Kwanini watu wakiacha pesa zao benki kwa muda mrefu akiba yao ndiyo inakatwa badala ya wao kupata faida?

Ni njia mojawapo ya kuiwezesha bank kujiendesha.
Kama NMB wanakata 1900 kila mwezi kwa personal account.

Unapotaka kuichimbia pesa mwaka mzima kule piga na mahesabu ya makato yao kabisa.

Pia nikukumbushe tu kutoa pesa dirishani ni 4000/= makato ila kwny ATM ni 900/=

Pia kutuma fedha kwa NMB mobile ni gharama zaidi kuliko kuitoa na kuituma kwa njia tofauti na hiyo.

Wengi wetu tunafanya miamala bila kufahamu tozo.
Kwa NMB Mobile Bank kulipia Bills za Maji,Umeme,TRA na kununua muda wa maongezi katika simu wanakata Pesa nijulishe mkuuu
 
Kwahiyo wewe unaoona huo utaratibu wa kukata hela kweye akiba ya mtu ambaye kaziacha tu ni sawa?

Siyo kila utaratibu uliowekwa na haya mabenki uko sawa,moja wapo ni huu uondolewe
Mtoa mada yuko sahihi sana.
Hata Mimi inaniboa sana kuweka hela benki.
Labda pesa kuanzia milioni 5 kwenda mbele ndio huwa nawaza kupeleka benki.
Vinginevyo ni hasara tupu.
Ukipiga mahesabu ni hasara tupu.
 
Nikazi kubwa sana mkuu, ila nnachojua ni kuwaambia tu nataka akaunt ambayo haina makato ya kila mwezi, sio kila benki wana hiyo akaunti, wengine hawana.

Kuna nyingine ni nzuri zaidi sema ina masharti kwenye kutoa, unatoa mara nne tu kwa mwaka, lakini unapewa asilimia ya riba kutokana na kiasi unachokua nacho benki. KCB anaiita Simba, hii benki nyingi wanazo ila ndio iwe ya kujiwekea akiba tu na sio ile ambayo utakua unatoa pesa mara kwa mara.
nenda kaweke equity bank, hawana makato
 
nenda kaweke equity bank, hawana makato

Nashukuru Mkuu, huko nna akaunti ya USD. Hawana makato ya kila mwezi, unakatwa unapofanya muamala tu.

Tatizo hawana ATM kwa hizo USD ambapo sio tatizo sana kwa upande wangu.
 
In a big picha ...

Kabla hujaweka fedha bank ni vema ukajiuliza, kwanini hizi hela nisikae nazo mwenyewe mfukoni ama nyumbani?

Zipo baadhi ya nyakati ni bora kubaki na hela zako mfukoni ama nyumbani kuliko kuzipeleka bank, kwa mfano:

- Kama una hela kidogo sana
- Kama gharama ya kuziweka bank ni kubwa kuliko ile ya kuzitunza mwenyewe

Sasa basi:

(1) Kama sababu kuu ya wewe kupeleka fedha bank ni ili bank ikusaidie kuzitunza coz ukikaa nazo unaogopa kuzipoteza ama kulia bata then hapo lazima uwalipe kidogo kwa kukulindia, kumbuka, wataziwekea bima na ulinzi wa kimazingira pia

(2) Kama unapeleka ili upate faida zaidi then, waambie na watakuelekeza kwa kiasi ulicho nacho hata kama ni kidogo ni kwa asilimia ngapi wanaweza kukufidia kwa kukaa na fedha zako

- Mwisho, kwenye kila bidhaa ya kibenki huwa kuna terms na conditions .... ukiweza, pata muda kuzisoma kabla ya kujiunga

Usiende tu bank kama unaingia super market kwamba chochote kitakachokuvutia utanunua
 
Ni njia mojawapo ya kuiwezesha bank kujiendesha.
Kama NMB wanakata 1900 kila mwezi kwa personal account.

Unapotaka kuichimbia pesa mwaka mzima kule piga na mahesabu ya makato yao kabisa.

Pia nikukumbushe tu kutoa pesa dirishani ni 4000/= makato ila kwny ATM ni 900/=

Pia kutuma fedha kwa NMB mobile ni gharama zaidi kuliko kuitoa na kuituma kwa njia tofauti na hiyo.

Wengi wetu tunafanya miamala bila kufahamu tozo.
Iyo pesa ya kutolea 900 na list au bila list
Nijulishe
 
Mobile money ni nzuri ila makato yake sasa kwenye kutoa na kutuma
 
Mkuu, sijasema ni sawa, lakini wao wanakutoza pesa kwa ajili ya kukupa huduma ya kukutunzia pesa zako.
Mimi akaunti yangu nakatwa pale nnapoenda kutoa pesa tu, mambo ya makato ya mwisho wa mwezi hayapo.
Ndio maana nikasisitiza kuelewa aina tofautitofauti za akaunti za uendeshaji wake. Nafikiri tumeelewana
Account gani iyo mkuu, ndo saving account au vipi
 
Back
Top Bottom