Kwanini Watu waliozaliwa na kukulia Kijijini wakija Mjini inakuwa rahisi kwa wao kufanikiwa kimaisha kuliko wale waliozaliwa na kukulia Mjini?

tang'ana

JF-Expert Member
Apr 3, 2015
11,809
15,059
Hello JF

Nimekuwa nikiona watu wengi waliozaliwa vijijini na kuja mjini kutafuta maisha,wengi wao huwa wanafanikiwa sana kimaisha. Mfano angalia watu kama akina Magufuli, Nyerere, Zitto kabwe, Reginald Mengi, Mkapa, Gachuma na wengine wengi tu

Literally walikuja mjini wakiwa tayari ni vijana wakubwa lakini wamekuwa ni watu waliofanikiwa katika maeneo yao waliyoyatumikia tofauti na watu wengi waliozaliwa maeneo ya Mjini ambao wengi wao tunaona wanashinda vijiweni tu na kujisifia kuwa wao ni born town.

Tatizo ni nini?
 
wanakuwa hawajapigwa misumari ya kutosha amini amini ninalokwambia hapa mjini pana mambo mengi sana ya wivu mbaya watu wanawaumiza wototo wa wenzao ili mradi kumkomoa mzazi asisaidiwe na mtoto amini by 75% hao mateja sio hiyari yao unapigwa kifaa cha bumbunali unakuwa huoni la kufanya mwishowe unaanza ulabu usio na mpango unaona bei kubwa unaanza gongo unaona haifai mwishowe kwisheney tatally DAR ES SALAAM IS A ROOM OF HIGHLY COMPETITIONS pana kila aina ya uovu IA MEETING PLACES OF ALL EVILS na ndio nyumbani kwa hela
 
Watu waliokuona tangu ukiwa mdogo hawawezi kukuona unafanikiwa na kuwazidi
Ndo maana wanasema Nabii hakubaliki kwao
Lazima utoke kwenu uende kwingine ufanikiwe..
Unakwepa wachawi wanaokujua..
Ugenini ni ni rahisi hakuna anaejua plans zako
 
Utafiti wako umethibitishwa na taasisi gani inayotambulika kitaifa na kimataifa? Hata DSM pia kuna vijiji. Maelezo yako hayatoshelezi kushawishi watu wajuao UTAFITI
 
wote uliotolea mifano waliletwa na elimu (tayari kichwani walikuwa safi) mbona wanaojiuza wengi wametoka bush ila mambo si mambo

watu wengi wapo vijijini na wanahamia mijini ko si ajabu wakija 1000 wakafanikiwa 20 lazima uwaone. ila wanaofanikiwa si wengi kiivo

wanaozaliwa mijini kusoma hawataki, wanaishia kuwa chawa tu ndo maana hawafanikiwi.
 
wanaozaliwa mijini kusoma hawataki, wanaishia kuwa chawa tu ndo maana hawafanikiwi.
Mkuu kwani wangapi wamesoma na hawajafanikiwa?

Watu wamjini wengi wamesoma ili wapate ajira na ajira hakuna ndo maana unawaona chawa.

Pia kusoma haikupi guarantee kwamba lazima ufanikiwe.
 
Utafiti wako si yakinifu wapo pia waokulia mjini wakafanikiwa mfano Mo ..kufanikiwa hakuitaji mjini Au kijijini kunaitaji uthubutu na kuwa karibu na watu wenye kukuonesha njia ya mafanikio” ndio wanaita connection”
MO hizo mali ni za urithi....usimfananishe na watu kama akina mzee Mengi ambao wameanza from scratch.
 
Utafiti wako si yakinifu wapo pia waokulia mjini wakafanikiwa mfano Mo ..kufanikiwa hakuitaji mjini Au kijijini kunaitaji uthubutu na kuwa karibu na watu wenye kukuonesha njia ya mafanikio” ndio wanaita connection”
Watu wanaongelea hustlers we unaongelea warithi!??
 
Watu waliokuona tangu ukiwa mdogo hawawezi kukuona unafanikiwa na kuwazidi
Ndo maana wanasema Nabii hakubaliki kwao
Lazima utoke kwenu uende kwingine ufanikiwe..
Unakwepa wachawi wanaokujua..
Ugenini ni ni rahisi hakuna anaejua plans zako
Kama ni hivyo tuwachukue watoto waliozaliwa mjini na kukulia mjini tuwapeleke kijijini tuone sasa kama hawatageuka walevi wa mnazi, mbege, rubisi na ulanzi tu
 
Utafiti wako umethibitishwa na taasisi gani inayotambulika kitaifa na kimataifa? Hata DSM pia kuna vijiji. Maelezo yako hayatoshelezi kushawishi watu wajuao UTAFITI
Wapi nimesema kuwa nimefanya utafiti?nilichokisema ni observations zangu tu.
 
waliokuja mjini ni wachache kuliko waliopo mjini kitambo hivyo basi waliozaliwa mjini wakafanikiwa ni wengi
 
Maisha hayana formula, chochote kinaweza kutokea...naamini bahati, kujituma ,
 
Back
Top Bottom