ERoni
JF-Expert Member
- Jan 9, 2013
- 43,635
- 90,026
Sisi waafrika hasa watanzania tunapenda sana kuiga vitu vya wazungu hata kama hatujui maana yake nini. Na kwa bahati mbaya sana tunaiga na kupitiliza kuliko hata hao tunaocopy kutoka kwao. Mimi sidhani kwamba ukoloni peke yake ndio ulioleta hii kasumba ya kupenda majina ya kizungu hata kama hatujui maan ya hayo majina bali pia kutothmini ila nadesturi zetu na kufagilia za nje. Si tk majina tu bali karibia kila kitu tunashobokea hata uchafu unaofanywa na wazungu. Hatjiamini na asili yetu na bahati mbaya sana hata serkali zetu hazikutilia mkazo kwenye suala la majina ya saili ndiyo maana tumefika hapa tulipo leo!
Kama kweli ni ukoloni ndio uliotufanya tuache majina yetu ya asili mbon nch kama za bara a asia kama CHINA, JAPANI, NCHI ZOTE ZA KIARABU watu wake wamedunmisha majina ya asili pamoja kwamba nao walitawaliwa na wakoloni? Hata baadhi ya nchi a Africa kama vile Africa ya Kusini na nchi za Afrika magharibi kam GHANA,NIGERIA na nchi nyingine za ukanda huo kwa kiasi ulani wanatumia majina yao ya asili? Hata nchi jirani kama Kenya na Uganda wanatuimia majina yao ya asili kwaasilimia kubwa ukilinganisha na Tanzania. Hivyo tatizo letu waafrika ni ulimbukeni wa kuiga na kuthamini vitu vya kizungu kiliko asili yetu tena tunaurahia kweli kweli!
Umefanya uchunguzi kujua waAfrika magharibi hawatumii majina ya kizungu?
Hakuna nchi wanayopenda kutumia majina ya kimagharibi kama waGhana, kuna kabila moja wanaitwa 'Chwi', majina ya walio wengi ni ya kizungu/kimagharibi...hata Liberia wanatumia sana haya majina...
Africa kwa ujumla tumetawaliwa karibu kila kitu....