Analogia Malenga
JF-Expert Member
- Feb 24, 2012
- 5,000
- 9,861
Kabla ya utambuzi wa uhesabu wa muda kwa kalenda, wazee walikuwa wanatumia vipindi kutaja umri wao.kipindi cha Mvua, Nzige njaa nk, na hata majina yao yaliwakilisha vipindi au matukio. Walipokuja wakoloni baadhi ya wasomi wakawa wanaweza kujua umri kwa kalenda, na kujua miaka yao.
Uwepo wa ajira ndio kwa kiasi kikubwa ulisababisha watu kuficha umri ili kupata kazi, yaani kama ajira ikitaka mtu mdogo basi mtu hujipa miaka michache, ikitaka mtu mkubwa naye hujipa miaka mingi
Swala hili la kudanganya miaka lilifanyika kwa muda mrefu kwa lengo la kujipatia ajira ‘white collar jobs’. Lakini kwa sasa kuna swala la vyeti vya kuzaliwa ambalo linaondoa haja ya mtu kuficha umri
Je, unadhani kwa nini watanzania tumeendelea kuficha umri tukiulizwa na watu hata kwenye sherehe ya siku za kuzaliwa?