Kwanini Watanzania ni masikini? Nimeokota stakabadhi za ATM, hawana kitu kabisa

ubarinolutu

JF-Expert Member
Oct 22, 2012
1,964
3,895
Leo nimeenda ATM moja ya bank fulani kwa ajili ya kupata huduma, nikasema embu leo niokote hizi receipt za Watanzania wenzangu nizichunguze, nikainama na kuokota risiti ishirini, nilichokiona nilistaajabu jinsi Watanzania tulivo hatuna pesa.

Kati ya risiti ishirini, receipt moja tu ndo ilikuwa na kiwango cha balance kikubwa Chá pesa ambacho ni milioni sita na laki nne, hizo nyingine 19 ni zina pesa kidogo kidogo, Yani laki moja, elfu hamsini, laki 3, laki 4, laki mbili, elfu tisini,

Nikasema huu ni umasikini wa kutupa, kwanini watu hawana feza za kutosha, kwanini tunateseka, Mimi pia nilienda kutoa elfu hamsini nina balance ya laki nne Kama na thelathini. Kwanini serikali isituwezeshe Ili angalau tuwe hata na milioni Kumi.

Asante tupeane mbinu
 
Yaani ukiiona mijitu ilivyochomekea,wengine wamekuja wamepaki magari kuja kutoa elfu 50 au 20!,Hizi si ni pesa za kuweka mfukoni tu,huenda akaunti hizi ni za lazima za kupokelea mishahara.

Unakuta dem amekaa anajua kidume chake kinaenda kudroo ela lakini kikifika kwenye kuku kinatetemeka kinaomba dem aagize broiler,kinaomba aagize mtori,kinaomba anywe apple quencher.

Hili litaifa ndiyo maana watu wanaumwa sana PRESSURE,mioyo yao haitulii,kauli za wakubwa pressure,nyumba za kupanga pressure,madem pressure,mchango wa Luku pressure,maji pressure,halafu bado na mavikao ya HARUSI,mioyo haitulii.
 
Hili hapa jibu
20190526_102136.jpeg
 
Back
Top Bottom