Kwanini Watanzania na Tanzania ni maskini pamoja na rasilimali (resources) tulizo nazo? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kwanini Watanzania na Tanzania ni maskini pamoja na rasilimali (resources) tulizo nazo?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Wambandwa, Dec 26, 2006.

 1. Wambandwa

  Wambandwa JF-Expert Member

  #1
  Dec 26, 2006
  Joined: Dec 3, 2006
  Messages: 2,240
  Likes Received: 337
  Trophy Points: 180
  KWA NINI WATANZANIA WENGI NI MASKINI?

  Sijawahi kumwona Mtanzania kwa wakati wowote ule ameondokana na umaskini, umaskini ambao sasa ni mkubwa mno na unakaribia kutudidimiza.

  Binafsi nauchukulia umaskini kama kukosekana kwa mahitaji ya lazima ya kila siku kwa mwanadamu: malazi mazuri, chakula bora (ambavyo hivyo vyote vinapatikana kama binadamu huyo huyo anakuwa na njia ya kujipatia kipato) na uongozi bora wa haki unaofuata sheria (ili huduma mhimu za jamii: shule, hospitali, barabara, maji salama nk vipatikane).

  Watanzania wengi tu maskini wa kutupa kwa sababu tunagharimia mno uendeshaji wa kila siku wa serikali yetu (isivyokuwa lazima).

  Wanasiasa ndio watoa maamuzi hata ya kitaalauma hata kama si wana taaluma husika.

  Wataalamu wetu hawathaminiwi na hii inatugharimu sana. Kihio kutoka A. Kusini analipwa mamilioni ya pesa hata kama utendaji wake ni mbovu. Mfano NET GROUP SOLUTION, wanaishi maisha ambayo hata kwao hawana. Na wazawa waliokuwa nao wanajilipa pesa ambayo haina mfano.

  Wanasiasa wanajilipa pesa nyingi ukilinganisha na wataalamu waliosomea taaluma mbali mbali.

  Tatizo la wanataaluma kutothaminiwa limewasukuma baadhi yao kujiingiza ktk siasa. Hapa ndo kichekesho kinatokea. Mwana taaluma huyo huyo akiwa nje ya siasa anakuwa critic wa governing system! Kuna prof. mmoja ambaye ni waziri kwa sasa wakati akiwa chuoni alikuwa ni mtu ambaye aliponda jinsi nchi yetu inavyoongozwa shaghala baghala, alivyoukwaa ubunge huko kwao akateuliwa ktk baraza la mawaziri.. nasikia alikwenda kuwashukuru waliompigia kura kwa dege la jeshi kwa gharama ya serikali. Wako wengi wa aina hiyo.

  Elimu ya mafunzo ya darasani na hali halisi iliyoko nje katika jamii inapaswa kuwa lila na fila. Unaelimishwa ili uweze kutumia elimu katika maisha yako ya kila siku.

  Ktk hali hiyo, mwanafunzi anaye hitimu darasa la 12 au 14 ni vizuri aongeze na taaluma kama uhandisi (VETA), uhasibu nk. Wa chuo kikuu huyo tayari ni wakutumika ama kwa kujiajiri au kuajiriwa. Kujiajiri hapa ni kimbembe tatizo linakuwa mtaji.,..

  Viongozi: Kama nilivyoeleza hapo juu, waviongozi wetu mara wachaguliwapo kuingia madarakani ni moja kwa moja wanona matatizo yao yamekwisha, hivyo swala la kumshirikisha mwanachi wa kawaida, labda ingekuwa kupiga kura kunakaribia.

  Mila na desturi zetu: kuna jitihada za makusdi kuzifilisisha.... (ni mjadala mrefu).


  KWA KIFUPI UMASKINI WETU UNATOKANA NA KUTOKUWA NA VIONGOZI WAADILIFU, WAONGOFU, WACHA MUNGU. TULIOKUWA NAO NI WANAFIKI NA WAFISADI.

  ===================

  Return Of Undertaker anasema,

  KWA WALE MSIO IJUA TANZANIA VIZURI SOMENI KWA MAKINI UTAJIRI WA TANZANIA HALAFU JIULIZE KWA NINI NI MASIKINI WA MWISHO NA MALI ZOTE HIZI


  1.Tz ilipata uhuru mwaka 1961 ina miaka 54 tangu ipate uhuru ikiwa ni ya kwanza Afrika Mashariki.

  2.Tz Kwa miaka 38 imeongozwa na CCM peke yake ambayo ni zao la TANU na ASP.

  3.Tz ni nchi ambayo haijawahi kupata majanga makubwa kama matetemeko ya ardhi, magonjwa
  ya mlipuko kama ebola, mafuriko na vimbunga au ukame.

  4.Tz ni nchi ambayo imekuwa na kitu ambacho nchi za Afrika zimekikosa. Kitu hicho ni AMANI. Kwa miaka yote 54 ya uhuru haijawahi kupigana vita vya wenyewe kwa wenyewe.

  5.Tz ina ukubwa wa 945,000 km za mraba yani sawa na uchukuwe Denmark, France, United Kingdom, Netherland, Ireland ujumlishe zote kwa pamoja.

  6.Tz ina eneo la bahari lenye ukubwa wa 1,424 km. Bahari inaleta fursa za usafirishaji, uvuvi, utalii na nyinginezo.

  7.Tz ni nchi ambayo imepakana na nchi za (Uganda, Rwanda, Burundi, Zambia, Malawi, D. R. Congo) ambazo zinategemea bahari yetu kwa usafirishaji wa mizigo na ni fursa nzuri ya kuzipelekea bidhaa za viwanda vyetu.

  8. Tz ina maziwa makubwa manne na mengine madogo mengi.
  Maziwa matatu makubwa yako kwenye kumi bora za ukubwa duniani na Maziwa makubwa matatu yote yapo Tanzania. Ziwa Victoria ni la tatu kwa ukubwa duniani (la kwanza Afrika) na ziwa
  Tanganyika ni la sita kwa ukubwa (la pili Afrika) na la kwanza kwa kuwa na kina kirefu duniani. Ziwa Nyasa ni la tisa kwa ukubwa duniani (ni la tatu Afrika).

  9.Tz ina mito mikubwa kumi ambayo ni mto Kagera, mto Ruvuma, mto Rufiji, mto Wami, mto Malagarasi, mto Mara, mto Pangani, mto Ruaha, mto Gombe, mto Mweupe wa Nile na ina mito midogo mengi kama mto Kilombero, mto Mbemkuru n.k

  10.Tz ndiyo nchi ya kwanza Afrika kuwa na maji mengi yasio na chumvi yaliyokuwa kwenye uso wa dunia (fresh surface water) kutokana na kuwa
  na mito na maziwa mengi na kupitiwa na bonde la ufa.

  11.Tz ni nchi ya nne kwa uzalishaji dhahabu Afrika baada ya Afrika Kusini, Ghana na Mali na ipo TOP 20 duniani. Kuna migodi nane inayochimbwa dhahabu na miwili imefungwa. Migodi inayochimbwa ni Buzwagi gold mine- (Shinyanga), Geita gold mine-(Geita), Golden pride gold mine-Nzega (Tabora), Bulyanhulu gold mine- (Shinyanga). New leuka Gold mine- (Mbeya),
  Tulawaka gold mine-(Kagera), North mara gold mine-(Mara). Iliyofungwa ni Korandoto gold mine (Shinyanga), Senkenke gold mine-(Shinyanga???).

  12.Tz ina madini ya almasi yanayopatikana Mwadui Shinyanga. Mgodi huo ulianza kuchimbwa tangu mwaku 1940. Mpaka leo bado unachimbwa, unamilikiwa na kampuni ya Waingereza.

  13.Tz ni nchi ya kwanza na ni nchi pekee inayozalisha madini ya tanzanite duniani. Mkufu wa kuvaa shingoni unatengenezwa na tanzanite na almasi unauzwa hadi shilingi milioni 25 za Kitanzania.

  14.Tz ina madini ya chuma yanayopatikana Mchuchuma, Ludewa- Njombe mgodi unamilikiwa na Wachina. Mgodi huo una hifadhi ya madini ya chuma tani milioni 122 ambayo yanawezwa kuchimbwa kwa zaidi ya miaka 100.

  15.Tz ina madini ya makaa ya mawe (Coal) yanayochimbwa Kiwira Mbeya, Mchuchuma na
  Liganga Njombe. Unamilikiwa na Wachina. Pia mgodi wa Ngaka kule Mbinga-Ruvuma unamilikiwa na
  kampuni ya Tancoal ya Australia. Hifadhi ya madini ya makaa ya mawe iliyopo ni tani bilioni 2. Makaa ya mawe ndio chanzo cha pili cha umeme wa bei nafuu duniani baada ya maji.

  16.Tz ina hifadhi ya madini ya Uranium kule Dodoma (Bahi) na ni mgodi ambao unamilikiwa na
  Warusi. Pia madini haya yanapatikana Namtumbo (Mkuju), Galapo, Minjingu, Mbulu, Simanjiro, Lake Natron, Manyoni, Songea, Tunduru, Madaba and Nachingwea.

  17.Tz ni moja ya nchi tatu Afrika zikiwemo Zimbabwe na Madagascar kwa kuwa na madini mengi ya graphite. Madini haya yapo Tanga, Mahenge-Morogoro, Mererani- Manyara. Madini ya graphite ndiyo yanayotumika
  kutengenezea betri za simu, kwenye injini na brake za magari na kwenye karamu za risasi (pencili).

  18.Tz ina madini ya nickel yanayopatikana kule Kabanga Kagera, milima ya Uluguru-Morogoro, North Mara, Ngasoma-Mwanza.

  19.Tz ni nchi ya tatu duniani kwa kuwa na hifadhi kubwa ya magadi soda duniani baada ya Marekani na Uturuki. Magadi soda hutumika kutengeneza vioo vya aina zote. Vioo vya nyumbani hadi magari pia kutengeneza sabuni na dawa mbalimbali za usafi.

  20.Tz ina hifadhi na mgodi wa madini ya niobium uliopo Panda hill Mbeya ambao ndio utakuwa mgodi mkubwa wa kwanza Afrika na wa nne duniani. Mgodi huu unamilikiwa na kampuni ya Australia. Madini ya niobium ni magumu sana
  hutumika kutengeneza mabomba pamoja na madini chuma pia hutumika kutengeneza baadhi ya sehemu za injini za ndege na vyombo vinavyoenda nje ya uso wa dunia (mfano Apollo 15 CSM), vioo vya computer na lenzi za camera.

  21.Tz ni nchi ya kwanza Afrika na ya pili duniani kwa kuwa na vivutio vingi vya utalii. Ya
  kwanza ni Brazil. Nchi zilizokuwa kwenye tano bora kwa utalii Afrika ni Tanzania, Botswana, Afrika Kusini, Kenya na Zambia.

  22.Tz ina mbuga zipatazo 16 na ile mbuga maarufu kuliko zote duniani Serengeti ipo Tanzania, mbuga iliyopakana na bahari iitwayo Saadani ipo Tanzania na mlima mrefu kuliko wote Africa Kilimanjaro upo Tanzania.

  24. Tz ina ardhi kubwa yenye rutuba na inayofaa kwa kilimo cha mazao mengi tofauti tofauti. Mashamba makubwa ya mpunga kwa mfano yaliyokuwa chini ya Shirika la NAFCO yalitoa mazao ya kulisha Tanzania na pia nchi nyingine.

  24.Tz ina gesi ya asili ya Carbon Dioxide (CO2) inayovunwa kule Kyejo, Rungwe-Mbeya na kampuni ya TOL. Gesi ya asili ya cardon dioxide inatumika sana kutengenezea vinywaji laini kama soda, bia na pia kutengenezea madawa, makaratasi na kutibia maji (water treatment).

  25.Tz ina gesi ya asili inayopatikana katika kisiwa cha Songo songo mkoa wa Lindi. Gesi hii imekuwa ikichimbwa na kusafirishwa hadi Dar es salaam tangu mwaka 2004. Inamilikiwa na kampuni ya Songas ya Uingereza.

  26.Tz imengundua gesi ya asili yenye zaidi ya meta za ujazo trilioni 55.3 iliyongunguliwa katika maeneo ya bahari ya Hindi na Mtwara.

  Pamoja na sifa zote hizi lakini Tz ni nchi iliyo kwenye kundi la nchi maskini duniani ambayo asilimia kubwa ya raia wake wanaishi chini ya Dola moja za Marekani na hali ya huduma za kijamii ikiwa duni.

  TATIZO NI NINI? NANI ANAFAIDI HUU UTAJIRI? NANI WA KUMLAUMU? NANI NI SABABU?
  KWA NINI TUNASHINDWA KUTUMIA HUU UTAJIRI?


  ===================================
  Mtaalam aeleza kwanini Tanzania ni maskini

   
 2. d

  dondola Member

  #2
  Dec 26, 2006
  Joined: Nov 14, 2006
  Messages: 29
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Mimi nafikiri umasikini ni kukosa mahitaji uyatakayo. Wewe kama unataka maji na huna maji au unayapata kwa shida (kama wewe unakubali kuwa unapata shida kuyapata) basi una umasikini kwenye nyanja hiyo. Kama unaumwa na umeshindwa kujitibu basi huo pia ni umasikini.

  Kwa kifupi maendeleo ya dunia ya kwanza, na wao kuja kwenye dunia yetu ya tatu, ndio kumeongeza umasikini wetu kwani kabla ya wageni kuja, tulikuwa tumeridhika na maisha yetu ya ujima, lakini hii leo, tumekwishavuruga system yetu ya ujima ya kujitegemea, tunategemea teknolojia ya wageni, inatuchanganya bado, hivyo tunashindwa kidhi mahitaji yetu. Kwa hiyo hakuna ubishi kuwa tuko masikini kwani hatupati tena mahitaji yetu kama tutakavyo leo (wakati wa ujima hatukuwa masikini kama hii leo).

  Kuna filosofa maarufu wa Kiyahudi-Kimarekani aitwaye Maslow aliamua kufanya utafiti kuhusu mahitaji ya binadamu (ingawa alifanya utafiti kwa kwanza kuchunguza nyani, na pia binadamu wachache waliofanya vitu vikubwa hapa duniani kama Einstein, Lincoln, etc Tunaweza kutumia utafiti wake kama kianzio katika kujadili umasikini wetu)

  [​IMG]

  bonyeza hapa kusoma huo utafiti wake: MASLOW'S HIERARCHY OF NEEDS

  Educational Psychology Interactive: Maslow's hierarchy of needs
  http://www.ship.edu/~cgboeree/maslow.html


  Abraham Maslow developed a theory of personality that has influenced a number of different fields, including education. This wide influence is due in part to the high level of practicality of Maslow's theory. This theory accurately describes many realities of personal experiences. Many people find they can understand what Maslow says. They can recognize some features of their experience or behavior which is true and identifiable but which they have never put into words.
  Maslow is a humanistic psychologist. Humanists do not believe that human beings are pushed and pulled by mechanical forces, either of stimuli and reinforcements (behaviorism) or of unconscious instinctual impulses (psychoanalysis). Humanists focus upon potentials. They believe that humans strive for an upper level of capabilities. Humans seek the frontiers of creativity, the highest reaches of consciousness and wisdom. This has been labeled "fully functioning person", "healthy personality", or as Maslow calls this level, "self-actualizing person."

  Maslow has set up a hierarchic theory of needs. All of his basic needs are instinctoid, equivalent of instincts in animals. Humans start with a very weak disposition that is then fashioned fully as the person grows. If the environment is right, people will grow straight and beautiful, actualizing the potentials they have inherited. If the environment is not "right" (and mostly it is not) they will not grow tall and straight and beautiful.

  Maslow has set up a hierarchy of five levels of basic needs. Beyond these needs, higher levels of needs exist. These include needs for understanding, esthetic appreciation and purely spiritual needs. In the levels of the five basic needs, the person does not feel the second need until the demands of the first have been satisfied, nor the third until the second has been satisfied, and so on. Maslow's basic needs are as follows:

  Physiological Needs
  These are biological needs. They consist of needs for oxygen, food, water, and a relatively constant body temperature. They are the strongest needs because if a person were deprived of all needs, the physiological ones would come first in the person's search for satisfaction.

  Safety Needs
  When all physiological needs are satisfied and are no longer controlling thoughts and behaviors, the needs for security can become active. Adults have little awareness of their security needs except in times of emergency or periods of disorganization in the social structure (such as widespread rioting). Children often display the signs of insecurity and the need to be safe.

  Needs of Love, Affection and Belongingness
  When the needs for safety and for physiological well-being are satisfied, the next class of needs for love, affection and belongingness can emerge. Maslow states that people seek to overcome feelings of loneliness and alienation. This involves both giving and receiving love, affection and the sense of belonging.

  Needs for Esteem
  When the first three classes of needs are satisfied, the needs for esteem can become dominant. These involve needs for both self-esteem and for the esteem a person gets from others. Humans have a need for a stable, firmly based, high level of self-respect, and respect from others. When these needs are satisfied, the person feels self-confident and valuable as a person in the world. When these needs are frustrated, the person feels inferior, weak, helpless and worthless.

  Needs for Self-Actualization
  When all of the foregoing needs are satisfied, then and only then are the needs for self-actualization activated. Maslow describes self-actualization as a person's need to be and do that which the person was "born to do." "A musician must make music, an artist must paint, and a poet must write." These needs make themselves felt in signs of restlessness. The person feels on edge, tense, lacking something, in short, restless. If a person is hungry, unsafe, not loved or accepted, or lacking self-esteem, it is very easy to know what the person is restless about. It is not always clear what a person wants when there is a need for self-actualization.
  The hierarchic theory is often represented as a pyramid, with the larger, lower levels representing the lower needs, and the upper point representing the need for self-actualization. Maslow believes that the only reason that people would not move well in direction of self-actualization is because of hindrances placed in their way by society. He states that education is one of these hindrances. He recommends ways education can switch from its usual person-stunting tactics to person-growing approaches. Maslow states that educators should respond to the potential an individual has for growing into a self-actualizing person of his/her own kind. Ten points that educators should address are listed:

  - We should teach people to be authentic, to be aware of their inner selves and to hear their inner-feeling voices.
  - We should teach people to transcend their cultural conditioning and become world citizens.
  - We should help people discover their vocation in life, their calling, fate or destiny. This is especially focused on finding the right career and the right mate.
  - We should teach people that life is precious, that there is joy to be experienced in life, and if people are open to seeing the good and joyous in all kinds of situations, it makes life worth living.
  - We must accept the person as he or she is and help the person learn their inner nature. From real knowledge of aptitudes and limitations we can know what to build upon, what potentials are really there.
  - We must see that the person's basic needs are satisfied. This includes safety, belongingness, and esteem needs.
  - We should refreshen consciousness, teaching the person to appreciate beauty and the other good things in nature and in living.
  - We should teach people that controls are good, and complete abandon is bad. It takes control to improve the quality of life in all areas.
  - We should teach people to transcend the trifling problems and grapple with the serious problems in life. These include the problems of injustice, of pain, suffering, and death.
  - We must teach people to be good choosers. They must be given practice in making good choices.


  Baada ya kusoma hizo needs (hata kama huziafiki, zitakupa mwanga wa kudefine za kwako;)) nadhani kuwa umasikini wetu uko haswa pale kwenye physiological needs, ingawa mtu atapata security needs(ya kiwango chake), love na self esteem; matatizo ya physiological needs na security ndio umasikini wetu halisi.
   
 3. d

  dondola Member

  #3
  Dec 26, 2006
  Joined: Nov 14, 2006
  Messages: 29
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  People are living in poverty if their income and resources (material, cultural and social) are so inadequate as to preclude them from having a standard of living which is regarded as acceptable by general society - VERY TRUE

   
 4. P

  Phillemon Mikael JF Gold Member

  #4
  Dec 26, 2006
  Joined: Nov 5, 2006
  Messages: 8,856
  Likes Received: 2,430
  Trophy Points: 280
  Umasikini hautaondoka kwa kuwa tumeamua kuweka nchi rehani,rasilimali zote kwa wageni. Mada nzuri hii.
   
 5. M

  Mwanagenzi JF-Expert Member

  #5
  Dec 26, 2006
  Joined: Sep 11, 2006
  Messages: 690
  Likes Received: 137
  Trophy Points: 160
  General society ni ipi?
   
 6. M

  Mkandara Verified User

  #6
  Dec 27, 2006
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Wanabodi,

  Sasa naona vitabu vinaanza hapa!

  Mnataka kuipotosha kabisa mada nzima kwa hizi definition. Hiyo ya Maslow's sijui inahusiana kivipi na Umaskini wetu zaidi ya kuwa hisia (instinctoid) ambazo hata wanyama na viumbe wote wanavyo...lakini sidhani kama kuna wanyama maskini (fukara) kati ya kundi la wenzao.

  Swala hapa ni umaskini wetu!...Why Tanzania is a poor nation?

  Kwanza huu umaskini umetokana na kitu gani?...Guys we can't think of eradicate poverty if we don't look for the source!.. haya mengine ya theories ni kubabaishana tu kwani sii lazima will work!

  Having said that, ebu just ask yourself:- Why remained poor amidst huge infomal sector with ample resources?..WHy continuous flow of aids has failed to transform the societies?

  Tukisha pata jibu la source ya hili gonjwa nadhani itakuwa rahisi kutafuta dawa... kwa hizo research zinazohusiana na viambukizo (cells) vya hili gonjwa - Umaskini.
   
 7. d

  dondola Member

  #7
  Dec 27, 2006
  Joined: Nov 14, 2006
  Messages: 29
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Mkandara


  Ni kweli kuwa ukiangalia harakaharaka utasema kuwa umasikini wetu hauna uhusiano wowote na hii hierarchy ya Maslow. Lakini central idea ya Maslow ya 'human needs' ina uhusiano mkubwa na umasikini wetu, na mimi ndio hiyo iliyonivutia, hata kama hoja zake bado ziko criticable, lakini idea yake ni ya msingi: MAHITAJI.

  - Kumbuka kuna watoa hoja hapa wameongelea swala la mtu aliyeridhika na maisha yake ya kubangaiza, anaishi bila ndoto ya maendeleo, ingawa wewe unamwona masikini na unamwonea huruma, sasa sio kweli kuwa huu ndio umasikini unaotusumbua leo?

  - Kwanini tunawalaumu viongozi wetu kuwa ni walafi, hata wale damu mpya?

  - Kwanini asilimia kubwa ya wanaomaliza shule wanaangalia ajira itakayotoa pesa nzuri: ni wanasayansi wangapi wanaomaliza UDSM kila mwaka na baadae kukimbilia Pricewaterscoopers kwenye interviews za 'kuhesabu pesa'?. Ni kwanini wanalazimika kufanya hivyo? Je wakiwa viongozi kesho?

  Theories huwa ni mbaya na nzuri vilevile, kwani majibu yote huzaliwa kutoka theories.

  Nafikiri waijua ecology: wanyama porini wafananao k.v.simba, hufanana kwa tabia na teknolojia watumiayo kupambana na mazingira yao. Turudi kwa binadamu, hatufanani, kwa vile hatutumii teknolojia ifananayo kupambana na mazingira yetu.

  Na hicho ndio chanzo cha umasikini wetu, kwa maana ya kuwa kabla ya dunia kuunganishwa (kuja kwa wageni), jamii zetu hazikuwa masikini. Zilikuwa na maisha yao, na teknolojia yao iliyowafaa kutokana na mahitaji yao, hawakuhisi kupungukiwa, mahitaji waliyapata, hawakuwa masikini.

  Wageni wakaja na teknolojia zao, 'ecosystem' ikawa disturbed, predator kaingia, ndio chanzo cha umasikini. Wakaingiza mfumo wao kwenye jamii zetu, wakatuonjesha teknolojia yao, toka hapo tumelazimika/tumeamua(?) kuwafuata ili tuikamate teknolojia yao, tuwe na style moja ya kupambana na mazingira yetu. Ni safari ndefu.
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 8. M

  Mkandara Verified User

  #8
  Dec 28, 2006
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Duuuuh! Dondola,

  Ndugu yangu darasa hilo mwenzako sioni ndani kabisa...

  Hayo ma-ecology na ecosystem mwenzako ndio kwanza nayasikia...

  Nachokuomba ni lugha nyepesi inayotafsirika vizuri kuhusu huu umaskini wetu kwani navyoamini mimi tunapotafuta dawa ya AIDS tunatazama source yake, jinsi inavyoambukiza na cells za gonjwa hili lakini sio kurudi nyuma sana na kutafuta nini maana ya Maradhi (Sickness) na uhusiano wake na mwili wa binadamu... Huko tunakuachieni nyie wasomi mliosomea elimu ya viumbe. Nafikiri sisi hapa tuna summaries mavitu to provide a common foundation of fact for conversation about, then action to close!

  Policymakers na sisi the public-at-large imetulazimu tuwe makini zaidi ktk kuangalia hili gonjwa la Umaskini than ever before.

  Wote, maskini kwa matajiri, wenye elimu na wasiokuwa na elimu tunaweza kupambana na hili janga bila kutumia lugha nzito kwani Umaskini sio technologia!

  Umaskini hauna rangi wala kipimo cha elimu ya mtu ila naweza kusema uzito wake ni sawa na ule wa kutafuta source ili kufuta Ujinga - ELIMU.

  Kwa kuanza tu naweza kusema hakuna uuwiano wa mapato kati ya mikoa yetu na wilaya zake ktk ujenzi wa investments zinazotoa ajira!... region ambazo ziko funded zaidi na kuwavutia wawekeshaji ndizo zenye maskini wachache. Sawa na mashule yetu ambayo yako funded vizuri huwa yanatoa wafaulu wengi kuliko yale yaliyotupwa!

  Na sababu kubwa ktk elimu utakuta kwamba zile shule zilizokuwa funded vizuri huwa na walimu wenye ujuzi zaidi ya zile zisizokuwa na fedha!..vifaa vya elimu n.k.

  Kwa hiyo uhusiano wa elimu na Umaskini hauhitaji kumtazama binadamu kama mnyama na mbinu zake za kinyama ktk kuishi pamoja. Laa sivyo tutakuwa tunawashtumu baadhi ya watu kuwa wao ni Predators!

  Sina maana kuwa viongozi wetu na baadhi ya matajiri hawawezi kuyafanya haya kwa makusudi ya mnyama..ila sidhani kama umaskini wetu unaambukizwa na hizi human natures za ecology!

  So, we beteer off start with a common foundation of fact for conversations about, then action to close!.
   
 9. Wambandwa

  Wambandwa JF-Expert Member

  #9
  Dec 28, 2006
  Joined: Dec 3, 2006
  Messages: 2,240
  Likes Received: 337
  Trophy Points: 180
  dondola

  Hiyo lugha si kwamba inaniacha mimi nyuma peke yangu, nafikiri ni wengi umetuchanganya!!

  Maisha yale 'stone age' hayawezekani kwa namna yoyote ile kuwa si ya umaskini. Nafikiri tulikuwa bado kwenye ujima.

  Wageni walipoingia wakiwa na teknologia mpya nafikiri ni hapo mambo yakawa mazuri na mpaka sasa wewe dondola umebukua kiasi hicho.

  Lakini naona hiyo lugha uiyeyushe mno zaidi iliwenzangu wengine tukwelewe!
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 10. M

  Mkandara Verified User

  #10
  Dec 29, 2006
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Maneno aliyoyasema Mh. Mzee Mtei katika moja ya hotuba zake kujibu hoja nadhani huo ni mwanga tosha kabisa hasa jinsi serikali inavyotakiwa kuwa kabla kabisa ya kuwafikia wananchi wenyewe!...POLICY!

  Jambo kubwa ambalo nimeweza kulifuatilia mimi kwa muda sasa, nii hii dhana ya kufanya mambo kwa pupa bila kujiandaa kwanza. mathlan, chukulia mfano mdogo wa interview ya Mkapa aliposema nchi kuwa na zahanati 3,000 lakini hazina mahudumu wake wala vifaa.

  Tunajenga mashule bila kuandaa walimu wa kutosha!...Jamani sasa unawalaumu Wahisani kwa kutokuwa na sera nzuri wewe mwenyewe!..Unakuwaje ujenge shule kibao hali huna walimu wala vitabu. majengo ya Zahanati hali huna fedha za vifaa wala wasomi!

  I mean, guys kweli tutaweza kufika huko tunakokwenda ikiwa hatujiandai mapema kwanza kabla ya Ujenzi?..Tutaijenga nchi kama nyumba za Kariakoo ambazo kila siku watu hufyatua tofali kulingana na kipato cha siku.

  Hii mikopo tunayopewa kwa nini tusiiweke kando kwanza kuwafundishe mawanachi Unesi, Udaktari na hata kupata idadi ya walimu wanaoweza kutosheleza shule kadhaa kisha hesabu zetu ziendane na graduates hawa!...

  Kichekesho kingine nimeona hotuba ya EL akisisitiza kujenga shule zaidi ili wanafunzi wa darasa la saba wapate NAFASI shule za sekondari, hapa akiwa na maana anategemea asilimia 70 watashinda lakini nafasi za kwenda sekondari ni chache zaidi!...Kifupi hapa kushinda mtihani sii hoja ila watu wanagombea nafasi za kuingia..haya huko nyuma tumeona tatizo hatuna walimu yaani maajabu yanazidi kupandana tu.

  Hivyo hivyo ktk kufuta Umaskini, nadhani serikali yetu inatakiwa kuwaanda wananchi kwanza kabla huja introduce kitu. Yametukuta ktk Ubinafsishaji, sasa Uwekeshaji ambako kila mwajiri amedai Watanzania hatuna elimu ama Ujuzi kwa hiyo wanachukuliwa watu toka nje!..

  Hata malori ya kusomba mchanga wa dhahabu, dereva anatoka South Afrika eti haya magari ni makubwa sana! guys, haya magari ni Dumptrucks tu hakuna mtu anayebeba uzito huo yeye na udereva wa dumptruck hauna tofauti na ule wa lori la mchanga!.. kuna viji gear vya hapa na pale ambavyo mtu akiwekwa darasani siku moja anaweza kabisa kulisukuma Lori. Na imekuwaje wananchi hawakuandaliwa mapema ktk uzalishaji wa dhahabu ili wapate ajira?

  Umaskini wetu umetokana na mentality ya kutojiamini!...Leo hii kila nchi iliyokuwa ya kijamaa hakuna hata moja uchumi wake haukuwi zaidi ya asilimia 7.

  Zote zilizobadilisha mfumo wake wa kiuchumi zinakwenda mbio kishenzi, Sii China, Ireland wala Vietnam wote wanakwenda kasi ya ajabu ktk kila fani ya maendeleo. tatizo kubwa ni kwamba wenzetu waliwaanda wananchi wao kushika nafasi ambazo wamezipa kipaumbele ktk maendeleo yake. Wachina ndio manpower ya kila kinachozalishwa China.

  Waliteremsha wanafunzi kibao nchi za magharibi na leo hii tunayaona matunda. Sisi tumekalia Elimu ni shule ya msingi hadi University wakati hatuna walimu wa kutosha wala vifaaa vya kimataifa kisha tunategemea kuzalisha Gas na Madini!

  Tuinasisitiza viwanda sijui vya kuzalisha kitu gani maanake hatuna wasomi wala shule zinazofundisha ujuzi huo. I mean hata kama ni kushona viatu basi fungueni shule za designing zenye hadhi na sio ktk vyumba vya mitaa ya Jamhuri.

  Wasomi wetu wengi wapo kwenye kilimo, leo hii kilimo ni uchumi uliosahahulika....sii ukulima wa mazao, mifugo wala uvuvi kote ni sinema tu wageni ndio wametawala.

  Kifupi, Tanzania tupo nyuma sana kielimu kulingana na maendeleo ya kiuchumi tunayokusudia!..
  dondola,
  All we need is:- Mtei with his vision!..
  tubuni filosofia na sera ambazo zingeepusha taifa kurudia makosa ya zama za ujamaa zenye sera zisizo na tija na uendeshaji wa kiimla. Wananchi ni lazima waweze kuamua mambo yahusuyo maendeleo ya taifa lao kwa uhuru kamilifu, ujasiri na bila ya woga na kuepuka utawala wa kiimla. Rasilimali za nchi ni lazima zitumike kunufaisha wananchi. Serikali ina wajibu wa kuweka mazingira yanayowezesha mitaji kuingia nchini.

  Uhuru wa soko ndiyo njia endelevu ya kuvutia mitaji ili raslimali za nchi ziweze kutumika kikamilifu, lakini papo hapo lazima umma wote ufaidike na mazingira yawekwe kuhakikisha wananchi wanajituma kwa kadri iwezekanavyo kupata kipato chao wenyewe. Wasiojiweza na ambao hawakupata ajira watadhaminiwa na umma. Miundombinu ya kiuchumi na ya kijamii itamilikiwa na umma na kuendeshwa kisayansi, kuhakikisha ni endelevu na ina tija. Miradi ya umma itabuniwa na kuendeshwa bila pupa za kisiasa..................................."  As to say, we luck:- Legal empowerment of the poor people which includes 1. Education, 2. Propety rights, 3. Entrepreneurship, 4. Labour rights, 5 Access to justice and rule of law..
  No one is above the law!
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 11. d

  dondola Member

  #11
  Dec 30, 2006
  Joined: Nov 14, 2006
  Messages: 29
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Wambandwa, ni kweli nimeongea lugha nzito mno na iliyo ngumu kueleweka:) Ngoja nifafanue ujumbe ulio nyuma ya lugha hiyo:Hoja inaongelea umasikini wa mtanzania, ila mimi nimeenda mbali hadi kwenye umasikini wa mtu mweusi
  - Jamii nyingi duniani zinaheshimu sana tamaduni zao licha ya elimu zao, lakini sivyo hali ilivyo kwa majority ya jamii za watu weusi, why? Ngoja nirudi kwenye mambo ya kanisa kidogo, kumradhi:) Mtaguso wa II wa Vaticano umefanya jambo moja zuri sana kwa kanisa la Afrika: Utamadunisho.

  Kuingiza tamaduni za kiafrika kwenye ibada za waafrika kadiri ya mazingira yao. Kitendo hicho ni vyema kikiendelea hadi nje ya kanisa: kuziheshimu kwa makusudi mazima tamaduni zetu-sio siri hii leo idadi kubwa ya waafrika tunataka kuwa wazungu. Kwa mfano mdogo tu 'Salamu' lakini nyuma yake kunaibua swali kubwa :waafrika walioko ulaya wanasalimiana kizungu, waarabu walioko ulaya wanasalimiana kiarabu, waasia walioko ulaya wanasalimiana kikwao. :eek:

  - Licha ya kwamba waafrika tunaongeza kasi ya kusalimiana kizungu, wazungu wakihamisha viwanda kwao vinaenda East Europe au Asia, kumbe kusalimiana kizungu hakuelekei kutusaidia eeh? Je tuendelee na mwelekeo huu au tunahitaji pia 'mtaguso' mwingine wa kuheshimu mila zetu?
  -etc

  Anyway, hata mimi pia nasalimiana kizungu,ila kwa kuongelea hayo maecology na predators, ujumbe wangu ulikuwa ni tuangalie vizuri nafasi ya culture kwenye maendeleo.

  ----------
  Mkandara nimekuelewa vilivyo kwa darasa lako, hasa hasa uliposisitiza ukweli huu:
   
 12. Mtu wa Pwani

  Mtu wa Pwani JF-Expert Member

  #12
  Jun 14, 2007
  Joined: Dec 26, 2006
  Messages: 4,095
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 135
  jamani hivi tunavyopiga kelele kumbe Rais wetu hapati usingizi kwa kufikiria jinsi gani ya kuondosha umaskini wetu, hivi haya ni ya kweli au ndio usanii?

  Umaskini wa watu wangu unanikosesha raha - JK

  2007-06-14
  Na Mwandishi Maalum  Rais Jakaya Kikwete amesema, hali ya dhiki na umaskini wa wananchi nchini inamkosesha raha na kwamba dhamira yake ni kuwaondoa katika hali hiyo.

  Alisema hali ya umaskini inayowakabili zaidi ya asilimia 39 ya watanzania hasa wale wa vijijini ni jambo linalomsumbua sana.


  `Wakati wote wa kampeni za uchaguzi, nilijitahidi sana kuelezea nia na dhamira yangu hiyo ya kuinua hali ya maisha ya wananchi kwa kuwapatia fursa ya kupata mikopo nafuu ili hatimaye waweze kuendesha shughuli za ujasiriamali zitakazowaongezea kipato. Ni dhamira niliyonayo na ni jambo linalonigusa sana,` alisema.


  Alisema ndio maana anabuni mikakati na mipango mbalimbali ya kuwaibua wajasiriamali wadogo na wakati ili hatimaye waongeze kipato chao na kuboresha maisha yao.


  Aliyasema hayo juzi wakati alipokuwa akibadilishana mawazo na mtaalam maarufu wa uchumi, mwanzilishi wa Benki ya watu maskini, Gramees Bank na Mshindi wa Tuzo ya Amani ya mwaka 2006 (Nobel Peace Prize Laurette), Profesa Yunus Mohamed, kutoka nchini Bangladesh.


  Alisema kuanzishwa kwa mchakato wa utoaji wa mikopo nafuu ambayo kwa sasa imepachikwa jina la `Mabilioni ya JK` ni sehemu tu ya mikakati yake ya kutafuta njia muafaka za kuwawezesha wananchi wa kipato cha chini na maskini.


  Rais akifafanua kwamba kunahitajika ubunifu zaidi, utaalamu na utashi wa kisiasa kutoka kwa viongozi na wananchi wenyewe katika mchakato mzima wa kuondokana na umaskini.


  Alimweleza Professa Mohamed kwamba nia yake ya kumwalika kuja nchini ililenga hasa kutaka wabadilishane mawazo, uzoefu na mbinu ambazo zitamuwezesha yeye binafsi kama Rais na wadau wengine wakiwemo watendaji serikalini, wamiliki wa mabenki, vyama vya kuweka na kukopa kwa pamoja nini kifanyike kuharakisha mchakato wa kuwaondoa wananchi katika umaskini.


  `Ninakushukuru sana profesa kwa kuukubali mwaliko wangu. Niliona ni bora tukutane na tuweze kubadilishana mawazo, lakini kubwa zaidi kuchota maarifa yako uliyotumia kuwaondolea umaskini maelfu ya wananchi wa Bangladesh na kuboresha maisha yao kwa njia ya mikopo nafuu,` alisema.


  Alisema kwamba siku zote amekuwa akiamini kwamba mabenki ya biashara si rafiki wa watu maskini, hivyo inatakiwa kuundwa mifumo rasmi nje ya mifumo ya benki za biashara ambazo licha ya kutoza riba kubwa lakini zimejaa urasimu mkubwa inapofikia suala la kuwakopesha watu wa kipato cha chini.


  Hata hivyo, Rais alisema kidogo kidogo baadhi ya benki zimeanza kuwaamini na kuwakopesha watu wa kipato cha chini kwa kuwa wameonyesha uadilifu mkubwa wa kurudisha mikopo hiyo.


  Akichangia mawazo yake ya 'nini Tanzania inaweza kufanya kuwaondolea umaskini watu wake, Profesa Mohamed alisema Tanzania ina uwezo' na kila sababu ya kuiondoa hali ya umaskini inayowakabili wananchi wake.


  Alisema tofauti na ilivyo nchini kwake Bangladeshi ambako kuna mamilioni 'ya watu maskini, kwa Tanzania' ambayo ina asilimia 39 sawa na familia milioni 2.5 tu, ina kazi nyepesi zaidi ya kuwaondolea umaskini watu hao kwa kuwa nchi inazo raslimali nyingi, serikali mathubuti na kinachotakiwa ni ubunifu tu .


  `Tanzania mnazo raslimali nyingi sana, hamna idadi kubwa ya watu maskini, kinachotakiwa ni kujipanga vizuri, kuwa wabunifu na kuamua kwa dhati kukitekeleza kile mlichoamua, na hapo mtaweza kabisa kuziondoa familia hizo milioni 2.5 katika lindi la umaskini`


  `Kila mtu ni mjasiriamali, hata ombaomba yule wa mtaani anaweza kuwa mjasiriamali, tofauti iliyopo ni kwamba wengine walipata fursa ya kujipambanua na kuwa wajasiriamali, na kundi jingine halijawezeshwa kufanya hivyo,` alisema Profesa Yunus.


  Profesa Yunus ambaye alikuwa hapa nchini kwa mwaliko maalum wa Rais Jakaya Kikwete, amemweleza Rais kwamba hakuna njia ya haraka na ya uhakika ya kuwaondoa wananchi katika umaskini kama ile ya kuwapatia fursa na uwezo wa kupata mikopo ama isiyo na riba kabisa au yenye riba ndogo sana.


  Alisema yuko tayari na wakati wowote kushirikiana kwa hali na mali katika utekelezaji wa nia hiyo.


  Akiwa nchini, pamoja na kuwa na mazungumzo na Rais, Profesa Yunus alikutana pia na kufanya mazungumzo na Waziri wa Fedha, Gavana wa Benki Kuu, wamiliki wa mabenki, asasi zisizo za kiserikali zinazojihusisha na utoaji wa mikopo midogo midogo, 'watafiti' na wataalamu wa uchumi.


  SOURCE: Nipashe
   
 13. Kitila Mkumbo

  Kitila Mkumbo Verified User

  #13
  Jun 14, 2007
  Joined: Feb 25, 2006
  Messages: 3,347
  Likes Received: 78
  Trophy Points: 145
  Inawezekana huyu bwana ana nia na uchungu, wasiwasi wangu ni kama kweli ana uwezo wa kuyakabila anayoyazungumza na kuwaza. Nafikiri hana! Na nia peke yake bila uwezo haiwezi kusaidia kumaliza umaskini, utasikitika sana lakini at the end of the day watu hatutampima kwa kiasi gani aliamia na umaskini wetu bali aliweza kupambana nao!
   
 14. Jembajemba

  Jembajemba JF-Expert Member

  #14
  Jun 14, 2007
  Joined: Feb 3, 2007
  Messages: 257
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Yule mwenzake (EL) alisema anakwenda kula hawezi kushughulikia matatizo ya wananchi wake (wanafunzi wa Ukrane)
   
 15. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #15
  Jun 14, 2007
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,484
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  Nakubaliana na Kitila. Mwungwana ni mtu wa watu. Kwa hiyo kwake kusema umaskini wetu unamnyima raha sitoshangaa. Sasa kama ni mbunifu anayeweza kuja na mikakati ya kutukwamua, hilo ndilo swali la dola milioni 64.
   
 16. Mtu wa Pwani

  Mtu wa Pwani JF-Expert Member

  #16
  Jun 14, 2007
  Joined: Dec 26, 2006
  Messages: 4,095
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 135
  Sasa jee huo ushauri aliopewa waweza kumsaidia? maana jamaa kasisitiza kujipanga ndio swala muhimu, na kinachoonekana timu ya JK haijajipanga.
   
 17. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #17
  Jun 14, 2007
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,484
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  Mtumwitu,
  Labda tumpe muda ajipange. Tunachotaka sisi ni kuona matunda ya ujipangaji huo.
   
 18. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #18
  Jun 14, 2007
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,360
  Likes Received: 6,377
  Trophy Points: 280
  Unaweza vipi kuwaondolea watu umasiki ambao hawajaelimika? Je kuwamwagia watu mabilioni ya pesa wakati hawana elimu ya usimamizi wa fedha, ubunifu wa biashara, n.k na wakatoka katika Umasikini? Wamarekani wamejaribu hayo ya kutoa pesa kwa kila aina ya mikakati ya "MKIDARUTA", "MKARABITA" na "MBUTABUTA" ili watu weusi waondokane na umaskini.. guess what? never happened! Watu weusi wanaoondokana na umasikini ni wale wanaopitia shule na kuelemika!!

  now.. that brings us back to Ukraine kids... unavijana masikini 30 wanaoomba kitu kimoja tu.. elimu! ... unasama "hatuwatambui"... halafu week moja badaye unasema "watu wangu"... hawa vijana 29 ni watu wa nani?
   
 19. M

  Mama Lao JF-Expert Member

  #19
  Jun 14, 2007
  Joined: Jan 16, 2007
  Messages: 238
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Anapanga nini miaka 12? Na hao wasaidizi wake vurugu tupu. Mh Rais might be having great ideas ila "utekelezaji" inakuwa balaa.Mfano ni zile bilioni 21..kulikuwa na longolongo kibao na inawezekana waliozipata sio walengwa.
   
 20. Mtu wa Pwani

  Mtu wa Pwani JF-Expert Member

  #20
  Jun 14, 2007
  Joined: Dec 26, 2006
  Messages: 4,095
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 135
  Mshauri Katutia Moyo Anasema Tanzania Iko Ktk Nafasi Nzuri Ya Kuuondoa Umaskini Kuliko Bangladesh Wakati Huo Alipopractice Ideas Zake.

  Mkjj

  Ama Kweli Yaani Sasa Hatuangalii Jambo Jengine Zaidi Ya Ukraine??????

  Hili Tumo Tunalifuatilia Na Hili Lisichanganywe Na Kule
   
Loading...