Kwanini Watanzania hatupendi maendeleo?

Nkerebhuke

JF-Expert Member
Nov 1, 2021
779
1,985
Kila mtu ni sehemu muhimu ya maisha yake katika nchi huru kama Tanzania. Kupiga hatua katika maisha ni kiu ya kila mmoja mwenye afya njema na akili timamu hivyo sio Jambo baya kwa mtu kuwa mfano mzuri wa kufanikiwa kupitia kipaji chake alichojaliwa na mwenyezi Mungu. Tanzania ni nchi iliyojaliwa vipaji vingi hasa vya muziki ndio maana kuna kila aina ya muziki lakini chuki, wizu, majungu, husda, uchawi na roho mbaya miongoni mwetu Watanzania vimechangia sana kuua vipaja.

Nakumbuka kwetu Kigoma miaka hiyo ya zamani kuna kijana alikuwa na kipaji Sana ila alikufa katika mazingira ambayo niyakishirikina. Kila naposoma mijadala mingi ya vijana kwa wasanii wetu inakatisha tamaa kwani imejaa chuki na majungu, kuna watu wanatamani Diamond ashuke, Alikiba ashuke sijue Konde boy mshamba hawa wote niwetu, tuwashauri wanapokesea na tuwapongeze wanapatia.

Tuangalie Diamond alitoka wapi mpaka alipofia sio mchezo, msanii toka nyumbani Linex Sunday mjeda toka kupanda treni bila nauli mpaka Dar akitokea Kigoma, Harmonaize kutoka kuwa machinga Kariakoo mpaka aliposasa. Wito wangu kwa vijana wenzangu tutumie vipaji vyetu vizuri hata kama nikuchonga vinyago kuleta mapinduzi kwenye maisha yetu badala ya kuendekeza na kukuza mijadala ya wivu na majungu kwa vijana wenzetu waliofanikiwa
 
Katika safari ya mafanikio hakikisha unayaacha yaongee yenyewe, ukiwekeza zaidi katika kupiga piga domo inakuwa kama unaringa, lazima utaongea mbovu tu.
 
Tunapenda maendeleo ila Atupendi watu walio endelea,hasa ndugu jamaa na marafiki na wengine tunao wajua
 

Similar Discussions

0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom