Kwanini watoto waliozaliwa nje ya ndoa huwa hawatajwi na baba zao pale wanapoulizwa wana watoto wangapi?

Equation x

JF-Expert Member
Sep 3, 2017
29,268
40,052
Imekuwa ni desturi kwa watu walio wengi, hasa kwa wanaume waliozaa nje ya ndoa, kutokuwaweka katika listi watoto waliozaa nje ya ndoa.

Kama wataulizwa mbele za watu; wana watoto wangapi? Watajibu kwa kuwataja wale tu, aliowazaa ndani ya ndoa. Na wale aliowazaa nje, hatowataja.

Iwapo, wale watoto waliozaliwa nje ya ndoa, watakuwa na mafanikio makubwa; wababa ndio wanakuwa wa kwanza kujinadi kwa kusema, yule ni mtoto wangu.

Sasa nauliza swali; Kwa nini watoto waliozaliwa nje ya ndoa, huwa hawatajwi na baba zao?
 
Mwanaume hajui idadi halisi ya watoto katika maisha yake,, Kama alitia mimba mwanamke na asimwambie!!hata kwenye sensa hilo swali huulizwa mwanamke tafiti za kuongezeka au kupungua kwa vizazi hufanyiwa wanawake,,
Kwa mantiki hiyo, sisi wanaume hatuna watoto...inawezekana watoto tulionao sio mbegu zetu; hapo unasemaje?
 
Jimmy Gordon
Cobbleport
Bruce Wayne
Don Falcon
Fishy
Havley
Pyg
Edmund Ed
Lee
Barbara
Seline
Sarah
Butch
Zczacy
Ra's Al Gul
 
Njooo wazinzi wa njee ya ndoa mjibu swalii hili .maana hao watoto wa njee ya ndoa mkifaga bilaa kuwatambulisha kwa ndugu jamaa,mkeo na watt wako wandani ya ndoa ,cku mkifaga mnawaachaga hao watt ktk mazingira magumuu sanaaa ,HAMJUI TU.
 
Imekuwa ni desturi kwa watu walio wengi, hasa kwa wanaume waliozaa nje ya ndoa, kutokuwaweka katika listi watoto waliozaa nje ya ndoa.

Kama wataulizwa mbele za watu; wana watoto wangapi? Watajibu kwa kuwataja wale tu, aliowazaa ndani ya ndoa. Na wale aliowazaa nje, hatowataja.

Iwapo, wale watoto waliozaliwa nje ya ndoa, watakuwa na mafanikio makubwa; wababa ndio wanakuwa wa kwanza kujinadi kwa kusema, yule ni mtoto wangu.

Sasa nauliza swali; Kwa nini watoto waliozaliwa nje ya ndoa, huwa hawatajwi na baba zao?
naunga hoja mkono
 
Mwanaume mwenye akili lazima atambulishe watoto wake wote kwa ndugu zake.
Maana hao ndio ndugu zao.
Mke sio lazima ajue, maana Hana undugu nao. Atapambana nao kwenye mirathi.
Kuwanyima hawezi na Hana namna ya kuwaondoa.
Mwanaume hutakiwi kumficha mwanao.
Ni ujinga kulea watoto wa kufikia wa mke aafu wanao unawaficha
 
Mim naona Kuna sabab zifuatazo:
1. Wanaume weng wanaopga mimba huwa hawana uhakika kuwa hyo mimba ni yake au kasingiziwa,hapa na akina mama lazma tuwalaum,maana unaweza ukamkuta mwanamke anatembea na wanaume lukuki,haraf akipata ujauzito anampoint mmoja wapo. Huyu aliepointiwa lazma awe na Mashaka,hawez akaamin kwa asilimia Mia.
2.Weng wanahofia usalama wa ndoa zao
3.Economic factor
4.Religion factor
 
Back
Top Bottom