantu na ninalipenda,wengine humu ni kama Mwallu,manka nk hawa ni wachache naowajua hapa wanatumia majina ya kibantu katika lugha za kibantu,hata signature nyingi humu hazitumii lugha zetu hata ile ya taifa,tatizo ni nini?



mfano.
ningependa kuweka majina machache ya kisukuma na maana zake tuone kama yana ubaya wowote kiasi cha wasichana na hata wanaume kuyakataa ama kukataa kuyatumia,tena wakiyaona ni majina ya kishamba


1.Kwangu(limetokana na neno kwangulija)-maana yake ni mtoto wa mwisho
2.Njile(neno njile lina maana ya kwenda,jina hili hupewa msichana kama ikitokea watoto wote wanaozaliwa wanakufa bila kukua,na hivyo wakizaa tena,wazazi wakuwa wanajua na huyu atakufa na hivyo wanampa jina hili)-maana ni msichana aliyetegemewa hatakua bali atakufa kama ilivyo kwa watangulizi wake.
3.Geni(limetokana na neno bhugheni)-huyu alizaliwa wakati wazazi wake walienda ugenini
4.Nyanzala(limetokana na neno nzala-njaa)-huyu alizaliwa wakati wa njaa
5.Kashinje-huyu alizaliwa akiwa ametanguliza miguu badala ya kichwa.
6.mshinga-ni staili ya dansi kama zilivyo chalanga,ama ile ya diamondi na nyingine nyingi,ni staili katika ngoma za kisukuma.
7.Nsabi(limetokna na neno nsabhi-tajiri)-lina maana ya tajiri
8.Mwigulu(imetokana na neno ng'wigulhu)-lina maana ya mbingu
9.Kamwa(limetokana na neno kang'wa-limetokana na mnyama SUNGURA)-msichana mwenye akili/SUNGURA
10.Nungu(limetokana na na neno nhunghu likimaanisha chungu cha kupikia)-lina maana ya chungu


mfano wa majina ya weupe.
1.Doricus
2.Irene-amani
3.Elizabeth-Kiapo cha Mungu
4.Tabitha-gazelle-swara.
5.Chelsea-chungu(port)
KWA NINI WATU WENGI HAWAYAPENDI MAJINA YA KIBANTU? MFANO MTU AKIITWA TABITHA(swara) atapenda kuliko akiitwa KAN'GWA(sungura) ama MTU ANAONA BORA NA FAHARI KUTUMIA JINA CHELSEA(chungu-port) kuliko kutumia Nungu(chungu-port)
 
Jibu rahisi, jepesi na la kivivu ni kwamba hayana mvuto kulingana na yanavyotamkwa...
 
jina langu la asili lina maana ya honey! asali- japo ni la kiume!

iam so sweet indeed! na hilo ndilo lililoko kwenye vyeti kuanzia chekechea mpaka cheti cha masters..!

proud to be born a kurya!!!
 
Mada nzuri ila usivyojiamini ukaona useme hasa wanawake!!!! aaarghhh! As if wanaume wote wanatumia majina ya asili.
Wewe kama wazazi wako walikupa la kibantu safi ila sisi wengine tumejikuta tumeshabatizwa haya ya wenzetu na hayo ya asili unayoyataka wewe hatuna!
 
Sasa je,yeye anataka aanze kutuletea majina ya kina "mashaka",Zimbwenyi nan anayataka hayo karne hii

Watu wamechoka majina kama Shida, Tabu, Sikujua nk..Siku hizi unapita town unasikia mdada anaitwa JLO.....
 
Jibu rahisi, jepesi na la kivivu ni kwamba hayana mvuto kulingana na yanavyotamkwa...
mvuto upi wakati majina mengi yasiyo ya kibantu hatuwezi kuyatamka hata inavyotakiwa,sasa mvuto gani kama hata kuyatamka ni shida?tunachokitamka ni tofauti na inavyotakiwa,mfano jina la MADIBA linakosaje mvuto?jina la OBAMA linakosaje mvuto?jina la NYERERE linakosaje mvuto?jina la MANKA linakosaje mvuto katika matamshi?hatuwezi kuleta hoja nyepesi kama ulivyoziita kama sababu,wengi wameathirika kwenye ubongo na kutojithamini na kujiamini.
kila jina linaweza kuwa na mvuto DUNIANI KOTE kulingana na MTU ANAVYOFANIKIWA AMA KUFANYA MAAJABU,mjina kama MADIBA-MANDELA,NYERERE,NKURUMAH,OBAMA,SAMOLA NK yana mvuto zaidi kwa sababu wenye majina wamefanya makubwa,hata wazungu leo wapo wanaotumia majina kama ya obama,mandela nk lakini wao wanafanya hivyo kwa sababu maalumu hasa upekee wa wenye hayo majina lakini si utumwa wa kutojiamini na kujithamini
 
jina langu la asili lina maana ya honey! asali- japo ni la kiume!

iam so sweet indeed! na hilo ndilo lililoko kwenye vyeti kuanzia chekechea mpaka cheti cha masters..!

proud to be born a kurya!!!

Nataka nikuonje aisee
 
Mvuto...... Au utumwa? Tanzania kuna makabila 120. Majina yapo mazuri na mvuto upo.

Naam ni utumwa pia...binafsi mimi watu8 natumia majina ya asili tena ya Kibantu...

Moja ya sifa kubwa za ukoloni walikuwa na sera moja wanaiita "assimilation policy", ilikuwa na nguvu sana katika makoloni ya Kifaransa, hawa jamaa walikuwa wanahakikisha wanaambukiza tamaduni zao zote kwa mataifa waliyotawala.

Kwa hiyo hata hili la majina linaangukia hapo, mathalani Kambarage pamoja na kuwa mstari wa mbele kwenye kumng'oa mkoloni hapa Tanzania (Tanganyika) lakini hakuacha kulitumia jinale la Julius alilopewa na Mzee Bulito.
 
Back
Top Bottom