Kwanini watanzania tuliowengi ni WAJUAJI TUSIOJUA? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kwanini watanzania tuliowengi ni WAJUAJI TUSIOJUA?

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Bongolander, May 19, 2012.

 1. Bongolander

  Bongolander JF-Expert Member

  #1
  May 19, 2012
  Joined: Jul 10, 2007
  Messages: 4,882
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 135
  Hebu tujaribu kujiuliza kidogo. NI kwanini watanzania wengi tukiulizwa tunasema tunajua lakini ukweli ni kwamba hatujui, au tunajua kiduchu tu?

  Ni kwanini watanzania ni hodari kusifu wengine lakini wenye wenye hatufanyi kitu cha maana? Jaribu kuuliza watu mji wa London na New York upi mzuri zaidi, angalia majibu yao, tena wengine wanaweza kujibu kwa majigambo. Halafu angalia tunachokifanya wenyewe nyumbani

  Ukiuliza ni kwanini? utasikia maelezo mengi? wakati mwingine unaweza kusikia lawama nyingi. Maelezo mengi lakini vitendo ni sifuri

  Tuna syndrome au vipi???
   
 2. Mkereketwa_Huyu

  Mkereketwa_Huyu JF-Expert Member

  #2
  May 19, 2012
  Joined: Feb 19, 2011
  Messages: 5,118
  Likes Received: 1,208
  Trophy Points: 280
  Jibu ni kwa sababu nchi imejawa na mambumbumbu na vimeo. Unaweza kutoa hoja nzuri yenye maadili ya maana na dataz unazo. utashangaa mbongo fleva (wanna bees/vijana wa vijiweni/wanaojifanya wamesoma) atakubishia huku akitia broken english wakati he/she know nothing. Anyways, hii ndo dalili za kughushi vyeti ili umalize shule haraka na upate kazi kwenye idara inayoongozwa na mjomba wakati waliosoma kweli wako wanauza mayai mitaani na kuhuzunika.
   
 3. zomba

  zomba JF-Expert Member

  #3
  May 19, 2012
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 17,081
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 0
  Kwa sababu wote ni wajinga na hatujui kitu, sasa unataka tukubali kuwa ni wajinga? Ndio maana wengi tunahadaiwa na wachache wanaoweza kukuaminisha kuwa wao wakiwa madarakani watakupa neema zote zilizopo na zisizokuwepo.

  Wewe utakaa, utatajirika bila ya kufanya kazi kwa bidii utakula na kulala tu, wao watakufanyia kila kitu. Na wote na yote mazuri yanayofanywa na wengine wao kwao ni mabaya tu, wao tu ndio wenye uwezo wa kufanya mazuri, cha kushangaza hatujaona mfano hata mmoja na bado wengi wetu tunaamini hivyo.
   
 4. Kabembe

  Kabembe JF-Expert Member

  #4
  May 19, 2012
  Joined: Feb 11, 2009
  Messages: 2,236
  Likes Received: 928
  Trophy Points: 280
  Because we don't read,na ukiona tunasoma basi ujue tuna mitihani.
   
 5. Ally Kombo

  Ally Kombo Verified User

  #5
  May 19, 2012
  Joined: Nov 11, 2010
  Messages: 11,440
  Likes Received: 68
  Trophy Points: 145
  Kwa sababu tunajua tusichojua !
   
 6. Bongolander

  Bongolander JF-Expert Member

  #6
  May 20, 2012
  Joined: Jul 10, 2007
  Messages: 4,882
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 135
  Mkuu ally Kombo mimi naona hatujui tusichojua, au hatutaki kujua tusichojua
   
Loading...