Kwanini Watanzania wengi wanaonekana hawana hamasa ya kupiga kura uchaguzi wa Serikali za mitaa 2019?

1.Uandikishaji umeanza nyakati za mvua, Hii ni changamoto.
2.Watanzania tumezoea deadline ikikaribia ndio tunaanza kujivuta kwenda kujiandikisha.
3.Zoezi bado changa na vituo viko vya kutosha hivyo watu hawana presha ya uwingi wanaendelea kusubiri(subira yavuta heri).
4.Wananchi wengi bado wanahangaikia ID za taifa (NIN), wakitoka huko watakuja kujiandikisha.
5.Kuna watu tayari wametengeneza matokeo yao kichwani hivyo hawaoni umuhimu wa kupiga kura.

IJIKO
 
Siyo kweli, labda hali itakuwa mbaya zaidi kwa Wachaga kwa kushindwa vibaya zaidi kwa Mbowe na chadema!

Hao wachagga unaowaongelea wao ni level nyingine kabisa...................... wakati ninyi mkijikushanya Waganga wa kiengyeji Gambosh... wao wanazindua ATM ya maziwa uko hapo? wao wako mbele kabisa kimaendeleo na hata kiali wewe kaa hapo ukisifia visivyo na maana kabisa.
 
Wakuu wa wilaya, polisi, tume ya uchaguzi na wakurugenzi ndo wanaamua mshindi na sio wapiga kura..
Sasa kuna sababu gani ya kujisumbua..
 
Najua wengi watanipinga ila ukweli ni kwamba watu wengi wanaonekana hawana mudi wala mpango wa kupiga kura wala kushiriki uchaguzi mdogo huu wa serikali jambo hili nimelishuhudia

Safari hii kuna gali linapita mtaani kwangu likihamasishe watu wakajisajili majina yao ili waweze kushiriki uchaguzi huu wa serikali mtaa kitu nilichoshangaa watu wengi wako bize na shughuli zao hata hawamsikilizi mtoa matangazo, wengi yaani tofauti na zamani nilikuwa na hamsha hamsha ya uchaguzi ila safari hiii sijui ni mini tatizo.
Kura gani? Hivi sasa kuna mchakato wa kuandikisha wale vijana ambao wamefikia umri wa kupiga kura. Suala la kuwa watu hawana mpango wa kupiga kura, ngoja wakati wa uchaguzi ndipo uweze kuongelea hilo.
 
Najua wengi watanipinga ila ukweli ni kwamba watu wengi wanaonekana hawana mudi wala mpango wa kupiga kura wala kushiriki uchaguzi mdogo huu wa serikali jambo hili nimelishuhudia
Safari hii kuna gali linapita mtaani kwangu likihamasishe watu wakajisajili majina yao ili waweze kushiriki uchaguzi huu wa serikali mtaa kitu nilichoshangaa watu wengi wako bize na shughuli zao hata hawamsikilizi mtoa matangazo, wengi yaani tofauti na zamani nilikuwa na hamsha hamsha ya uchaguzi ila safari hiii sijui ni mini tatizo.
Jana Mkurugenzi wa Manispaa kwenye mkutano na wafanyabiashara anawataka wamchague mgombea wa CCM!
Wanapanga wenyewe, wanatangaza wenyewe, wanaendelea kukampeni wenyewe, watasimamia wenyewe, watahesabu kura wenyewe, watamtangaza mshindi wenyewe na watasherehekea wenyewe. Wamefagia magereza kwa kutoa misamaha ya wahujumu ili nafasi ziwepo kwa wapinzani watakaolalamikia mwenendo wa uchaguzi.
 
Utasikia muda si mrefu kuna watumishi wa serikali watatumbuliwa kwa kosa la kutokupiga kura
 
Hao wachagga unaowaongelea wao ni level nyingine kabisa...................... wakati ninyi mkijikushanya Waganga wa kiengyeji Gambosh... wao wanazindua ATM ya maziwa uko hapo? wao wako mbele kabisa kimaendeleo na hata kiali wewe kaa hapo ukisifia visivyo na maana kabisa.

Hahaha naunga mkono hoja, wepi hao wana atm maziwa? Uru, Rombo, Marangu au wa Kibosho?
 
Ungesema Chadema ndio wamekata tamaa ingependeza zaidi.Arusha na Moshi nimepita kule chadema wengi wameapa hawaji piga kura milele.Sijajua sababu Ni Nini.
Sababu matokeo ya uchaguzi yanajulikana. Same kama kwenye by elections zilizopita. Iwe isiwe, lazima mgombea wa chama atangazwe mshindi. Common sense....!!!
 
Tunaojitambua hatutapoteza muda tena hata kujiandikisha hatuendi ni kupotezeana muda tu.
Watangaze tu watu wao. Kwangu nathamini sana viongoizi wangu wa NZENGO tunaosaidiana nao katika taabu na furaha zetu mtaani lakini sio hao viongozi wasaka tonge wanaotuletea vurugu nyingi na kuvamia maeneo yetu ya wazi na kuyauza.
 
Maana ya uchaguzi haipo, ikiwa mnao wachagua hawana madaraka kama wanaoteuliwa.
Nadhani wangeteuana tu ikaeleweka.
 
Najua wengi watanipinga ila ukweli ni kwamba watu wengi wanaonekana hawana mudi wala mpango wa kupiga kura wala kushiriki uchaguzi mdogo huu wa serikali jambo hili nimelishuhudia

Safari hii kuna gali linapita mtaani kwangu likihamasishe watu wakajisajili majina yao ili waweze kushiriki uchaguzi huu wa serikali mtaa kitu nilichoshangaa watu wengi wako bize na shughuli zao hata hawamsikilizi mtoa matangazo, wengi yaani tofauti na zamani nilikuwa na hamsha hamsha ya uchaguzi ila safari hiii sijui ni mini tatizo.

Ni vema tukikaa na kutafakari njia ya kuitoa ccm madarakani lakini siyo kwa njia hii ya kura.
 
Hao wachagga unaowaongelea wao ni level nyingine kabisa...................... wakati ninyi mkijikushanya Waganga wa kiengyeji Gambosh... wao wanazindua ATM ya maziwa uko hapo? wao wako mbele kabisa kimaendeleo na hata kiali wewe kaa hapo ukisifia visivyo na maana kabisa.

Usitudanganye hapa,
Huwa nikirudi likizo bongo, lazima nitembelee Arusha na kilimanjaro. Kwakweli, Arusha inakua kwa kasi sana, lkn Moshi iko vile vile, inabadilika pole pole.
Ule mji ni shidaa, hauendelei, umebaki kuwa mji wa matambiko. Ni mizimwi tu kila mahali. Hauna tofauti na gamboshi.
😝😛😝
 
Back
Top Bottom