Kwanini Watanzania tuna roho mbaya??!!!

mayenga

JF-Expert Member
Sep 6, 2009
4,118
1,966
Ndugu zangu,

Nimekaa nikitafakari kuhusu uroho,uchu,ufisidi wa watanzania tulio wengi sipati jibu.Kwanini tunasemana vibaya kila mahali tulipo?Kwanini uzalendp umebaki kwenye makaratasi?Ni juzi tu imeraifiwa mtoto wa mkubwa mmoja kaingiza cementi tani nyingi tu huku kukiwa na viwanda vya wazawa.Kwanini tunawanyenyekea wageni na kujisahau ya kuwa hii ni nchi yetu?Kwanini tunaangamiza nchi hii kwa madawa ya kulevya?Kwanini utanganyika wetu hatuutetei wenzetu wako busy na harakati za kuteeta visiwa vyao?Why Kwaniniiiiiiiiiiiiiiiiiii!!!???
 
Maswali mengii!! Ngoja nitafakari kidogo, kwa ujumla nchi yote imeoza labda swali dogo tu mtoa mada Ulishawahi kutoa rushwa au kupokea rushwa? Ntarudi

Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
 
nazan kijana aliyeingza cement anafahamika ambaye pia inaelezwa kuwa anafanya Illegal business nyingi...muda wao utapta time will tell na watafilisiwa
 
Si mumtaje huyu kijana kwa jina, labda wengine wanajua mengi zaidi ili wayamwage hapa jamvini.
 
Ni baada ya Azimio la Arusha kuuawa. Wafanyabiashara (halali na zisizo halali) wakaingia kwenye siasa, wakapewa madaraka, wakayatumia kujinufaisha binafsi na familia zao, wakasahau (au wakaacha) kujali maslahi ya jamii pana (haswa wanyonge na maskini), wakapeana tenda juu kwa juu, wakateua ndugu na marafiki zao kwenye nafasi za ajira kwa ajili ya ulaji wa pamoja na kulindana.....wanajeshi wastaafu nao wakapewa shavu na kupewa nafasi za uongozi wa kisiasa ili kuwalinda mafisadi walioamua kufisadi rasilimali za nchi....wananchi wakakata tamaa ya kuletewa maendeleo na viongozi wao, nao wakaamua kila mbuzi ale kwa urefu wa kamba yake bila kujali uzalendo, maadili wala kumuogopa Mungu. Kwa hiyo tunajua tumefikaje hapa na ni kina nani wametufikisha hapa. Jambo la msingi ni kuwakataa katika sanduku la kura! Tusipofanya hivyo tutakuwa pia sehemu ya tatizo na hatutakuwa na haki ya kumnyooshea kidole yeyote awaye.
 
Maswali mengii!! Ngoja nitafakari kidogo, kwa ujumla nchi yote imeoza labda swali dogo tu mtoa mada Ulishawahi kutoa rushwa au kupokea rushwa? Ntarudi

Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums

Sijawahi kula wala kutoa rushwa mdau!
 
Nawwe huna cha kupost?kwani kufanya business ni roho mbaya?nawe uifanye!!hukatazwi!!!acha wivu wwe!!!!
 
Ndugu zangu,

Nimekaa nikitafakari kuhusu uroho,uchu,ufisidi wa watanzania tulio wengi sipati jibu.Kwanini tunasemana vibaya kila mahali tulipo?Kwanini uzalendp umebaki kwenye makaratasi?Ni juzi tu imeraifiwa mtoto wa mkubwa mmoja kaingiza cementi tani nyingi tu huku kukiwa na viwanda vya wazawa.Kwanini tunawanyenyekea wageni na kujisahau ya kuwa hii ni nchi yetu?Kwanini tunaangamiza nchi hii kwa madawa ya kulevya?Kwanini utanganyika wetu hatuutetei wenzetu wako busy na harakati za kuteeta visiwa vyao?Why Kwaniniiiiiiiiiiiiiiiiiii!!!???

Yawezekana unaloliongelea hapa lina ukweli fulani, lakini katika uchunguzi wako, je ni nchi gani ambayo wananchi wake wana roho nzuri?
 
Mkuu mayenga uyasemayo ni ya kweli na kukujibu tu kwa muono wangu ni kwamba watanzania wengi tumechoka usanii na kutaka vitu vya ukweli. Hata viongozi wetu wanajuwa kuwa karibia ya vitu vingi Tanzania ni vya kimagumashi ila kuvifuatilia na kuchukua uhamuzi wa dhati ndo tatizo simply because they don't care. Kuja kwenye elimu ndiyo kabisaa kwani hata viongozi hupeleka watoto wao nje kusoma baada ya kugundua ujinga wa elimu yetu. Yaani bongo tumegeuka kuwa wachina wa Afrika kwa kutumia usanii kwa karibia ya kila kitu. In short, tunatisha!
 
Last edited by a moderator:
Hii nchi ili uishi kwa raha lazima ujifaye chizi au mwehu la sivyo kila siku utajikuta unalalamika.I mean hili joto hasira,,,,upepo hakunaaa.....
 
Wakati ukifikiri hivyo, toka nje ya Tanzania usikie wengine hasa Waafrika wenzetu wanasemaje kuhusu Tanzania na Watanzania. Usije ukastaajabu kusikia huko nje Watanzania wakionekana kama "malaika". Nimekutana na watu wengi sana toka nchi mbalimbali walionisisitizia kwamba nchi yetu ni ya watu wazuri hakuna mfano, "a country of angels". Na, huwaambii kitu. Wanaiona nchi hii na watu wake kama Paradiso! Ukiwaarifu kwamba tunazo siasa za ushindani wanabaki kushangaa tu: "mbona hatusikii kama hata kuna upinzani wowote huko?". Halafu, ni nani huyo anayeweza kutaka "kumpinga Rais wenu; such a pleasant and nice gentleman?"

Nimejiuliza sana kwa nini tuna picha kinzani kiasi hicho kati ya mambo ya ndani na yale ya nje? Jibu linalonijia ni moja tu: lazima tumefanikiwa kiasi kikubwa sana katika SANAA YA UNAFIKI katika maisha yetu. We have almost perfected the art of hipocricy! Kwa wageni, tunajibaraguza na kuwanyenyekea kupita kiasi huku kwa wenyewe kwa wenyewe tunachomana moto tu. Binafsi, nimeshawahi kuzunguka nchi na baadhi ya jamaa zangu wa nje nikitumia kiingereza na kifaransa tu katika mawasiliano yangu. Nilipata huduma za kifalme tofauti na nyakati nilipojitambulisha kama Mtanzania na kiswahili changu. Kwa wenzetu wengi ni kinyume!
 
Ndugu zangu,

Nimekaa nikitafakari kuhusu uroho,uchu,ufisidi wa watanzania tulio wengi sipati jibu.Kwanini tunasemana vibaya kila mahali tulipo?Kwanini uzalendp umebaki kwenye makaratasi?Ni juzi tu imeraifiwa mtoto wa mkubwa mmoja kaingiza cementi tani nyingi tu huku kukiwa na viwanda vya wazawa.Kwanini tunawanyenyekea wageni na kujisahau ya kuwa hii ni nchi yetu?Kwanini tunaangamiza nchi hii kwa madawa ya kulevya?Kwanini utanganyika wetu hatuutetei wenzetu wako busy na harakati za kuteeta visiwa vyao?Why Kwaniniiiiiiiiiiiiiiiiiii!!!???
My dear,
Binadamu wengi tunajisahau, tunathamini pesa kuliko utu, tunatazama matumbo yetu bila kujali hali ya mtu wa pembeni, tuko radhi kusababisha huzuni kwa mtu mwingine ili sisi tucheke.
Kusemana ovyo siku izi imekua kama njia ya kujisafisha ilihali ni kujichafua na kuzidi kujipaka matope, n abov ol ni kupoteza muda wa kufanya mambo ya muhimu.
uzalendo umebaki kwenye makaratasi sababu kila anaye shika madaraka fulani hasa siasa, anakua na dream ya kuwa na tajiri badala ya kuwa na ndoto za kuiokoa nchi yake, though atajitetea kwa point nzuri zenye ladha nzuri sana, na kuact kua ni "hero" wa nchi.
Tunawanyenyekea wageni sababu ya kupenda kulelewa kimsaada, "a begger can never be a chooser" tutafata yale amabayo wao wanataka unless tubadilike. hilo la kwanza bt mbili ni kua wenzetu wanajijali wenyewe, once they get money, wako radhi kuwa watumwa forever bila kujali kuwa wamewapeleka pabaya wananchi wanaliowategemea na kuwaamini mpaka kuwakabidhi majukumu.
Watu hawana hofu ya mungu tena, wanaabudu pesa na mali, ndivyo wanavyoona vya muhimu, Mungu aturehemu sana.
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom