Kwanini watanzania wana matusi sana?

my name is my name

JF-Expert Member
Jan 12, 2015
2,017
2,384
Watanzania wana matusi sana. Unaweza ukakuta post ina comments 500 basi comments 450 zote ni matusi. Tofauti na post ambazo sio za watanzania katika hizo comments 500 unakuta 10 au 20 ndio wametukana wengine wana comment kutokana na post au wana joke lakini sio matusi ya nguoni.kuja kwa watanzania sasa wewe utawapenda unakuta mtu ameandika tusi mpaka wewe msomaji unastuka halafu unajiuliza kama mimi msomaji nimestuka hivi huyu muandishi itakuwa vipi? halafu una conclude Hapana hii comment lazima itakuwa imejipost wenyewe hakuna mtu anaweza kupost hivi. Baadae unakumbuka hamna haiwezi kuji post wenyewe lazima kuna alie post, mwisho wa siku unabaki njia panda imejipost au imepostiwa? Wana matusi kama wamesomea vile mengine hata mtu hujawai kuyasikia.sijui ni nini nyie watanzania Hebu pu nguzeni matusi ndio maana mna dharaulika mna akili za kutambua majina yenu tu na sehemu mnaishi lakini hamna akili kwenye mambo ya ulazima. Mbadilike
 
Mwenyekiti alianzisha kampeni ya kushikisha "UKUTA" vijana wake, sijui alishikisha wangapi. Daah
 
Watanzania Wana matusi nimeprove Ila ni watu waoga zaidi Duniani . Nyerere aliwai kusema kama ametengeneza kizazi cha watu waoga Mungu amsamehe. Watanzania ni watu waoga Sana ila kutukana wanaweza.
 
Mitusi ipo insta huko hapa tunatukanana kisomi, imeletwa hoja, unajibu kiungwana unajibiwa mitusi ya ajabu.
Sasa na wewe kwenye beleshi huweki kipawa,unaleta kabisa vile vidampa kumwaga uchafu.spedo call it a speedo muende sawa.
 
Umeandika kitu cha maana sana hili hata mimi huwa nashindwa kulielewa unakuta kijana huku mtaani katika mazungumzo yake katika maneno kumi tano ni matusi, cha ajabu mitandaoni nako ndo hatari mtu atoa matusi mpaka unahisi kama amelelewa na ibilisi, sio ajabu kupitia huu uzi ukapokea matusi.

Kuna mmomonyoko mkubwa sana wa maadili nadhani TRA wangeanza kutoza kodi kwa kila tusi tungekusanya pesa nyingi mno za kujenga SGR na Nyerere George, kwa nini mtu afanye biashara ya matusi bure?.
 
Matusi matamu, ukianza kutukana huwezi kuacha. Hasa upate wa kutukanana nae......
 
Back
Top Bottom