Kwanini watanzania wanamlaumu mwalimu Nyerere kwa kukosa elimu?

Haya ndugu kama tumeshakutajia mambo aliyoyafanya ambayo hata viongozi wa sasa wanajikanyaga kuyafanya basi sina mengi zaidi. Labda uniambie kuwa ulikuwa moja wa mabepari wachache walioathirika na maamuzi ya Nyerere. Hivyo hata kama alifanya mabo ya maendeleo kwa watu wa namna yako hawawezi kuyaona kamwe!
 
Alikamata, kwa nguvu, shule za Kanisa na shule za mashirika mengine. Ni pamoja na shule zifuatazo:

(1) St. Mary's College (ambayo baadaye iliitwa Tabora Girls)

(2) Assumpta College (ambayo aliamua kuiita Weru Weru)

(3) St. Francis College (ambayo aliamua kuiita Pugu)

(4) St. Andrew's College (ambayo aliamua kuiita Minaki)

(5) Mariam Collge (Shule ya Wasichana Morogoro)

(6) Umbwe Secondary School

Etc. Ni list ndefu sana]

Lengo lilikuwa ni nini? kuzuia watanzania wasisome au kuhakikisha hata yule maskini wakutupwa anapata elimu? Alizuia shule binafsi lakini aliruhusu shule za jumuia na yote alilenga kuondoa dispality kwa walionacho na wasionacho.
 
Alikamata, kwa nguvu, shule za Kanisa na shule za mashirika mengine. Ni pamoja na shule zifuatazo:

(1) St. Mary's College (ambayo baadaye iliitwa Tabora Girls)

(2) Assumpta College (ambayo aliamua kuiita Weru Weru)

(3) St. Francis College (ambayo aliamua kuiita Pugu)

(4) St. Andrew's College (ambayo aliamua kuiita Minaki)

(5) Mariam Collge (Shule ya Wasichana Morogoro)

(6) Umbwe Secondary School

Etc. Ni list ndefu sana.

Alikamata vile vile shule nyingine binafsi kama Lyamungo Secondary School na Alliance High School.

Mwalimu aliacha Seminari na shule chache za Kanisa (kama Kibosho na Kiraeni).

Mwalimu alikataza watu binafsi kuanzisha shule. Kwa kufanya hivyo, alidumaza sana Elimu ya Tanzania
Kwa sera ya wakati ule ELIMU ilitakiwa itolewe bure.
Hakuna mtu binafsi ambaye angetoa elimu bure,mtu binafsi angeuza elimu kama huduma.

Bado kwa hilo sioni ni kwa jinsi gani alidumaza elimu.Kwangu mimi alibroaden wigo wa upatikanaji wa elimu.Fikiria shule hizo zingekuwa chini ya makanisa au watu binafsi,wewe unajua sasa hivi shule bora ni za seminari na gharama zake wazijua pia.
Swali:
1.Ni watanzania wangapi, miaka 45 baada ya uhuru wanauwezo wa kulipia watoto wao seminari?
2.Je hizo shule kama zingeendela kuwa mikono mwa hao wafanyabiashara tungekuwa na idadi hii tuliyonayo leo ya wasomi? HATA KAMA WAHATOSHI.

Bado naona hoja yako hapo juu haina mshiko.
Nishawishi zaidi ndugu yangu.
 
Hata hiyo amani aliikuta, hakuna historia inayoonyesha kutokuwepo na Amani Tanganyika, kama ni vita zilikuwa na wageni.
Mkubwa nakuheshimu.

Watanganyika tumepigana sana.

JE UNAJUA MAANA YA DHANA NZIMA YA UTANI WA MAKABILA?

Kwa faida yako na wengine wasiolijua hili , makabila yote wanayoitana WATANI hawa walipigana vita za hizo za kale.

Historia ya nchi yetu imegawanyaika katika sehemu kuu tatu:
1.KABLA ya uhuru
2.WAKATI vuguvugu la uhuru
3.BAADA ya Uhuru.

Muda mwingi umetumiwa na wasomi wetu kufanya analysis na presentation kwenye sehemu hizi mbili za mwisho.

Hakuna anayejishughulisha na historia ya tanganyika kabla ya uhuru,ni wachahe mno kama wapo na kazi zao hatuzithamini.

Nakushauri ndugu yangu, chukua hiyo kama changamoto uanze kusoma historia hiyo.utakuwa enlightened sana.

Unajua kuna siku moja, nilikuwa pale UDSM, it was one or two years baada ya Professor BABU kufariki.Kulikuwa na mdahalo pale wakuzungumzia legacy yake.

Unajua nilikutana na mwanafunzi pale, bwana mdogo wangu tukazungumza mawili matatu,nikamweleza nipo pale kwa ajili ya mdahalo ule.

Akaniuliza WHO IS BABU ?

Unaweza kupata jibu, huyo ni msomi wa UDSM ambaye hajui BABU ni nani.

Wapo wengi wa sampuli hiyo.Wapo wengi wasomi wa sasa wasiomjua FIELDMARSHAL OKELLO na wengine.

WAPO WENGI WASIOJUA HISTORIA YA TANGANYIKA KABLA YA UHURU.
 
Alikamata, kwa nguvu, shule za Kanisa na shule za mashirika mengine. Ni pamoja na shule zifuatazo:

(1) St. Mary's College (ambayo baadaye iliitwa Tabora Girls)

(2) Assumpta College (ambayo aliamua kuiita Weru Weru)

(3) St. Francis College (ambayo aliamua kuiita Pugu)

(4) St. Andrew's College (ambayo aliamua kuiita Minaki)

(5) Mariam Collge (Shule ya Wasichana Morogoro)

(6) Umbwe Secondary School

Etc. Ni list ndefu sana.

Alikamata vile vile shule nyingine binafsi kama Lyamungo Secondary School na Alliance High School.

Mwalimu aliacha Seminari na shule chache za Kanisa (kama Kibosho na Kiraeni).

Mwalimu alikataza watu binafsi kuanzisha shule. Kwa kufanya hivyo, alidumaza sana Elimu ya Tanzania

Asante Mwl kwa maelezo yako.......however,

sidhani kama alikataza, ila sera alizokuwa nazo kipindi hicho hazikuwa na mazingira yenye mvuto kwenye uwekezaji katika sekta ya elimu (ukizingatia private school ni Investment and business oriented), mazingira hayakuruhusu watu kuwa na vipato vya ziada, kwa hata ukianzisha shule sana sana ni wachache sana wangeenda hizo shule,

........hata hivyo shule nyingi tu binafsi ziliendelea kuwepo na nyingine kuanzishwa (especially za dini mbali mbali.....za kiislamu, kikristo na kihindu/bohora pia ktk mikoa mbali mbali eg Dar, Tanga Arusha Morogoro, Mwanza, Kagera, Mbeya etc), kwani hawa kupitia mashirika yao ya kidini waliweza kuendesha hizo shule and ofcourse at the same time wakiimarisha imani zao..........

again kusema alidumaza sana elimu ya Tanzania......you may wish to give us some statistics if you don't mind........nakumbuka nia na dhati na juhudu alizokuwa nazo ili kuendeleza elimu kipindi kile Waziri Elinawinga (Sijui kama yuko hai) akiwa Waziri wa Elimu.......
 
Kuna mdau mmoja anasema hata watoto wake Nyerere mwenyewe hawakusoma na hawawezi kuwa hata makatibu kata.
Ni kweli kwani kusoma hakuusiani na Baba yako kwani anayeingia darasani na kusoma ni wewe mtoto na wala sio baba yako na akili ni yako na sio ya baba yako au ya Nyerere.Kama ukishindwa kielimu wa kujilaumu ni wewe mwenyewe kama ukiwa kila siku unaishia kuvuta bangi na kumdanganya baba yako unakwenda shule hilo ni kosa la baba yako au lako.Elimu ni kitu cha jitihada na wala haliusiani kabisa na baba yako na ndio maana hata watoto wa wakulima wamesoma bila hata ya baba zao kuwa wanaelimu.

Elimu ni wewe mwenyewe kujua nini unataka na unataka kuwa nani na hakuna uhusiano wowote na baba yako na ndio maana watoto wengi ambao baba zao wamesoma wao ni magarasa tena joker
 
You can force Donkey to go to the river but you can't force Donkey to drink water on the river.

Same with Education, You can force people to go to School but you can't force those people to study because education and studying required determination and strength
 
uote:
Augustine Moshi

Alikamata, kwa nguvu, shule za Kanisa na shule za mashirika mengine. Ni pamoja na shule zifuatazo:

(1) St. Mary's College (ambayo baadaye iliitwa Tabora Girls)

(2) Assumpta College (ambayo aliamua kuiita Weru Weru)

(3) St. Francis College (ambayo aliamua kuiita Pugu)

(4) St. Andrew's College (ambayo aliamua kuiita Minaki)

(5) Mariam Collge (Shule ya Wasichana Morogoro)

(6) Umbwe Secondary School

Etc. Ni list ndefu sana.

Alikamata vile vile shule nyingine binafsi kama Lyamungo Secondary School na Alliance High School.

Mwalimu aliacha Seminari na shule chache za Kanisa (kama Kibosho na Kiraeni).

Mwalimu alikataza watu binafsi kuanzisha shule. Kwa kufanya hivyo, alidumaza sana Elimu ya Tanzania.


Ndugu yangu wakati tumepata Uhuru hakukuwa na mtu binafsi yoyote ambaye aliweza kuanzisha shule hata kwenye nchi za mabepari hawakuanza na shule za private ni serikali ndio ilikuwa inaanzisha shule na mpaka leo hii kwenye serikali zote za mabepari nyingi zinamilikiwa na seriklai na sio watu binafsi mfano na kwa faida yako Oxford and Cambridge ni shulle za serikali kwani kufanya reseach na development sio kazi mchezo na hakuna mtu binafsi ambaye angeweza kuanzisha elimu ya maana kipindi hicho
 
Uliyeanzisha posti ningependa kuelewa kwanini mpaka leo Tanzania hipo kwenye life support ya kutegemea misaada.

Ukiweza kueleza hayo unatujua kwanini alichemsha.
 
Mwalimu alifanya mambo mengi sana kwa taifa letu hasa katika maeneo ya elimu, tiba, kilimo na uchumi.

Kumbuka kuwa mwalimu alipokabidhiwa madaraka ya kuongoza serikali ya Tanganyika kutoka serikali ya Uingereza alikuta misingi imara na dhabiti iliyokuwepo. Lakini aliaanza kwa kubadili misingi hiyo bila ya kujali athari zake kwa jamii na kamwe alikuwa hashauriki. Kwa maneno mengine ni kuwa mwalimu aliweza kuwafunika Watanzania katika usingizi mzito.

Alikuwa na dhamira ya kujenga na kustawisha taifa imara la Tanzania, na aliaanza kwa kuchukuwa shule zote za makanisa ili watoto wote wapate kuingia madarasani na kupata elimu. Hilo likawa ndilo kosa lake la kwanza.

Kama kiongozi mwenye serikali alitakiwa kujenga shule nyingine zaidi ya zilizokuwepo ili idadi kubwa ya watoto waingie darasani kupata elimu. Ndiyo maana idadi ya nafasi za watoto kuiingia darasani iliendelea kubaki ndogo kwani shule zilibaki zilezile na mipango yote ya kupanua shule na kujenga mpya ilifutika baada ya makanisa kunyang,anywa shule zao.

Mwalimu baadaye alianzisha elimu ya watu wazima, sehemu kubwa ya bajeti ya wizara ikawa ni kusomesha wazee. Wazee wetu wakaelimika kwa kiwango cha asilimia 85 ya watanzania wote. Lakini elimu yao waliyopata haikuwa na tija kwao wenyewe wala kwa uchumi wa taifa.

Baadaye mwalimu akashituka tena, kuwa amewasahau watoto kupata elimu na akawapa baba zao. Hiyo akanzisha mpango (program) ya harakaharaka iliyojulikana kama “Universal Primary Education (UPE)”

Mpango huu wa UPE ndio ulibomoa kabisa ELIMU ya taifa la Tanzania.

Elimu ilikuwa ni ya bure kabisa kwa watoto wote kwa nchi nzima. Idadi ya watoto kwenye shule ilikuwa ni kubwa mno, wakati huo hakuna waalimu hakuna madarasa, hakuna madawati, hakuna ... kila kitu kinachomuweza mtoto akaitwa kuwa ni mwanafunzi wa shule.

Kilichofanyika aliwachukua wanafunzi wote waliomaliza elimu ya msingi ya darasa la saba (7) kisha wakaajiriwa kufundisha bila ya mafunzo yoyote ya kueleweka. Matokeo yake na adhari zake hata sasa bado zipo. Mtoto anamaliza darasa la saba hajui kuandika jina lake.

Mwalimu baadaye akaja tena na azimio lingine la ajabu ajabu kabisa, hili liliitwa AZIOMIO LA MUSOMA. Azimio hili shabaha yake ilikuwa ni kusaidia jamii ya kike kupata nafasi za kusoma vyuo vikuu kwa idadi kubwa zaidi kuliko jamii ya kiume. Azimio hilo liliwalazimisha vijana wa kiume kufanya kazi miaka miwili kwanza wanapomaliza darasa la kumi na nne, ndipo waombe kujiunga na elimu ya juu.

Kipindi hicho ndicho taifa lilikuwa halina kitu chochote madukani kuanzia dawa ya meno hadi sabuni. Biashara ya kuvuka mipaka na kuigiza kanga, sabuni, mafuta, nk ikawa ndiyo ajira iliyokuwa nyepesi kwa vijana hawa walionyimwa haki yao ya elimu. Kipindi cha miaka miwili hawa vijana wakawa wanafanya biashara nzuri sana mipakani wakijulikana kama walanguzi. Suala la kurejea vyuoni likawa halipo kwao tena.

Mwalimu baadaye akaja na elimu ya mgao. Kila mkoa ulipewa alama za kufaulu anazotakiwa apate mwanafunzi ili achanguliwe kuingia kidato cha kwanza. Mfano Mkoa wa Arusha ili mtoto achanguliwe kiingia kidato cha kwanza ni lazima apate alama 60, Mtwara 45, Mwanza 50 Tanga 70, Kilimanjaro 80 mgao ambao sasa serikali imeufutilia mbali.

Nilianza kusema misingi ya elimu, uchumi, tiba n.k ilibomolewa, ndiyo maana awamu hii ya sasa imekuja na shule za sekondari zinazojulikana kama shule za kaya ambazo hazina tofauti na mpango mbovu wa elimu wa UPE.

Watanzania bado tuna matumaini kuwa Mwenyenzi Mungu atatusimamishia kiongozi wa kurudisha misingi ya Taifa iliyobomolewa.
 
Uliyeanzisha posti ningependa kuelewa kwanini mpaka leo Tanzania hipo kwenye life support ya kutegemea misaada. Ukiweza kueleza hayo unatujua kwanini alichemsha.

Ingawa sijaianzisha post hii, lakini naweza kukujibu yafuatayo. Tunaendelea kutegemea misaada kwa sababu viongozi waliopo madarakani wanapenda mteremko toka wakati wa Mwinyi mpaka Kikwete. Mpaka sasa hawajui mihimiri ya uchumi wa nchi yetu ni ipi na katika hiyo hawajui wanaweza kupata sh. ngapi wakiamua kusimamia kwa ufanisi. Na kama wanajuwa basi hawataki kujibidiisha kuhakikisha inaboreshwa na kama watataka iboreshwe basi maslahi yao yanatangulizwa mbele hivyo miradi husika kutokuwa na tija. Mifano ni mingi Madini, bandari, reli, kilimo, nishati hakuna hata kimoja ambacho watanzania tunaweza kujivunia kuwa kinafanya kazi na kuleta tija kwa nchi. ukija suala la ukusanyaji kodi na matumizi yake ndio usisiseme. Kidogo ni huduma za kibenk ndio angalau zinapaform lakini nazo nyingi ni zakutoka nje na watu wa nje wanazimiliki kwa asilimia 100 hivyo pesa inayobaki nchini kuwa kiduchu. Utalii nao unasuasua watu waanashinda Ulaya kutangaza utalii kila kukicha. Mapato na matumizi haviendani hata kidogo. Ndugu si umeisikia Ethiopia? pamoja na matatizo yote yaliyowakumba, toka ameingia Zenawi Madarakani hataki mchezo. Benk zote nchini humo either zinamilikiwa na wa Ethiopia au kwa ubia kati ya wageni. Lakini katika Ubia, sheria yao ya uwekezaji inawataka wageni kumiliki 51% tu, na 49% ya hisa lazima zitokane na wazawa. Uchumi wao unakua kwa asilimia 8 mpaka 10. Miongoni mwa maamuzi mazito waliyoyafanya, wanajenga bwawa la kuzalisha umeme wa nguvu za maji kwa thamani ya dola za kimareka million 800 (Source; Alexander's Gas & Oil Connections - Ethiopia to build country’s largest ever dam) na miradi mingine mingi ya umeme wa nguvu za maji inaendelea. Sisi huku tumeacha maji yakipotelea indian ocean huku tukilipa more than sh. billion mia mbili na nusu kwa ajili ya capacity charges ya magenereta na hapo bado hatujanunua umeme wenyewe. Tunasingizia ukame kila kukicha. Ndugu upo hapo, nakwambia sisi bado hatujawekeza ila 'tunadimba'

Hivyo ndugu misaada tunayohangaikia kuomba ni yakujitakia na kutushushia utu wetu watanzania.
 
Mwalimu alifanya mambo mengi sana kwa taifa letu hasa katika maeneo ya elimu, tiba, kilimo na uchumi.
Mwalimu baadaye alianzisha elimu ya watu wazima, sehemu kubwa ya bajeti ya wizara ikawa ni kusomesha wazee. Wazee wetu wakaelimika kwa kiwango cha asilimia 85 ya watanzania wote. Lakini elimu yao waliyopata haikuwa na tija kwao wenyewe wala kwa uchumi wa taifa.

Baadaye mwalimu akashituka tena, kuwa amewasahau watoto kupata elimu na akawapa baba zao. Hiyo akanzisha mpango (program) ya harakaharaka iliyojulikana kama “Universal Primary Education (UPE)”

Ndugu ungetutajia miaka ya matukio yalivyokua yanatokea ungetusaidia sana otherwise utakuwa unatuingiza chaka. Kwa kumbukumbu zangu UPE ilianza towards the mid of 1970s na elimu ya watu wazima ikafuatia. Shule nyingi sana za msingi zilijengwa kwa nguvu za wanachi wakishirikiana na selikari, during 1970s hivyo si kweli kuwa pamoja na kunyang'anya za watu binafsi na taasisi hakufanya jitihada za kujenga nyingine. Wabunge wa maeneo husika au viongozi wa ndio walikuwa wamezembea kuwahamasisha wananch kujenga shule. ni katika kipindi cha mwalimu, Mkoa wa kilimanjaro na Iringa zilihamasika kujenga shule kibao za sekondari za wazazi na selikari. Pia mniambie shule za sekondari za Ruvu, Tarime, Kibiti, Kilosa, Ifakara n.k ambazo zote ni za selikari zilijengwa kwa jitihada za nani? Kwa sehemu kubwa uzembe wa watendaji ndio umechangia elimu kuwa nchini. Mambo ya kuanzisha shule yalikuwa katika uwezo wa halimashauri husika walichokuwa wanakifanya ni kuvuruga utaratibu mzuri ambao mwalimu aliouweka. Mfano halmashauri yangu ya Mbozi pamoja na kukusanya mamillioni ya mapato toka kwenye kila kilo ya Kahawa kwa ajili ya maendeleo ya elimu, halimashauri haikuwa na shule hata moja ya selikari hadi kufikia mwaka 1987. Haya tukaanzisha shule ya sekondari kwa kuchukua majengo ya shule ya msingi ya Vwawa mwaka 1988, nayo kuiboresha tu ilikuwa patashika. Tulibaki na hiyo shule miaka yote mpaka mpango wa shule za kata ulipoanza miaka ya 2000 ndipo shule zikaanza kuongezeka. Hivyo ndugu watendaji wazembe mpaka leo ndio tatizo la mambo yetu kielimu kutokwenda vizuri!
 
It is too long to read! I do agree with him " it is time for action now and quit bitching. Most people are lazy and like to justfy their behaviour for blaming others. I am away from those people and I have zero terelance with thier stupidity
 
Nakushukuru Majimoto kwa mchango dume. Nitanukuu baadhi ya uliyoandka:
Mwalimu alipokabidhiwa madaraka ya kuongoza serikali ya Tanganyika kutoka serikali ya Uingereza alikuta misingi imara na dhabiti iliyokuwepo. Lakini aliaanza kwa kubadili misingi hiyo bila ya kujali athari zake kwa jamii na kamwe alikuwa hashauriki
He was a social scientist who converted an entire country into his experimental lab. It was not a very original experiment though. He copied whatever was happening in China.

Kama kiongozi mwenye serikali alitakiwa kujenga shule nyingine zaidi ya zilizokuwepo ili idadi kubwa ya watoto waingie darasani kupata elimu.
Sijui ni kwa nini hakumwiga Jomo Kenyatta badala ya kuwaiga Mao Tse Tung na Kim Il Sung. Wakati Mwalimu akilazimisha Maaskofu wamkabidhi shule zao za sekondari, Kenyatta alikuwa anazunguka Kenya nzima akihimiza ujenzi wa shule za HARAMBEE!

Mwalimu baadaye alianzisha elimu ya watu wazima, sehemu kubwa ya bajeti ya wizara ikawa ni kusomesha wazee. Wazee wetu wakaelimika kwa kiwango cha asilimia 85 ya watanzania wote. Lakini elimu yao waliyopata haikuwa na tija kwao wenyewe wala kwa uchumi wa taifa

Mpango wa Mwalimu wa Elimu ya Watu Wazima ulikuwa ni nguvu ya soda. Ndio maana uliachwa na kila mtu, ikiwa ni pamoja na Mwalimu, miaka michache baadaye. Mwalimu alipenda sana kuongoza kwa CAMPAIGN.

Mwalimu baadaye akaja tena na azimio lingine la ajabu ajabu kabisa, hili liliitwa AZIOMIO LA MUSOMA

Hapa aliiga mojawapo ya hatua za Cultural Revolution ya China. Mwalimu alidhani ni lazima uwe mzee kwanza, au uwe umefanya kazi, ndio uweze kusoma Chuo Kikuu. That was a very mediocre idea. Equally mediocre was his view that primary education was adequate to prepare youth for life.

Waziri wa Kwanza wa Elimu, Solomon Eliufoo, alikuwa independent thinker. Waliomfuata wakawa mabwana ndio Mzee tu. Kati yao, aliyechangia kuvuruga Elimu kuliko wote ni Chediel Mgonja.
 
Mwalimu Augustine Moshi,
Mkuu wewe utamlaumu mwalimu kwa sababu ya imani yako ya dini.. Ni sawa na Kaburu tu kwangu maanake sisi waislaam kabla ya shule hizi hazijachukuliwa tulilazimishwa kubadilisha dini, wengine tulibadili majina tu ili tupate elimu ya Msingi..Na mimi ni ushahidi tosha wa madai nayoyaweka..
Na kama unabisha nakuomba nambie jina la Muislaam hata mmoja aliyekuwa akisoma shule hizo bila kutengwa kutokana na dini yake sasa hawa walikuwa na tofauti gani na Kaburu!

Tena kibaya zaidi ni kwamba leo hii baadhi ya shule za dini zimerudia mfumo ule ule wa kutenga watu kwa dini zao..Leo hii kuna shule za Makanisa na za kiislaam zinawatenga watoto na walimu kutokana na dini zao (imani ya dini)..Sii ujinga mkubwa huu wa mwafrika yaani dini imekuwa ndio tegemeo la elimu ya mwananchi?

Kwa hiyo namba ya shule na wanafunzi inaweza kuonekana kubwa sana lakini ukweli ni kwamba elimu inayotolewa leo ni mbovu kuliko wakati wowote ule..Wee tembelea hivyo vyuo na University ndipo utafahamu kwamba wingi wa shule zetu (Quantity), hauna maana yoyote kwa mwenye kuelewa maana..
Inashangaza sana kuona watu humu mnasifia hali ya Elimu leo hii Tanzania kuliko wakati wa Mwalimu...watu wanaua Albino wakitafuta Utajiri, Waganga wa Kienyeji wana hesabu kubwa ya wagonjwa kuliko Hospital.. hizi ni alama kubwa za UJINGA!... Yaani ni vichekesho vitupu!

Mimi nitamshukuru Mwalimu hadi siku nakufa kwani kama sio yeye sijui ningeipata vipi elimu nikiwa kijijini huko Mwibara!
Na namshukuru Mungu kuona kuwa karibu asilimia 80 ya waandishi wazuri humu JF ni matunda ya wanafunzi wa mfumo wa Mwalimu hadi Mwinyi..
 
Bwana Mkandara,
Umesema Waislam walilazimishwa kubadili dini; are you sure? Mie kuna ndugu zangu zaidi ya watatu ambao ni Waislam na wanamajina ya ki-islam walisoma vizuri sana na kumaliza shule hizo hizo.
Infact suala la elimu kwa nyerere on nationalization lilikuwa political (control); centralisation and governance. Kama alivyosema mwalimu hapo juu, kichwani kwa mwalimu pamoja na kuwa na charisma; vile vile ule ujamaa wa ki-China uimwingia mno. He just wanted everything in a central government for him to exercise control. Je kama angetoa amri kwa hizo Shule zisomeshe watoto wote waislam na wakristo nani angekataa? It was more political.

Hebu mwenzetu tuambie, kulikuwa na sababu gani, niliona baadhi ya mikoa shule za msingi hadi zile shati za kuvaa shule ziliondolewa "collar" wanafunzi wakawa wanavaa kama wachina. Eti shati inaitwa choen-lai.

Achilie mbali hayo yote, you 're right in one issue; wengi wetu tumshukuru huyu mzee kwa elimu hii, wazazi wengi hawakujua nini maana ya elimu.

Lakini tena uneni-acha hapa "matunda ya wanafunzi wa mfumo wa Mwalimu hadi Mwinyi". Hivi kuna zuri alilofanya Mwinyi? To me all what he did (Mwinyi) was detrimental to our unity, and good governance; the national was in total paralysis; economically, socially and politically!! All the time I pray not to have a president like that (like Mwinyi)!
 
Intersted Observer,
Bwana Mkandara,
Umesema Waislam walilazimishwa kubadili dini; are you sure? Mie kuna ndugu zangu zaidi ya watatu ambao ni Waislam na wanamajina ya ki-islam walisoma vizuri sana na kumaliza shule hizo hizo.
Mkuu nasema hivi kila Muislaam aliyesoma shule za Misheni aidha alibadilisha jina (nikiwa mmoja wao) au alibadilisha dini..Hii nazungumzia kabla ya mwaka 1967 waulize wazee wote waliosoma miaka ya 50 hadi 60 kuhusiana na ubaguzi elimu nchini..kuna mbinu tofauti zilitumiwa na Waislaam kusajili watoto wao, hivyo ni lazima uwe mmoja kati ya wazazi hao upate kuelewa.

Mkuu wangu, hizi habari za China zinakuja tu kwa sababu tulifuata siasa ya Kijamaa, leo hii Chevez anayafanya hayo hayo kabla ya hata ushurika wa China na Urusi ambao wote leo hii sio Wajamaa tena ni Mabepari..
Tatizo la sisi binadamu ni pale tunapotaka kutafsiri kila kitu kwa siasa... leo hii Obama anapo Bail out mashirika na kutangaza regulation wanasema ni Ujamaa wakati swala sii lazima iwe Ujamaa kuelewa kwamba regulations zinatakiwa kuwepo iwe ktk mfumo wowote ule wa Kisiasa...Nyerere kabla hata ya Ujamaa alitaifisha baadhi ya Hotel Dar -es Slaam kwa sababu walikataa kuwahudumia watu weusi tena nakumbuka kisa cha Meya wa kwanza Dar es Salaam..
Kashogi alipokwenda Kenya miaka ya 70, alinyimwa chumba hotel moja ya Kenya, kesho yake aliinunua Hotel nzima na kuwafukuza wafanyakazi waliomnyima chumba..Kitendo hiki hakimfanyi Kashogi kuwa Mjamaa binafsi!..

Kwa hiyo maamuzi haya hayana siasa isipokuwa ni kutazama haki. Trust me, hata kama mimi ningekuwa Bepari kiasi gani siwezi kukubali shule za Kikristu au za Kiislaam zisajili watu wenye imani zao tu wakati wanapotoa Elimu Dunia..Mkuu wangu wewe hukupitia haya na kwa bahati mbaya unasikiliza simulizi za watu ambao sifahamu wamesoma shule zipi..Na unaposema wamesoma vizuri tu ktk shuloe hizo hizo hufahamu mbinu zipi wazazi wao walitumia kuwasajili watoto hao..Acha wakati ule wa Mkoloni wewe unafahamu kwamba hata leo hii wapo watoto wanaobadilisha dini ili wapate ELIMU nzuri - Tanzania?.. Unajua kwamba wapo watoto wanaobadilisha dini ili wapate huduma za NGO's zilizoingia nchini kusaidia watoto Yatima na wale wa familia zisizojiweza..
Unajua kwamba kuna watu waliokufa, wameshindwa kuzikwa na ndugu zao kwa sababu tu wamebadilisha dini?...Huu upuuzi wa Elimu ya dini kutawala Elimu dunia na utu wetu unatoka wapi kama sio makombo ya fikra duni za kupandikizwa..Hivi kweli mnaona maisha ya leo yana unafuu wowote ktk jumuiya zetu wakati Watanzania tumepoteza kabisa values zetu leo hii tunaona Uzungu na Uarabu kuwa ndio deal..kiasi kwamba hata watoto wetu tunawakanya urafiki au ushirikiano na mtoto mwenye imani tofauti..
Mkuu wangu Tanzania inakoelekea ni Kubaya zaidi na sijui kama wewe umewahi kufikiria tanzania ya kesho itakuwa na picha gani..Sasa kama Nyerere alikuwa ameambukizwa na Wachina sijui mfumo huu mtasema tunaambukizwa na Utawala gani?..

Ohh by the way nimesema mfumo alioacha mwalimu hadi Mwinyi, nikiwa na maana mfumo wa ELIMU sio Mwinyi alichokifanya au utekelezaji wa utawala wa Mwinyi..
Hata leo hii ndani ya mfumo huu anaweza kuja kiongozi akaongoza vizuri, lakini haina maana mfumo mzima ni mzuri.. sikubaliani na Dini kuwa chanzo cha elimu dunia ya mwananchi..
 
Moshi,Interested Observer,

..namlaumu Mwalimu kwa kukifanya Kiswahili lugha ya kufundishia shule za msingi.

..matokeo ya uamuzi huo ni kushuka kwa kiwango cha ujuzi wa Kiingereza, na vilevile kushuka kwa kiwango cha elimu ya sekondari.

..Kiswahili tayari kilikuwa kinazungumzwa na sehemu kubwa ya Watanzania/Watanganyika kabla Mwalimu hajaingia madarakani.

..wakati wa harakati za uhuru ni Mwalimu alilazimika kuzungumza kwa kutumia mkalimani ktk mikutano aliyofanya Mwanza na Mbulu. maeneo mengine yote alizungumza Kiswahili na alieleweka.

Mkandara,

..Mwalimu hakupaswa kutaifisha shule za taasisi za Kidini. alichopaswa kufanya ni kuongeza kasi ktk kujenga shule za serikali.

..Mwalimu alitaifisha mpaka mashule yaliyokuwa yanamilikiwa na vyama vya ushirika. shule ya Lyamungo ilikuwa mali ya KNCU. sidhani kama zoezi la kutaifisha shule za taasisi za kidini lengo lake lilikuwa ni kuondoa ubaguzi wa kidini.

..tatizo ni kwamba kila alichotaifisha Mwalimu aliishia kushindwa kukiendesha. shule,hospitali,mashamba makubwa,majumba, etc etc.
 
Jokakuu,
Mkuu wangu samahani sana lakini maelezo yako ni Upofu wa kutoelewa maana ya hoja yangu.. Unaposema kosa la mwalimu ni Kutaifisha hizo shule una maana gani?..Shule ya msingi niliyosoma mimi hata baada ya kuitafifishwa walimu wake walikuwa wale wale Watanzania wazawa na wazungu masista wawili ambao waliondoka baadaye mwaka 1968. Hivyo tufauti kubwa iliyokuwepo ni walimu wawili..
Pili, Kwa mfano wako wa kutazama makosa unaelekea unatafuta mchawi.. Ni sawa na kusema ilikuwa kosa kubwa kwa South Afrika kuondoa Apartheid kwa sababu ya Ujambazi unaotokea leo au Ni makosa kwa South Kupata Uhuru kwa sababu hali ya uchumi wa nchi hiyo leo umedhoofika.. Mkuu hapa kama kuna mtu wa kumlaumu ni rais aliyepo madarakani ambaye kashindwa kuiendeleza nchi hiyo kiuchumi na sio swala jingine..
Yes, nakubali kabisa kuwa Mwalimu alikuwa na makosa mengi sana lakini sio ktk hili hata kidogo.. Ukisoma mawazo ya Kina Moshi utaona kwamba hoja zao zina base ktk Ukristu.. Mifano ya Jomo Kinyatta wameshindwa kutazama upande wa pili ambao waislaam wa Kenya kwa silimia yao ndogo huwezi kupata hesabu nzuri ya wasomi.. Ni chini ya asilimia 2 ya Waislaam wa Kenya wamesoma yaani kati ya kila Waislaam 100, wawili waliweza kupata Elimu, lakini kama utatazama Kenya nzima ambayo ina zaidi ya asilimi 70 wakristu utasema wamesoma sana kuliko Tanzania.. yes Wamesoma sana na hesabu hiyo hiyo unaweza kuipeleka Saudia au Iraq ukasema wairaq wamesoma sana hali ni sehemu ndogo sana ya Wakristu wamehusishwa ktk mjadala mzima...Palepale tunarudi - KIla Taifa tunatazama WATU na MAZINGIRA..

Kisha swala la Kiswahili kuwa lugha ya kufundishia sijui unachotaka kusema hapa.. Leo hii shule zote za private zinatumia Kiingereza na hesabu ya Failure imekuwa kubwa sana..wakati miaka yetu ya mwalimu hesabu ya walioshindwa ilikuwa ndogo sana isipokuwa wengi walikosa nafasi ya kuendelea mbele kutokana na uchache wa shule za sekondari. Hivyo tatizo sio kuchukuliwa kwa shule zile isipokuwa ni uwezo wetu mdogo ktk ujenzi wa shule zile. Kumbuka mikopo yuote tuliyoipata wakati ule ktk ujenzi wa Taifa ilikuwa na masharti magumu sana ambayo hayakutupa nafasi ya kuchagua wapi tunaweza kuwekesha..
Licha ya yote haya sio kwamba najaribu kumsafisha Nyerere hata kidogo.. Alishindwa kuendeleza ELIMU kwa wingi wa shule na sio Ujenzi wa Elimu bora kwa wanafunzi wake..Viongozi wote unaowaona leo hii ktk mashirika na serikali ni wanafunzi wa mwalimu na nakuhakikishia kwamba vijana wa leo hawawezi kusimama nao sambamba iwe ktk Elimu dunia au fikra tu. Hadi leo Madaktari wazuri Tanzania ni wale waloisoma wakati wa Mwalimu, leo hii mafunzo yanafanywa kwa kutumia PC kweli utaweza kufanya upasuaji?..

Nooo wakuu wangu, nachozungumzia mimi ni chances za mwanafunzi kupata Elimu.. wakati wa mwalimu kulikuwa na nafasi kubwa ya mtu yeyote kupata elimu kwa uchache wa shule zetu lakini leo hii pamoja na kuwepo shule kibao (magugu) mkafikiria wingi wa shule ndio maendeleo basi bila shaka tutakuja vuna magugu..Yanapandwa magugu zaidi ya mbegu zinazohitajika ktk elimu dunia na ndio maana Udini na imani za kichawi zinastawi nchini..

Nitarudia kusema hivi Kiingereza ni LUGHA sio elimu hivyo ni Ujinga mkubwa kumfundisha mtu kwa lugha asiyoifahamu..Kiingereza kinafundishwa kama somo yaani LUGHA ambayo faida yake ni sawa kabisa na faida ya masomo mengine kama vile Hesabu..Ni makosa ya kila shule kutokuweka vipindi vingi vya lugha ya Kiingereza kwani zipo shule ambazo zilifanya hivyo..Ni muhimu sana wanafunzi wetu wafuyndishe kiingereza kutokana na kwamba ndiyo lugha inayotumika zaidi tunapofanya mikataba na mazungumzo nje ya nchi yetu.... LUGHA!
Ni rahisi sana kumfundisha mtoto wa Kitanzania kuwa - Mbili kujumlisha na Mbili ni sawasawa na NNE, na akaelewa (kuelimika) kuliko hiyo Two plus Two equals to Four kwa sababu kwanza atatakiwa kujua hiyo Two ina maana gani, plus ina maana gani na hiyo equals.. hivyo fundisho la Lugha ya Kiingereza linatangulia kwanza kabla ya kuifanya Lugha ya nje kutumika..Kama wewe mzazi ungemfundisha mtoto wako kiingereza toka azaliwe sidhani kama Mwalimu angebadilisha mfumo wa Lugha ya kufundishia...
 
Mkandara,
Nawashangaa kabisa wale wanaosema Mwalimu angemuiga Kenyatta kuliko Wachina.
Kenyatta was a tribalist. Full stop. Hata hizo shule za Harambee alifanya kwenye maeneo ya Wakikuyu. Na hata kama Mwalimu angefanya harambee tatizo la Tanzania wakati wa kuondoka mkoloni ni kwamba hatukuwa na waalimu wa kutosha kuzijaza hizo shule ambazo zingejengwa kwa harambee. Pia kama Mtanzania najivunia Kiswahili changu na Kiingereza nakitafuna sawasawa. Otherwise mkuu tupo pamoja.
 
Back
Top Bottom