Ablessed
JF-Expert Member
- Mar 19, 2013
- 4,616
- 3,499
lkn sio la kilugha.........Happy New Year
Mie langu la kiswahili kabisaaa..
lkn sio la kilugha.........Happy New Year
Mie langu la kiswahili kabisaaa..
ni kweli,japo kwa mchanganuo wangu wanawake wamezidi
je wewe unayachukulije majina ya kibantu ?unaweza kumpa mtoto wako?
NIKIWA NIMETULIA LEO TAREHE 02/01/2014 wazo la matumizi ya majina linanijia wakati nafikiria niweke topiki ipi ya kwanza ndani ya mwaka huu.
ni mada nyingi zinakuja kichwani lakini nimeona ni muhimu leo tujadili matumizi ya majina kwa namna tofauti tofauti.
IMANI JUU YA MAJINA YA WATU
1.kuna majina yanahusishwa na upole
2.kuna majina yanahusishwa na uzuri
3.kuna majina yanahusishwa na ukarimu
4.kuna majina yanahusishwa ufalme/utawala
5.kuna majina yanahusishwa na umalaya
6.kuna majina yanahusishwa na ukatiri
7.kuna majina yanahusishwa na uchoyo nk nk
UKWELI NI KWAMBA MAJINA PIA YANA MAANA ZAKE
1.kuna majina yanamaana ya upendo
2.kuna majina yana maana ya uzuri
3.kuna majina yana maana ya upole
4.kuna majina yana maana ya unyenyekevu
5.kuna majina yana maana ya vitu mbalimbali kama wanyama,miti,miamba nk
UKWELI MWINGINE.
kila kabila lina majina yenye maana mbalimbali karibu kila kundi.
CHA KUSHANGAZA.
watu wengi hawapendi kutumia majina ya kibantu hata kama yana maana nzuri kuliko yale ya watu weupe wanayotumia.
na ni-ukweli usiopingika kuwa wanawake ndio wanaongoza kuchukia majina ya kibantu na huwa hawapendi kuyasema hadharani majina hayo na kuna wakati mwingine wanayakana ama kukataa kuwa wao hawana majina ya kienyeji pamoja na ukweli kwamba majina wanayo na walipewa toka utotoni.
KWA SAMPULI YA HARAKAHARAKA hata hapa MMU ugonjwa huu upo kwa kiasi kikubwa na ninaomba nitumie MMU kama sampuli ya harakaharaka kwa ninachokisema.
binafsi natumia jina la kibantu na ninalipenda,wengine humu ni kama Mwallu,manka nk hawa ni wachache naowajua hapa wanatumia majina ya kibantu katika lugha za kibantu,hata signature nyingi humu hazitumii lugha zetu hata ile ya taifa,tatizo ni nini?
mfano.
ningependa kuweka majina machache ya kisukuma na maana zake tuone kama yana ubaya wowote kiasi cha wasichana na hata wanaume kuyakataa ama kukataa kuyatumia,tena wakiyaona ni majina ya kishamba
1.Kwangu(limetokana na neno kwangulija)-maana yake ni mtoto wa mwisho
2.Njile(neno njile lina maana ya kwenda,jina hili hupewa msichana kama ikitokea watoto wote wanaozaliwa wanakufa bila kukua,na hivyo wakizaa tena,wazazi wakuwa wanajua na huyu atakufa na hivyo wanampa jina hili)-maana ni msichana aliyetegemewa hatakua bali atakufa kama ilivyo kwa watangulizi wake.
3.Geni(limetokana na neno bhugheni)-huyu alizaliwa wakati wazazi wake walienda ugenini
4.Nyanzala(limetokana na neno nzala-njaa)-huyu alizaliwa wakati wa njaa
5.Kashinje-huyu alizaliwa akiwa ametanguliza miguu badala ya kichwa.
6.mshinga-ni staili ya dansi kama zilivyo chalanga,ama ile ya diamondi na nyingine nyingi,ni staili katika ngoma za kisukuma.
7.Nsabi(limetokna na neno nsabhi-tajiri)-lina maana ya tajiri
8.Mwigulu(imetokana na neno ng'wigulhu)-lina maana ya mbingu
9.Kamwa(limetokana na neno kang'wa-limetokana na mnyama SUNGURA)-msichana mwenye akili/SUNGURA
10.Nungu(limetokana na na neno nhunghu likimaanisha chungu cha kupikia)-lina maana ya chungu
mfano wa majina ya weupe.
1.Doricus
2.Irene-amani
3.Elizabeth-Kiapo cha Mungu
4.Tabitha-gazelle-swara.
5.Chelsea-chungu(port)
KWA NINI WATU WENGI HAWAYAPENDI MAJINA YA KIBANTU? MFANO MTU AKIITWA TABITHA(swara) atapenda kuliko akiitwa KAN'GWA(sungura) ama MTU ANAONA BORA NA FAHARI KUTUMIA JINA CHELSEA(chungu-port) kuliko kutumia Nungu(chungu-port)
Hahaaaaaa..... Onisecha ng'wanike!
jina langu hilihili hapa kwenye id. na nimeeleza maana ya mshinga hapo kwenye madakwanza mbona hujatuambia la kwako? Pili mbona shule ulikuwa unatumia beatus dominic na dada yako mkampa mary? Mbona yule mtoto wako umemwita carlos?
Kumbe eeh,ngoja nianze kukuandama nikufaidi
jina langu la asili lina maana ya honey! asali- japo ni la kiume!
iam so sweet indeed! na hilo ndilo lililoko kwenye vyeti kuanzia chekechea mpaka cheti cha masters..!
proud to be born a kurya!!!
Dah! Hatariiii! Kwa lugha yetu asali tunaita ' UCHI' hahaha! Happy new year UCHI
karibu!!
ila sidhani kama tutamechi vipimo!
mi navaa 55!
Tutamechi hata kwa lazima,lol
wewe binafisi unayachukuliaje majina ya kibantu?unaweza kumwita mwanao kwa jina la kibantu?
okey mkuu subir ntabadilishamsaada huanzia nyumbani!
Wewe hata usingetumia kiluga, ungejiita 'mlima' ingekua poa sana!
nilianza na neno mlima nikaambiwa kuna user anatumia ilo neno...nikatafufuta neno mlima kwa lugha yangu ya mama ikawa haina neno mbadala,,,nkaona haina kelele wacha niende kwenye lungha za kigeni.......msaada huanzia nyumbani!
Wewe hata usingetumia kiluga, ungejiita 'mlima' ingekua poa sana!