Kwanini watu wa uswahilini ni waoga sana juu ya wageni?

gwankaja

JF-Expert Member
May 16, 2011
5,910
2,000
Wadau mara nyingi watu ambao ambao wanaishi haya maeneo huwa wanaogopa sana watu wageni na wasiowafahamu..
Ni zaidi ya mara moja mimi nimeshindwa kufika/kupata watu ninawahitaji wakihofia eti mimi ni polisi, mara ya kwanza ilikuwa naenda kwa ndugu yangu na nilielekezwa tu mitaa anayokaa..niliuliza sana kila mtu anasema hamjui..mtu wa mwisho baada ya kujieleza sana ndo akanipeleka na kunipa ABC kwanini wale watu walikana kumfahamu yule ndugu yangu, eti walihofia nisije nikawa polisi..

Majuzi nilienda mitaa inayofanana na hiyo, huko kuna binti nina mahusiano naye ..ilipita muda sijaonana naye na simu yake ikawa haipatikani! Kwao napafahamu vizuri ila nilienda nyumba moja karibu na pale kwao na kumuulizia..cha ajabu walimkana kabisa eti huyo mtu hawamjui wala hawajawahi kumsikia..nikabaki nacheka tu moyoni! Sasa leo nimeonana na huyu binti akaniambia kwamba walimwambia nilienda ila kwakuwa hawajawahi kuniona wakaogopa kumtaja kwamba wanamfahamu!

Sasa ninachojiuliza, hawa watu kwaninu wanakuwa wanajihami sana..hata kama mimi ni polisi je ni halali kwao kuficha wahalifu? Je ni kulindana au wanakosa uelewa tu?
 
Castr

JF-Expert Member
Apr 5, 2014
17,510
2,000
Hiyo uswahilini ya mkoa gani? mkoa wa Dar es Salaam uswahilini kote nilipoishi na kutembea hivyo vitu vilikua zamani enzi hizo polisi polisi kweli na sungu sungu wanakimbia hadi unajiuliza kwanini wasijiunge riadha.

Mleta uzi unaonekana ni mtoto wa kishua hujui hata jinsi ya kuongea na kujipresent mbele ya mtu kutoka uswahilini.
Ukienda umevaa kiofisi halafu suruali inapepeaaaa na umenyoa panki watu watakutafsiri wewe ni polisi (zamani ilikua unapigwa ukihisiwa wewe ni polisi).

Jaribu hivi, vaa pensi ila lisiwe pensi nyanya (utaonekana mshamba utakabwa), na raba au sendoz na fulana saizi yako.
Usivae cheni zaidi ya moja au pete isiwe zaidi ya ya ndoa.
Unapoenda karibu na eneo ukikuta watu wanacheza drafti au pool table kaa hapo cheza hata na watu wawili, kisha mfuate unayemuona unamuweza halafu ulizia unayemtaka.

N.B. Hiyo process yote unaweza kuivunja kama utaweza kwenda huku umevaa sare za shule za Sekondari au Msingi.
 
Poa poa mkuu umesomeka!
 
Murano

JF-Expert Member
Mar 11, 2012
2,063

Very true jamaa alifeli kwenye mavazi, mavazi yake yalikuwa serious sana na ukiangalia wabongo tunamjudge mtu kwa mavazi
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom