Kwanini watoto wa watumishi wa Mungu hawana maadili mazuri?

omosangora

Member
Oct 29, 2017
53
26
Wanajamvi mm si mwenyeji sana humu japo huwa nasoma sana humu jamvini na kujifunza kutokana na mijadala mbalimbali inayotolewa humu ndani,

Leo nimejitokeza kwenu kutaka msaada wa kimawazo
Kuna watumishi wa Mungu wanaitwa wachungaji nimekuwa nikifuatilia familia zao hususani watoto wao kwanini hawana maadili ili hali baba zao ni wachungaji wa kiroho?

Naomba kuwasilisha tafadhali
 
Wanajamvi mm si mwenyeji sana humu japo huwa nasoma sana humu jamvini na kujifunza kutokana na mijadara mbalimbali inayotolewa humu ndani,Leo nimejitokeza kwenu kutaka msaada wa kiwazo kuna watumishi wa mungu wanaitwa wachungaji nimekuwa nikifatilia familia zao hususa watoto wao kwanini hawana maadili ili halo baba zao ni wachungaji wa kiroho? Naomba kuwasilisha tafadhali
Maombi hawayaelekezi kwa familia zao, wanamuombea mpendakuombewa na mpendasifa mkuu mr. Jaramogi Punda Milia
 
Shetani akishindwa kukupiga moja kwa moja (mwili, nafsi na roho yako) hukupiga kupitia vinavyokuzunguka kama vile mke, watoto, mali, marafiki n.k Hivyo watumishi wengi wa Mungu shetani huwapata kirahisi zaidi kwa vita ya nje ikiwemo watoto wao. Wakati kwa asiye mtumishi anapigwa kirahisi zaidi yaani magonjwa n.k
 
Ni kweli kabisa best friend wangu ni mtoto wa mchungaji. Wakati tupo chuo mwaka wa kwanza alikua ananisihi sana niache gambe tulipofika mwaka wa pili dah sio gambe tu alikua anapiga fegi, bangi na mademu kama kawaida na kabla hatujamaliza chuo mwaka wa nne jamaa alikua na mtoto tayari. Sema wazazi wake hawajui kama mtoto wao alipinda kiasi kile. tulikua kukirudi likizo jamaa anakua mfano wa kuigwa hakosi kanisani na kwenye kwaya kama kawaida kumbe nyuma ya pazia kaficha mengi.
 
Correct hata mm kuna mchungaji tunakaa karibu na home na kanisa lake lipo hapa toka mwaka 1993 na ana watoto mixer ke&me sasa hao watoto ni vituko mmoja huyo (ke)alikuwa anasoma bordng,alikuwa analuka ukuta shule na kwenda kupigwa dudu na masela,huyu mwingine alianza kiburi yani hata chech alikuwa haend kisa anamchukia babaake na mamaake sabau walikuwa et wanaingilia maamuzi yake jeuli ilipo zidi akahama home kabisa na kujichanganya vijiwen.jamaa alikuwa ashauliki baaday akawa mlandukaji mzuri sana wa ndumu na embassy. sielewi kwa nini watoto wa wachungaji huwa wanakuwa kivi?..

By Mahenge jr
(maisha ni popote.)
 
Wanajamvi mm si mwenyeji sana humu japo huwa nasoma sana humu jamvini na kujifunza kutokana na mijadala mbalimbali inayotolewa humu ndani,

Leo nimejitokeza kwenu kutaka msaada wa kimawazo
Kuna watumishi wa Mungu wanaitwa wachungaji nimekuwa nikifuatilia familia zao hususani watoto wao kwanini hawana maadili ili hali baba zao ni wachungaji wa kiroho?

Naomba kuwasilisha tafadhali
Shetani anawawinda sana watumishi wa Mungu wakiwemo Mapandri, Maaskofu, Wachungaji n.k Hivyo tunpaswa kuwaombea sana. Shatani anaposhindwa kuwashughulikia hawa moja kwa moja anatafuta hatanamna ya kuwadhalilisha ikiwemo kuharibika kwa watoto n.k.
Tunatakiwa kuwaombea sana.
 
Wanajamvi mm si mwenyeji sana humu japo huwa nasoma sana humu jamvini na kujifunza kutokana na mijadala mbalimbali inayotolewa humu ndani,

Leo nimejitokeza kwenu kutaka msaada wa kimawazo
Kuna watumishi wa Mungu wanaitwa wachungaji nimekuwa nikifuatilia familia zao hususani watoto wao kwanini hawana maadili ili hali baba zao ni wachungaji wa kiroho?

Naomba kuwasilisha tafadhali
Maelezo yako bila mifano iliyo hai kwangu naona kama porojo tu
 
Kila mtu na roho, nafsi yake wala hamtofanana hata siku moja hata Yesu alikuwa na wanafunzi anaiwaamini lakini mwisho wa siku yuda akamgeuka.
 
Si lazima kwa sababu wewe ni mchungaji kwamba mwanao awe mtu mwema kwenye jamii.

Kila mtu Ana destiny yake hapa duniani kwa jinsi anavyojipangia.

Mchungaji anao wadhfa wakimfundisha tu mwanae ya kwamba ni kipi kizur na kipi kibaya.

Haitaji kuchungwa ili kua mkamilifu ulimwenguni.
 
Wao wapo busy kutoa borit kwa jiran wanasahau kutoa zao kwanza
 
Maisha ndo yamepelekea wengi kuwa Watumishi ila Wenyewe hawakuwa na Ndoto hizo unatarajia nini hapo???
 
Shetani akishindwa kukupiga moja kwa moja (mwili, nafsi na roho yako) hukupiga kupitia vinavyokuzunguka kama vile mke, watoto, mali, marafiki n.k Hivyo watumishi wengi wa Mungu shetani huwapata kirahisi zaidi kwa vita ya nje ikiwemo watoto wao. Wakati kwa asiye mtumishi anapigwa kirahisi zaidi yaani magonjwa n.k
nimekusoma mnoo 100%
 
Maisha waliyokuzwa yanawachosha ndiyo maana wanaamua kufanya kitu kinaitwa "having a change of a scene"! Wanaingia kwenye vitu ambavyo hawavifahamu ndiyo maana wanapotea.
 
nasubiri wahenga waliosema chini ya mwembe huwezi kuokota mapera waje kujibu hapa.
 
Kila mtu na akili zake.
Hatuwezi laumu wachg coz akili na utashi ni wa mtu husika.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom