Kwanini watu husahau kusema 'KAMA UNAYO' pale wanapoomba pesa

fuma

JF-Expert Member
Oct 3, 2016
214
407
Kuna hii tabia ya mtu(unayemfahamu na anayekufahamu kabisa) anakutumia SMS yenye kusema......'naomba unisaidie sh.elfu kumi...nisaidie nina shida'

Unabaki unajiuliza huyu jamaa ana uhakika gani kama niko na hii kitu...kwann watu tunasahau haka kasentensi??? 'kama unayo'
 
Jibu la ms lincoln limejitosheleza
Unajitosheleza?

Shukran mkuu kwa jibu murua
Inabidi ujifunze utaratibu wa kuishi ndani ya uwezo wako.Siombi ili nisiombwe,sikopi ili nisikopeshe.,mara nyingi sio mara zote.Naepuka kukopa sana sana,kwanza ukiniingizia habari za hela natetemeka kabisa.Kukopeshana kunavunja undugu na urafiki.
 
Kukopa haimaanishi kwamba unaishi nje ha uwezo wako.
 
unaogopa mikopo ya kitaasisi au mikopo ya kijamii huko nyumbani? Maana BOT wametoa utafiti unaonesha watanzania Wengi wanaogopa mikopo
 
Sasa mtu anakuja kukopa hela ndogo,ndogo kiasi kwamba ukimtafakari unaona uwezo wa kuingia mitini ni mkubwa sana,au mpaka utaona aibu kudai.Pili mtu anakwepa maswala ya kumkopesha mtu na kumdirect saccos au mkopo wa riba kwa kuepuka usumbufu.
Kukopa haimaanishi kuishi nje ya uwezo wako,ndio maana kwenye sentensi yangu nimesema mara nyingi,sio mara zote.Mwaka unaweza kupita hata miaka 2.Naogopa kuresort kwenye mkopo kwa kuwa huwa NAONA UCHUNGU KULIPA,mpaka iwepo pressing matter.
 
Unaweza usiwe unajitosheleza bali unajibana uishi kulingana na mazingira uliyopo. Usipokua tayari kuliwa huli maana kama ni mwanamke akitaka maisha ghali huku uwezo hana ndio mwanzo wa madeni lukuki,michepuko kibao.
Halijajitosheleza abadani, mnachodhani nyie ni kwamba mtu anakopa kwasababu anaishi nje ya uwezo wake kifedha. Haiko hivyo.
Kuna wengine wanaomba hela wakiwa hawana shida kubwa basi tu kazoea maisha ya kuomba omba,wengine wanakua na shida kweli ila tatizo hajali huyo anayemuomba ana hela au hana yeye anachotaka ni kuambiwa ipo ntakupa
 
Mkopo hatari kuna watu watatu walinikopa,kwenye kudai ndio shughuli dana dana kibao mpaka kununiana. Mtu anakopa anasema ntakurudishia wiki ijayo inakua miezi ijayo.

Wale wa kuomba hela wanatumia mbinu ya una mia tano hapo au una elfu kumi hapo ukimpa ukidhan atarudisha baadae ndio imetoka hio hesabu umetoa msaada
Sasa mtu anakuja kukopa hela ndogo,ndogo kiasi kwamba ukimtafakari unaona uwezo wa kuingia mitini ni mkubwa sana,au mpaka utaona aibu kudai.Pili mtu anakwepa maswala ya kumkopesha mtu na kumdirect saccos au mkopo wa riba kwa kuepuka usumbufu.
Kukopa haimaanishi kuishi nje ya uwezo wako,ndio maana kwenye sentensi yangu nimesema mara nyingi,sio mara zote.Mwaka unaweza kupita hata miaka 2.Naogopa kuresort kwenye mkopo kwa kuwa huwa NAONA UCHUNGU KULIPA,mpaka iwepo pressing matter.
 
Inashangaza pale mtu anapokuomba msaada wa pesa na ukimwambia hauna, anakukasirikia na kushindwa kabisa kuficha hisia zake.

Cha ajabu ni kwamba wewe hata siku moja haujawahi kuthubutu kumuomba yeye huo msaada wa pesa.
 
unaogopa mikopo ya kitaasisi au mikopo ya kijamii huko nyumbani? Maana BOT wametoa utafiti unaonesha watanzania Wengi wanaogopa mikopo
Mkopo wa kijamii.
Wa kitaasisi nikipata nafasi ya ku-abscond malipo naitumia vyema.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom