Kwanini watoto wanawatunza mama zao kuliko baba zao?

Tabutupu

JF-Expert Member
Nov 26, 2010
13,108
18,325
Nimeona familia nyingi, mshua kama hana pesa anakuwa na maisha magumu sana uzeeni kwa sababu mara nyingi watoto wanapitisha fedha kwa mama.

Pia wanaume sio wepesi sana kuomba fedha kwa watoto , wengine wanasema hii inaweza kuwa sababu wanaume wengi kufa haraka.

Wale vijana, hakikisheni mnaoa wanawake ambao watawajali uzeeni au tafuteni miradi ambayo itawapa pesa uzeeni .

Mnasomesha watoto, lakini link za watoto zipo kwa mama.
 
Tatizo wamama nao wakitumiwa pesa anaifudumia kibindoni yn hata hasemi kua tumetumiwa pesa hii hapa yani unajikuta umetuma pesa leo then kwa kesho yake ukapiga simu kwa mzee kumjulia hali tu ila ukagundua kabisa mzee hana taarifa nakile kiasi nilichotuma
 
Umewahi kusikia ule usemi, "Greda linatumika kutengeneza barabara lakini likishamaliza haliruhusiwi kupita barabarani".

Baba atateseka kuwapeleka watoto shule, kuwalisha na kuwavalisha lakini heshima yote ataibeba mama coz watoto wapo karibu na mama yao kuliko baba.
 
Kutokana na hali ya maisha na utaratibu wetu wa maisha. Baba anakua busy kutafuta pesa za matunzo ya familia kitu ambacho kinampa mama nafasi ya kuwa na watoto zaidi kwa hio watoto wana bond zaid na mama na hawakumbuki baba alikua anaadimika kwa ajili yao. Baba kama ni mnywaji hali ndo inakua mbaya zaid uzeen.

semper fidelis
 
Na mzee ukimtumia anapigia pombe yote.
Tatizo wamama nao wakitumiwa pesa anaifudumia kibindoni yn hata hasemi kua tumetumiwa pesa hii hapa yani unajikuta umetuma pesa leo then kwa kesho yake ukapiga simu kwa mzee kumjulia hali tu ila ukagundua kabisa mzee hana taarifa nakile kiasi nilichotuma
 
Haaaaa.. wanaume jipangeni , ezee ni kazi
Umewahi kusikia ule usemi, "Greda linatumika kutengeneza barabara lakini likishamaliza haliruhusiwi kupita barabarani".

Baba atateseka kuwapeleka watoto shule, kuwalisha na kuwavalisha lakini heshima yote ataibeba mama coz watoto wapo karibu na mama yao kuliko baba.
 
Changamoto kubwa niliyo jifunza kwa wazee wengi ni:-

1- Wakati wa ujana, ningumu sana kumtambua kama mke atatutunza uzeeni.
Pia sisi wanaume tumekuwa tukiwatesa sana na kuwajeruhi wake zetu kipindi cha ujana wetu hali ambayo hupelekea mke kuishi na majeraha huku akipoteza upendo kwa mume na kuishi kwenye ndoa kwaajili ya watoto (huwa wanasema kwamba, nasubiri wanangu wakuwe). Hivyo basi wamama wengi huishi na kuzeeka kwenye ndoa wakiwa wamekufa mioyo.

Alafu wababa ni ngumu kuwaeleza watoto matatizo ya mama zao, lakini kinyume chake hili ni tatizo kubwa kwa wamama kiwaeleza mambo wananyo yapitia pamoja na changamoto za baba zao. Hii hali ya kuwaeleza negativity watoto hujijrnga akilini mwao na hivyo watoto huanza kujaa sumu na chuki kwa baba zao.

2- Pia nijukumu la baba kuandaa maisha yake na mkewe pindi watakapo zeeka.
Hapa wazazi tunasahau na kusema eti tunawekeza kwa kuwasomesha watoto, lakini tunasahau kwamba hawa watoto hawakuomba tuwazae, na bali tuliwazaa kwa starehe zetu. Hivyo basi, kumsomesha mtoto ni jambo la lazima ili kumuandalia maisha yake.
 
Inabidi kuanza kujisort mapema wakati nguvu bado zipo. Hii ipo sana. Mtoto anaenda home kutembea ila wakati wa kutoka mzee anapewa 10 ya bia huku mother anakunjiwa hata kilo kwenye kiganja.

Wanaume hatuaminiki. Ukipewa nyingi hukawii kwenda kuhonga kwa vibinti...
 
Madingi tatizo tunaviburi..😅
Ukimtumia mzee hela itapigwa ganji ya kula home itaenda kidogo!.. kule sasa kwenye waiter leta nyengine zitaenda asilimia 90!!
Halafu sisi tunakuwaga makaksi Sana kwa watoto!!
Idara ya vipondo tumepewa sisi!!
Mtoto akifanya kosa utasikia ngoja baba yako aje..😜
Na akija ni tifu kweli Sasa tutapendwajwe na watoto kama Mambo yenyewe ndo hivyo!!

Ukiingia tu watoto wanapoteana..😂
Dah! The dingi a.k.a the baba ni Moto mwengine huo!

Nitajitahidi nikipata watoto niweke bond nao ili ntakapokuwa namapengo nisiteseke ila wakizidi kitaeleweka kenge!!.. misimamo ya kibishi lazima isimame ukiwadekeza itakula kwako 😅
 
Haaaaa..
Inabidi kuanza kujisort mapema wakati nguvu bado zipo. Hii ipo sana. Mtoto anaenda home kutembea ila wakati wa kutoka mzee anapewa 10 ya bia huku mother anakunjiwa hata kilo kwenye kiganja.

Wanaume hatuaminiki. Ukipewa nyingi hukawii kwenda kuhonga kwa vibinti...
 
Sisi wote tunao changia mada umu ni watoto je tunawatunza baba zetu Kama mama zetu? Kama Sio wote tukubaliane tukitoka umu tuanze kutoa 50% 50% kwa baba na mama naiman tukiweza baada ya miaka Mia itakua dunia mzima infanya lakin tukiwa na sisi Kama watoto tunakuja jamiforums kutoa Uzi alafu tukitoka tu tunakimbilia kwa Mama zetu, Yan wengine umu kuongea na baba zao ni mpaka awe anaongea na mama yake akisha maliza zile dakika mbili zilizo Baki ndio utasikia Mama Kama upo na baba Apo mpe nimsalimie

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ni malezi tu, kuna watu wanawapenda baba zao hadi too much.
wanaume wanasahau kua, pesa unazotoa kwa mtoto kwa mahitaji na shule pekee havitoshi,

Maneno ya baba kwa mtoto ni Muhimu sana, na sio pindi kakosea tu, wakati ambao kupo shwali ndio wasaa mzur wakuongea na kijana.
 
KENZY
Kumbuka mtoto ‘anayetuma’ hela ama kutunza wazazi sio mtoto tena, ni mkubwa sasa na huenda anao watoto tayari... anapoyafanya hayo yeye anajiona wapo akizeeka.?

Ninachojifunza hapa ni tujiandae kujitunza wenyewe, tulee na kuwaandaa watoto wakajitegemee ila sio kwa ‘all out’ phenomena... tuzingatie kuwa panapo uzima tutazeeka hivyo tuwe na akiba yetu kwa ajili ya uzeeni.

Nature inatutinga kujenga hiyo so called bond, mishe nyingi za hapa na pale ndo kipatikane chochote kitu... and ofkozi vichapo na mateso kwa wake zetu husimuliwa watoto na kujenga chuki.
 
Madingi tatizo tunaviburi..
Ukimtumia mzee hela itapigwa ganji ya kula home itaenda kidogo!.. kule sasa kwenye waiter leta nyengine zitaenda asilimia 90!!
Halafu sisi tunakuwaga makaksi Sana kwa watoto!!
Idara ya vipondo tumepewa sisi!!
Mtoto akifanya kosa utasikia ngoja baba yako aje..
Na akija ni tifu kweli Sasa tutapendwajwe na watoto kama Mambo yenyewe ndo hivyo!!

Ukiingia tu watoto wanapoteana..
Dah! The dingi a.k.a the baba ni Moto mwengine huo!

Nitajitahidi nikipata watoto niweke bond nao ili ntakapokuwa namapengo nisiteseke ila wakizidi kitaeleweka kenge!!.. misimamo ya kibishi lazima isimame ukiwadekeza itakula kwako
Dah! Basi kwa namna hiyo ni ngumu sana mdingi kuwa na bond kama aliyonayo mama kwa watoto kwasabu ni lazima atokee mzazi mmoja mwenye msimamo kuweka sawa misingi kwa watoto na hapa ndipo wamama wanapochukua points za bure kwa watoto kwasabu mdingi ndo utaachiwa upambane na mwisho kuonekama kama gaidi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom