Kwanini watanzania wanamlaumu mwalimu Nyerere kwa kukosa elimu?

weka MAJINA ya seminari za kiislamu ambazo nyerere ametaifisha na sio za kihindu

za kikristu ambazo nyerere ametaifisha pugu, minaki, old moshi, mkwawa, ihungo, tabora boys and more....

Huoni kuwa hiyo ilikuwa danganya toto? jee, unayosababu yeyote ya kwanini seminari za kikiristo zingine ''ataifishe'' na zingine la? na za dini zingine zoooooooooote ataifishe?
 
yeye alisoma lakini hakujua kuitumia elimu yake alikuwa anamaanisha nini mtu akikutwa na TV anaambiwa hujumu uchumi that is non sense kabia inamaanisha alikuwa hataki maendeleo ya wananchi wake ndio mpaka sasa wafuasi wake [
 
dar-es salaam,
Mkuu wangu napenda sana mijadala na tena naweza kubisha vizuri sana kwa hoja ambazo sii porojo kama unavyofikiria kwa sababu ni wewe unayesoma hadithi na vitabu vya watu wakati mimi nimeishi ktk mazingira hayo..
Kwanza unapozungumzia swala la kutaifisha, sii kweli kwamba Nyerere alitaifisha baadhi ya shule za Kikristu na akataifisha zote za madhehebu mengine.. Sii kweli nakumbuka Mwanza tulikuwa na shule ya Lake Primary na Sekondary, Dar kuna Shaban Robert, Mzizima na kadhalika..Sasa hii habari yako unaitoa wapi..
Zaidi ya yote hayo ni shule gani ya Kiislaam ambayo ingeweza kusajili Wakristu? nambie hata moja wakati na Kabla ya Nyerere kama sio shule hizi ziliendelea kujenga tabaka la Watanzania kwa kufuata imani za dini..
Mkuu kwanza ni muhimu utambue kwamba Elimu dunia sii elimu ya dini wala kabila kuelimika..WHY unaingiza dini ktk elimu hiyo!.. Na kama mwilimu asingechukua hizo shule mbili sijui tatu szisizojaa mkononi, waislaam wangapi wangeweza kupata elimu hata ya darasa la saba!..Mimi sina hakika labda leo ningekuwa muumini wa dini nyingineyo kwa sababu ya shida..
Mkuu tunashindwa hata kujisadia sisi wenyewe na baraza lenu la Bakwata.. Mmepewa jengo zima na kiwanja kikubwa leo tembelea pale ofisi Utafikiri umetoka MnaziMmoja uko Tandale kule Uwanja wa fisi.. Hii yote bado unamlaumu Nyerere!..
Acheni uchuro jamani acheni, msalie mtume....Mungu hapendi Unafiki..
 
Zakumi,
Babuu nakusikia sana isipokuwa hili neno sustainable unalitumia vibaya sana ktk swala hili la Elimu.. kifupi hata sikupati zaidi ya kusema kwamba nimekusoma sana huko nyuma na mara zote nimeona unapotea vibaya.. Pengine ni kwa sababu ya chuki binafsi au huelewi kili/na-chotokea..
Kushindwa kwa Ujamaa kama mfumo wa Siasa haina maana Ujamaa ulikwisha..bali Ujamaa ulifanyiwa marekebisho mengi sana yanayoambatana na mazingira ya kiuchumi duniani, kiasi kwamba wachumi na wanasiasa wakaanza kusema huo tena sio Ujamaa..

Mabepari hawawezi kuufahamu Ujamaa kuliko wajamaa wenyewe. China hadi kesho wanasema wao ni Wajamaa kwa sababu sii swala la serikali ku control uchumi ndilo linaufanya Ujamaa kuwa Ujamaa, ni kipengele ambacho kilihitaji marekebisho kwani wamekuja gundua kwamba serikali haiwezi kufanya wala ku control biashara, ni wajibu wa serikali kujenga policies na mazingira ambayo biashara inaweza kushamiri bila kupotosha ama kulaghai wananchi wake...

Ni sawa na Ubepari, sio swala la serikali kutoingilia maswala ya Uchumi ndiko kunakoufanya Ubepari uwe Ubepari..wala sio kweli kwamba uchumi hujiendesha wenyewe kwa kufuata soko la mahitaji na usambazaji kwa sababu uchumi haujiendeshi wenyewe bali huendeshwa na watu, watu wenye kila aina ya tabia na tamaa..
Na ndio maana kuna crimes..haijatokea hata siku moja watu wote tukaamini dini na mwoingozo wa dini zetu tukasahau kuweka sheria za serikali kupambana na wahalifu pamoja na kwamba misahafu inatufundisha mwengi mazuri ya yenye upendo.. Adhabu na regulation zipo kila sehemu na dini haiwezi kupotosha Udini wake kwa sababu kuna masharti ya kufanya ibada...Na ndio amana kuna watu wanaoshindwa kuelewa kwa nini dini zinakuwa na masharti ikiwa dini ni imani ya mtu..

Hivyo basi, ndio maana leo wanakubali kuweka regulations ktk chumi za nchi za Kibepari, regulations ambazo ktk misahafu ya Ubepari kulingana na mrengo wa Conservative unapingana..Leo hii serikali zote za nchi za Ulaya zinatoa madharti hadi kuingilia ajira za CEO ktk mashirika yalnayofanya vibaya..

Kati ya yote haya ni somo zito kwetu sote kuelewa kwamba Uchumi ni somo lakini ktk utendaji wake ni sawa na kamari hakuna mtu hata mmoja anayefahamu mzungu kalala wapi..Ujamaa ulishindwa na tukarekebisha sehemu ambazop zilikuwa na hitilafu hivyo hivyo Ubepari unarekebishwa sehemu ambazo zina hitilafu, kitu ambacho hakikubaliki pande zote..
Mwalimu alikuwa na makosa yake na hasa ktk Uchumi mipango yote ni sawa na utabiri wa hali ya hewa.. Kinachotokea leo hii ni sawa na ile Tsunami ambayo pamoja na kwamba walitegemea kuwepo na machufuko hayo lakini hawakufahamu ukubwa wa gharika lile.
Kama unakumbuka GT aliwahiu kuniuliza kuhusiana na hali ya Uchumi nchini Marekani kama wataweza kutoka kirahisi..Nilimjibu nini?..
Nilisema sio swala dogo kabisa kama vile watu wanavyofikiria na litatingisha nchi za magharibi..Mwisho nilisema solution itakuja patikana lakini watajifunza mengi machafu ambayo huambatana na Ubepari..Leo hii tupo katikati ya mtingisho mkubwa wa mfumo mzima wa Kibepari na marekebisho yanafanyika..
Now, what is sustainable ktk kumtazama mwalimu.. Ni kile alichoweza kujenga ktk jamii yetu. Kweli hatuna elimu nzuri kuliko nchi nyinginezo duniani lakini sii swala la Nyerere tena...
Nyerere alijenga dams kwa ajili ya Umeme, leo hii ni utaalam ulipitwa na wakati na bado hautoshelezi..Huwezi kusema sii sustainable kwa sababu tu Tanzania nzima bado asilimia 14 ndio wenye Umeme wakati dams hizo hazijawahi kutumika ipaswavyo, na leo hii zinafanya kazi kwa asilimia 50 chini ya kiwango chake,kisha sisi tumeshindwa kuziendeleza kwa njia yoyote ile.. Wee tazama Uwanja wa ndege JKN, toka Nyerere aujenge tumeongeza kitu gani zaidi ya kujenga bustani na kuupa jina jipya!..
Mwinyi, Mkapa wamejenga policies zipi ambazo ni sustainable!..Mkuu dunia ya leo hakuna policy wala sera ambayo ni sustainable kwani policies siku hizi hazijengwi kutokana na matumizi ya vitu hivyo isipokuwa upatikanaji wake..
Marekani ilikuwa haramu kununua vitu toka China leo hii ndivyo vimejaa madukani na wao wameshindwa kabisa kusema - BUY AMERICANS kwa sababu lugha ile ya Reagan haiwezi tena kufanya kazi ktk mazingira ya leo - Utandawazi..sasa kwa sababu tumefuata Utandawazi did Reagan failed au sera zake za kununua mali ya Marekani zilishindwa au zilikuwa sii sustainable wakati ziliwaondoa Marekani toka ktk Depression ya mwaka 1982!....Sidhani!
 
Huoni kuwa hiyo ilikuwa danganya toto? jee, unayosababu yeyote ya kwanini seminari za kikiristo zingine ''ataifishe'' na zingine la? na za dini zingine zoooooooooote ataifishe?
Sababu ni kuwa shule za madhehebu zilikuwa za namna

Moja kuna shule zilizokuwa zinaandaa watu kuwa mapadri au wachungaji. Hizi Nyerere hakuzigusa hata kidogo aliziacha. Mfano ni Maua Seminary,

Aina nyingine za shule za makanisa ni zile zilizokuwa business oriented lakini bado zilibagua watu kulingana na madhehebu yao. Hizi Nyerere hakuzibakisha hata moja zikiwemo Rungwe Secondary, Pugu e.t.c

Tatu kulikuwa na shule za madhehebu na za jumuia ambazo zilikuwa zinapokea watu kutoka madhehebu tofauti na ada ilikuwa ya chini hizi hazikutaifishwa bali ziliendelea kupokea msaada kutoka selikarini kwa ajili ya kujiendesha
 
Back
Top Bottom