Kwanini watu wa diaspora, mfano black Americans na kutoka nchi nyingine nje ya bara la Africa, wanakimbia Tanzania

Gilbertlit

Member
Jun 10, 2021
25
10
Habari wana jamvi natumai mko poa, leo nimeona ngoja niletea huu uzi hapa kwenu wana jamvi juu ya hili swala.

Kipindi cha nyuma kidogo kama miaka mitatu hivi au minne watu wenye asili ya Africa toka nchi kama Marekani na Uingereza walikuwa wanapenda sana kuja Tanzania, wengine kuhamia kabisa, mpaka ikafikia kipindi ikawa siyo siri tena hata ukienda YouTube unakuta wengi wana kiri kuipenda Tanzania na wengine wamesha hamia kabisa wanafanya YouTube videos kuisifia nchi yetu.

Lakini sasa hivi naona kama upepo una badilika polepole, wengi wao sasa wanaiponda Tanzania tena wengine wamefikia hatua ya kutangaza kuhama na kwenda kuhamia nchi nyingine kama Kenya, Rwanda, na hasa hasa Ghana.

Nini haswa sababu ya wao kuhama Tanzania na kwenda hizo nchi nyingine. Tukumbuke kuwa hawa wakija nchi zetu hizi wengi wao wanakuja na ujuzi, elimu au maarifa tofauti, wanachangia kuleta hela ndani ya nchi mwisho wa siku uchumi wetu unakua, pia hata mitaa yetu ina changamka zaidi, ila cha kushangaza sasa hivi ukiingia YouTube videos nyingi za hawa Diaspora ni kuhusu WHY I LEFT TANZANIA, WHY I DECIDED TO RELOCATE FROM TANZANIA.

Na video nyingi sana ni za hivi karibuni.

SHIDA NI NINI HASA.

Tupeane mawazo.


Screenshot_20210717-171533.jpg
 
Back
Top Bottom