Kwanini watu wanapotea na kutekwa na Jeshi la Polisi lipo kimya?

Chakaza

JF-Expert Member
Mar 10, 2007
40,319
72,743
Kuna matukio ya kupotea watu wenye itikadi ya aina fulani na iko wazi kabisa kuwa majibu ya vyombo vinavyohusika na usalama wetu vinatoa majibu mepesi sana.

Kuna nini? Wanachukuliwa na nani na wako wapi? Kwanini wapoteaji ni wale kwenye kuwasema watu wa aina fulani tuu? Yuko wapi Saanane? Leo tena siku ya tatu Roma polisi wanasema hajulikani kapelekwa wapi lakini simu iko hewani.

Tumbane Mwigulu aseme anachojua maana toka tukio la bastola kwa Nape inaonyesha usalama wa maisha ya Watanzania umehama kutoka wizara yake uko chini ya kikundi ambacho hana uwezo/mamlaka wa kukigusa.
 
Ukitaka kuwa polisi sifa ya kwanza inabidi uwe mwana ccm pure.
sasa hapo unafikri polisi atamsaidia nini mtu wa upinzani?

Kuna jamaa mmoja amewahi kuniambia ukitaka kupata kazi ya polisi kiurahisi.
kipindi cha kampeni kuwa karibu sana na ccm.
 
Nikikumbuka ile kesi ya mwigu.. kumsingizia Mnyika nakosa imani kabisa na huyu mtu,sijui haogopi Mungu maana duniani tunapita na madhambi hubatilizwa vizazi hata vizazi...mnaenda kanisani na misikitini ili muonekane wema machoni mwa watu? mnamsahau Muumba wenu!?kutenda mema si kwaajili yako tuu Bali vizazi vyako pia!! Utatesa wanao na wajukuu kwa maovu unayohisi unafanya sirini,kwake Mungu hakuna siri. Awake liar leaders
 
Kuna matukio ya kupotea watu wenye itikadi ya aina Fulani, na iko wazi kabisa kuwa majibu ya vyombo vinavyohusika na usalama wetu vinatoa majibu mepesi sana. Kuna nini? Wanachukuliwa na nani na wako wapi? Kwa nini wapoteaji ni wale kwenye kuwasema watu wa aina Fulani tuu?
Yuko wapi Saanane? Leo tena siku ya tatu Roma polisi wanasema hajulikani kapelekwa wmaisha ya Watanzania umehama kutoka wizara yake uko chini ya kikundi ambacho hana uwezo/mamlaka wa kukigusa.
Mkuu chakaza haya yote yana mwisho na yataisha kwa anguko kubwa sana kila mtanzania anaona na anajua kile kinachoendelea tukatae tukubali hawa CCM wanaelekea kibla kipnd kijacho
 
Tatizo kubwa hua ni mfumo wa uongozi wa kutojali sheria, lakini pia uoga wa watanzania ndio umetufikisha hapo.
Kwa nchi zenye kufuata katiba na sheria upuuzi kama huu hauvumiliki.
Kama polisi hawafuatilii pangeundwa chombo huru kwa ajili ya kufuatia matukio kama hayo.
Kamati za ulinzi za wilaya husika zinafanya kazi gani kama wananchi wake hawana usalama?
Leo linaonekana kama ni jambo dogo sababu tu linatokea zaidi kwa watu wenye mrengo fulani,je siku ikitokea hivyo kwa upande wa pili watakaa kimya?
 
Tatizo la police wenyew wanatumwa tu kama pakanight akili hamna hata kuhoji kuwa kqfanya nn na akamatwe kwa kosa lipi yenyew ni mbio tu
.
.
.
Kyenekyaka nkighanile une
 
Mkuu polisi kwa sasa wanafanya kazi kwa maelekezo ya watu wawili. Wanasahau wanatufundisha kupambana nao wanapokuja kututeka.
 
Mkuu polisi kwa sasa wanafanya kazi kwa maelekezo ya watu wawili. Wanasahau wanatufundisha kupambana nao wanapokuja kututeka.
Ndio wasiwasi wangu kuwa watu waanza kujilinda pale wanapoona wanakamatwa kwani hawana hakika kama wanapokamatwa wanapelekwa kwenye vyombo salama au wanapotezwa.
Ndio mwanzo wa mapambano na umwagaji damu, kwani nani atakubali anapojua kuwa hapa naenda kupotezwa?
 
Mke Wa Roma mpaka sasa Kaishafika kituo cha polisi na kuchukua RB. Polisi wanadai hawajapata taarifa yoyote juu ya kukamatwa kwa Roma na Jeshi la Polisi. Polisi wanadai watalishughurikia swala la kupotea kwa Roma.

Tukumbushane hata kupotea kwa sanane walisema hivyo hivyo. Ila mpaka sasa hawajafanya lolote na hajulikani Sanane alipo.

Haiwezekani mtu apotee Tanzania hii asijulikane alipo. Leo Roma anapigiwa simu inapatikana lakini haipokelewi. Hata message za Whattsup zinaonesha kufika na kusomwa. Polisi wanashindwa nini kutrack iyo simu ya Roma.

Watanzania Tukiendekeza hii Tabia ya kukaa kimya Watu wanapotea tuu ovyo tutambue kuwa hatuna amani. Hatutofautiani na Rwanda sasa.

Tusikubali haya mambo yatokee katika nchi yetu. Mara ya mwisho matukio kama haya yalitokea ndani ya Uongozi wa Nyerere. Na tunajua ni kwanini watu walikuwa wanapotezwa. Sasa awamu hii inaonesha dalili ya kuwa watanzania atupo safe hata kidogo ndani ya nchi yetu.


USHAURI
KAMA POLISI HAWAJUI ALIPO. VIJANA TUANZISHE KAMPAINI YA KUMSAKA ROMA INCHI NZIMA. NYUMBA HADI NYUMBA. PORI HADI PORI, MILIMA HADI MILIMA. HADI IKULU TWENDE TUKAMSAKANYUE.
 
unamaanisha mwenyeheri Nyerere! tuombe radhi umekosea kumdhalilisha baba wa taifa
 
Kuna matukio ya kupotea watu wenye itikadi ya aina Fulani, na iko wazi kabisa kuwa majibu ya vyombo vinavyohusika na usalama wetu vinatoa majibu mepesi sana. Kuna nini? Wanachukuliwa na nani na wako wapi? Kwa nini wapoteaji ni wale kwenye kuwasema watu wa aina Fulani tuu?
Yuko wapi Saanane? Leo tena siku ya tatu Roma polisi wanasema hajulikani kapelekwa wapi lakini simu iko hewani.
Tumbane Mwigulu aseme anachojua maana toka tukio la bastola kwa Nape inaonyesha usalama wa maisha ya Watanzania umehama kutoka wizara yake uko chini ya kikundi ambacho hana uwezo/mamlaka wa kukigusa.
Polisi si "wanahusika na usalama wa raia na mali zao(?),"sasa unalalamika nini.
 
Nafikiri ni wakati muafaka ofisi kama hizo kua na cctv cameras na kumuweka angalau mlinzi mmoja mlangoni (sijui kama eneo alilochukuliwa halina hivi vitu).
Ishu ya Roma ingeanza kwa kumuuliza mlinzi na kuziangalia rekodi za cctv cameras.

Watanzania bado hatujajifunza kuamua madhara, tunaacha madhara yatokee kisha tuanze kujiuliza tumekosea wapi
 
Lema hapa kawaambia ukweli
Jana kuhusu Ben kwa kutoa mfano wa mtoto wa Maghembe, Mwinyi nk
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Back
Top Bottom