Kwanini Watanzania wanaogopa kujadili matatizo/changamoto za nchi yao kwa mtazamo wa kuwa watapotezwa?

Robert Heriel Mtibeli

JF-Expert Member
Mar 24, 2018
21,339
51,883
Anaandika, Robert Heriel

Ni lini mtazamo huu utaondoka?
Nani atauondoa?
Mtazamo huu umefanya Watanzania wengi kuwa waoga wa kujadili Kwa Uhuru mambo yanayohusu nchi Yao hasa Kwa kuigusa moja Kwa moja serikali.
Sio wazazi
Sio Wake au watoto wetu,
Sio Wasomi au wasiosoma
Sio Mafukara na Wakwasi, wote wanaogopa kuijadili serikali pale inapokosea au mambo yakiwa hayaendi vizuri.
Nina uzoefu kiasi na Jambo Hilo.

Je ni Kwa sababu Watanzania hawawezi kujadili na kukosoa mambo ya hovyo bila kutukana?
Je ni Kwa sababu historia ya Matukio ya kikatili yaliyotokea nyuma kwa Wale waliojitokeza kujadili na kuichimba Sana serikali?

Je kuzuia na kutia hofu wananchi Wasijadili na kuichimba serikali ndio namna ya kuleta maendeleo ndani ya nchi?

Wakati nipo kwenye makundi Fulani ya whatsApp, ukionyesha kutoikubali serikali katika Jambo fulani, ukaikosoa, utashangaa kuona Washiriki wakipungua na wanabaki wale wanaokutisha,
Wengine inafikia hatua wanakupigia simu kabisa😊😊.
Kwa nini ndani ya nchi watu waishi namna hii?
Naamini wapo wakubwa zangu, wakongwe na wenye akili zaidi yangu watakuja kuniambia ni Kwa nini itumike mbinu hii katika taifa letu. Nipo tayari kusikiliza hoja, Ila sio hoja za kulazimishana,

Au je, taifa letu bado ni changa hivyo kulikabidhi Uhuru wa moja Kwa moja kwa Raia ni hatari?

Au je Taifa letu wajinga ni wengi hivyo kuwaruhusu wafanye watakavyo inaweza hatarisha Usalama wa nchi?

Au je Ili taifa libaki kuwa salama lazima sheria ziwape nguvu watawala kuliko wananchi?

Ajabu ni kuwa ukiwa mtu wa kujadili na kuikosoa serikali na usiposhughulikiwa na serikali sio ajabu ukaitwa Usalama wa taifa/kachero au Askari kanzu. Hivyo watu bado hawatakuwa na Imani na wewe.

Ajabu zaidi, ukiwa unajadili Sana serikali na kuikosoa, watu watasema umetumwa na Mabeberu au Kwa lugha nyingine wewe ni kibaraka.

Nini KIFANYIKE?

1. Wanawake ndio watakaoikomboa nchi hii. Ikiwa watakuwa tayari kuwaruhusu watoto na waume zao kuipigania nchi.
Wanawake Kama watakuwa waoga na wanataka watoto na waume zao waendele kuishi maisha ya dhiki basi maisha yataendelea kuwa vivihivi.

2. Elimu ya Haki ipewe kipaombele na namna ya kuipigania.
Dini na mitaala ifanye hivyo.

3. Wanaume waandaliwe kuwa wanaume watakaoweza kulinda familia na Nchi Yao.

4. Wanaume na wanawake wafundishwe ubaguzi uliokomaa.
Ubaguzi ndio msingi wa maendeleo ya nchi yoyote Ile.
Hii itapunguza gap ya wageni kuwa na Utajiri mkubwa kuliko wenyeji.
Serikali pasipo kuhusika moja Kwa moja iteue watu wenye akili za kutosha kuhakikisha inasimamia Sara za kibaguzi.

5. Sheria Kali ikiwezekana za kifo ziwekwe kwa watumiaji wa mamlaka vibaya, Rushwa na ufisadi.

6. Mtumishi wa umma awe na kazi moja tuu ya utumishi serikalini.
Sio mtu mmoja Mbunge, mtu huyohuyo sijui katibu kitu gani, mtu huyohuyo mwenyekiti sijui wa nini, ili kutoa fursa ya watu wengine Kula Keki ya taifa.

7. Sera ya Uvamizi ifanyiwe kazi mara moja ili Kupunguza kuminyana Kati yetu.

8. Kodi Kwa vijana wanaoanza biashara au kujiajiri wenyewe zipunguzwe kama itashindakana kuondolewa kabisa.

9. Biashara hatari ziratibiwe, na vijana wenye akili na uthubutu waingizwe huko kuhakikisha nchi inakusanya Utajiri WA dunia. Hii ni kutokanatkuwa nchi haina dini.

Nipumzike Sasa.

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Dar ES SALAAM
 
Watanzania wengi kwa sasa wanawaogopa policcm na uvccm wachache waliojivika koti la usalama wa Taifa.
 
Umemsahau yule Mkurugenzi wa shirika la reli alielalamika tozo what's up group akatolewa kazini? Aaah! Naogopa mwenzangu sithubutuuu!

Nawaachia Missionaries waliosoma Cuba
 
Wakitupoteza Mungu naye anawapoteza, mifano ipo hai na tumeyaona, so tusilalamike sana, Mungu wetu anajibu.
 
Back
Top Bottom