Kwanini watu wanawachukia sana wanasiasa vijana wa CCM?

mdukuzi

JF-Expert Member
Jan 4, 2014
16,038
35,911
Sina haja ya kuwataja majina, ila wanasiasa vijana ndani ya CCM wanachukiwa na watu kulinganisha na wenzao ndani ya UKAWA and vice versa, wazee ndani ya UKAWA hawapati heshima kama ya wazee wa CCM.

Kijana ndani ya CCM akijitahidi kuonyesha uwezo wake ataambiwa mnafiki, anajipendekeza, anatumia umaarufu wa baba yake n.k.

Hii ni hatari kwa mustakabali wa CCM huko mbeleni.
 
Hebu niambie mbunge yeyote kijana toka CCM anayetetea wananchi badala ya chama, wewe mwenyewe ni shahidi wabunge wengi toka CCM hawatetei wananchi zaidi ya kujipendekeza ili wakumbukwe kwenye nafasi
 
Hebu niambie mbunge yeyote kijana toka CCM anayetetea wananchi badala ya chama, wewe mwenyewe ni shahidi wabunge wengi toka CCM hawatetei wananchi zaidi ya kujipendekeza ili wakumbukwe kwenye nafasi

Na huu ndio ukweli wenyewe!
 
lete uthibitisho
 
Na ccm imetambua kuwa vijana wao wanajipendekeza na hawawezi tetea maslahi ya Taifa ndio maana imekinya chama taasisi ya familia zao, akifa baba/mama nafasi anapewa mtoto.
 
Wanalilia vyeo, kuna mmoja aliwatukana sana chadema, kweli bwana kalambishwa unaibu Wazir wa njuruku 😀😁😱
 
Sina haja ya kuwataja majina, ila wanasiasa vijana ndani ya CCM wanachukiwa na watu kulinganisha na wenzao ndani ya UKAWA and vice versa, wazee ndani ya UKAWA hawapati heshima kama ya wazee wa CCM.

Kijana ndani ya CCM akijitahidi kuonyesha uwezo wake ataambiwa mnafiki, anajipendekeza, anatumia umaarufu wa baba yake n.k.

Hii ni hatari kwa mustakabali wa CCM huko mbeleni.

Wewe ungependa yupi, kati ya yule anayefanya siasa za tumbo au yule anayefanya siasa kwa ajili ya umma??

Hao wazee achana nao, wanasumbuliwa na limbwata la maji ya bendera za TANU na ASP!
 
swali,kwa nini hawatetei wananchi?
Mnahangaika sana. Mwigulu Nchemba ni kijana na kama kuna watu wanamchukia basi ni wale Mafisadi. Nape Moses Nnauye ni kijana ambaye amesimamia mapambano dhidi ya ufisadi wakati wa uteuzi wa wagombea na amefanikiwa. Paul Makonda alijitokeza na kusema waziwazi kuwa Lowasa ni fisadi. Baada ya hapo mawakala wa mafisadi walimchukia sana
 
Hebu niambie mbunge yeyote kijana toka CCM anayetetea wananchi badala ya chama, wewe mwenyewe ni shahidi wabunge wengi toka CCM hawatetei wananchi zaidi ya kujipendekeza ili wakumbukwe kwenye nafasi
Nakubaliana na wewe ndugu!
 
Msukumo mkubwa walionao vijana kuingia kwenye uongozi kiuhalisia hautokani na utashi wao, Mtazamo wa vijana wengi baada ya kumaliza elimu yao ni ajira. Kwa bahati mbaya ajira imekuwa ni changamoto kubwa duniani na haipatikani kirahisi.
Kutokana na hali hiyo vijana wengi wanaoingia CCM ni wachumia tumbo, na wengi wanachukiwa kutokana na tabia yao ya kujipendekeza kwa viongozi na kuwa loyal kwao kuliko maslahi ya umma. Na kutokana na mfumo wa utawala wa nchi hii ulivyo viongozi huwateua vijana hawa kushika nyadhifa mbambali kwa upendeleo na si kwa sifa stahiki ili walinde maslahi yao. Mifano tunayo Nape, Makonda, January na wengineo. Mfano wa karibuni kabisa ni Naibu Spika wa Bunge Dr Tulia Mwansasu, angalia alivyobebwabebwa hadi anaipata nafasi hiyo. Na hii ni kwa sababu aliwafurahisha watawala kuhakikisha kesi ya Ukawa kuzuia watu wasisimame umbali wa mita mia mbili toka kituoni baada ya kupiga kura aliifanikisha na CCM wakatumia mwanya huo kuiba kura walivyotaka. Kimsingi wengi wao wanakuwa ni mamluki wa kuimba nyimbo za kuwasifia waliowafikisha hapo na CCM hata katika mambo yasiyo na msingi.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom