Kwanini watanzania hatupendi kutaja umri?

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Feb 24, 2012
5,000
9,861
Kabla ya utambuzi wa uhesabu wa muda kwa kalenda, wazee walikuwa wanatumia vipindi kutaja umri wao.kipindi cha Mvua, Nzige njaa nk, na hata majina yao yaliwakilisha vipindi au matukio. Walipokuja wakoloni baadhi ya wasomi wakawa wanaweza kujua umri kwa kalenda, na kujua miaka yao.

Uwepo wa ajira ndio kwa kiasi kikubwa ulisababisha watu kuficha umri ili kupata kazi, yaani kama ajira ikitaka mtu mdogo basi mtu hujipa miaka michache, ikitaka mtu mkubwa naye hujipa miaka mingi

Swala hili la kudanganya miaka lilifanyika kwa muda mrefu kwa lengo la kujipatia ajira ‘white collar jobs’. Lakini kwa sasa kuna swala la vyeti vya kuzaliwa ambalo linaondoa haja ya mtu kuficha umri

Je, unadhani kwa nini watanzania tumeendelea kuficha umri tukiulizwa na watu hata kwenye sherehe ya siku za kuzaliwa?
 
Inategemea anaeniuliza ni nani? Ananiuliza kwanini? Kwani kuna haja mimi nimtajie mtu random tu umri wangu. Kama hamna umuhimu wa kumtajia na akishurutisha basi nitamdanganya.

Kuna maswali ya kiwaki lazima yajibiwe kiwaki. Au mtu anakuuliza wewe kabila gani, ili iweje?
 
👏🏽👏🏽👏🏽👏🏽👏🏽👏🏽👍🏽 Ulivyoandika Mkuu utadhani uliingia kichwani mwangu.

Inategemea anaeniuliza ni nani? Ananiuliza kwanini? Kwani kuna haja mimi nimtajie mtu random tu umri wangu. Kama hamna umuhimu wa kumtajia na akishurutisha basi nitamdanganya.

Kuna maswali ya kiwaki lazima yajibiwe kiwaki. Au mtu anakuuliza wewe kabila gani, ili iweje?
 
Mimi toka miaka ile naanza mapenzi hadi leo miaka yangu haijawahi kubalika ni ile ile tu 22,mpenzi niliyemtongoza mwaka 2015 nilimwambia ni 22 na hata atakae niuliza mwaka huu nitamwambia 22 hyo hyo.
 
Kuna watu nikiwatajia umri wangu tunaweza kukosana.. unakuta upo kwenye kundi la watu wenye miaka mi 5 kukuzidi halafu mnaongea mambo ambayo watu wanaongea na age mates wao.
Kuficha umri sometimes inasaidia kunyumbulika na kujichanganya na watu wa lika tofauti tofauti.
 
Tabia ya kuficha umri inafanya hata tusijue umri wa wasanaa, wachezaji au maarufu wa nchini kwetu....wakati huo watu maarufu wa nje tunawajua hadi urefu wao
Why are we like this
 
Inategemea anaeniuliza ni nani? Ananiuliza kwanini? Kwani kuna haja mimi nimtajie mtu random tu umri wangu. Kama hamna umuhimu wa kumtajia na akishurutisha basi nitamdanganya.

Kuna maswali ya kiwaki lazima yajibiwe kiwaki. Au mtu anakuuliza wewe kabila gani, ili iweje?
Maelezo yako, ndiyo msingi wa swali la mtoa mada!

Kwanini kuna kigugumizi cha kutaja umri wako linapokuja suala la kutaja umri?

Inasaidia nini kuficha umri wako halisi?
 
Nikutajie umri uniroge?
Kabla ya utambuzi wa uhesabu wa muda kwa kalenda, wazee walikuwa wanatumia vipindi kutaja umri wao.kipindi cha Mvua, Nzige njaa nk, na hata majina yao yaliwakilisha vipindi au matukio. Walipokuja wakoloni baadhi ya wasomi wakawa wanaweza kujua umri kwa kalenda, na kujua miaka yao.

Uwepo wa ajira ndio kwa kiasi kikubwa ulisababisha watu kuficha umri ili kupata kazi, yaani kama ajira ikitaka mtu mdogo basi mtu hujipa miaka michache, ikitaka mtu mkubwa naye hujipa miaka mingi

Swala hili la kudanganya miaka lilifanyika kwa muda mrefu kwa lengo la kujipatia ajira ‘white collar jobs’. Lakini kwa sasa kuna swala la vyeti vya kuzaliwa ambalo linaondoa haja ya mtu kuficha umri

Je, unadhani kwa nini watanzania tumeendelea kuficha umri tukiulizwa na watu hata kwenye sherehe ya siku za kuzaliwa?
 
Nilipata totozi moja kali ina miaka 18 ili na mimi nisionekane muhenga nikajipunguza miaka mingine nikawapa TRA hadi nikabakia na miaka 24 tu,mwisho wa siku kuna siku niliacha kitambulisho changu ovyo akaona miaka yangu halisi akajifanya kununa sema kwa vile ulishamkolea hadi leo kaniganda kama ruba
 
Kwa hiyo mkuu na arobaini na ngapi?
 
Similar Discussions

4 Reactions
Reply
Back
Top Bottom