Kwanini watanzania hasa waliosomea Lugha wanashindwa kuchangamkia fursa za kazi za ualimu wa Kiswahili, Kiingereza na utafsiri wa lugha nchini Japan

Mleta mada utakuwa umefanya msaada mkubwa sana endapo utaweka link ya namna ya Ku apply hizo kazi ....na kama vp mwongozo mzima wa namna ya kuomba

Sent using Jamii Forums mobile app
mkuu tatizo hamtembelei site za ajira za nje/kimataifa pale japan baada ya lugha za kimataifa kuwa tatizo nchini mwao sasa wanakimbizana kwa kasi ili watu wao wajue lugha za kimataifa na serikali ikafadhiri mpango wa kuanzishwa kwa site ambazo zitakuwa zinatoa matangazo ya ajira na kuaajiri wageni kwa ajili ya kufundisha lugha nchini mwao mojawapo ni hii
WORK JAPAN Co., Ltd itembelee utaona
 
Nirahisi kusema kuliko, nadhan mtoa mada hajui akisemacho. izo fursa maybe kuzipata ukiwa kula ila sio ntumie pesa kusoma izo course bila kua na uwakika wa kazi, mfano hyo ieltl ina kikomo mda ukipita imeexpire, na inasomwa kwa purpose.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hawazioni kivipi mkuu
Wengi sio wapambanaji wakutafuta tarifa na michongo kama Wakenya na Wanaigeria.Hata kama Scholarship zipo awataki kuomba graduate anakaa nyumbani akisubiri kazi hili hali anaweza kuaply hata Scholarship za China tu zisiso na ushindani kama za Europe na America.
 
Mtu unaweza kuomba tatizo namna ya kufika huko yani hiyo michakato ya kupata tu passport ndani ya nchii hii utafikiri unaomba kazi full kuzungushana . Mbaka mtu unashangaa . ukweli mambo mengine ndani ya hii nchi yanachukiza kweli kweli.
 
Watanzania wengi ni Washamba tu

Ni watu wa kukariri kulingana na nature ya elimu yetu, hawana Exposure na ni waoga wa kuthubutu.

Wanajali starehe zaidi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
wakuu bado lock-down inaendelea japo kuna mwanga unaanza kuonekana baada ya hotuba ya leo ya waziri wa uchumi wa hapa switzerland bwana Guy Parmelin kuonesha matumaini ya kulegezwa kwa masharti katika phase ijayo ya kupambana na huu ugonjwa.

Turudi kwenye tafakuri ya leo kama heading inavyoeleza, walimu wa fani ya lugha wanaomaliza huko nchini kwenye vyuo vya nyumbani wanashindwa nini kuchangamkia fursa za kimataifa na ikiwa ukweli ni kwamba wana uwanja mpana wa fursa huku?

Nimekaa Japan nchi ina uhitaji mkubwa wa walimu wa kiingereza, kiswahili na watafsiri wa lugha(Interpreter/Translator) na si Japan tu hata mataifa ya karibu na japan kama china na korea kusini nako wanahitajika sana, nini hasa kinawakwamisha vijana wenzangu wahitimu wa hizi fani kuzichangamkia hizi fursa za kimataifa? Ukiwa nchini Japan unakutana na wakenya wengi wanafundisha kiswahili lakini huwezi kukutana na mbongo anafundisha kiswahili na wakati wahitimu wapo wengi wa hizi fani na pia hii ni lugha yetu toka kuzaliwa.

kwa Japan hawa watu ni kati ya watu wanaolipwa vizuri nimeshuhudia watu wa mataifa ya uganda hata kiswahili hawajui vizuri wanafanya kazi za part time za kufundisha kiswahili na wanalipwa 300,000Yen kwa mwezi, na rafiki yangu mkenya yeye alikuwa analipwa 4,500,000m Yen anafundisha kiswahili na ni mkalimali pia sisi ndio lugha yetu lakini tukamwa hata kuifundisha kimataifa pamoja na kuwa tunahitajika, tatizo ni nini?

Kwa wahitimu wa fani hii, fani yenu haina changamoto kimataifa kabisa kama walivyo wa fani za Engineering, IT &Telecomunication Engineering ama manufacture/Industrial engineering ambazo nchi zilizoendelea haziwezi kutilia maanani elimu hizi zilizotoka baadhi ya nchi za kiafrica kufanya kazi kwenye taasisi zao japo zinahitajika kwa wingi.

Hivi mnashindwa hata kusoma Certification za CELTA,TELF na TESOL/TESL au ESL kwa miezi kadhaa ili muweze kuwa wa kimataifa kidogo, British Council hawa wapo kila nchi matawi yao nadhani hata tanzania wapo, mnashindwa kusoma hizi programme kwa miezi michache then mkachangamkia fursa kimataifa? AMKENI VIJANA MSITEGEMEE SOKO LA AJIRA LA NDANI TU MNAHITAJIKA SANA HUKU DUNIANI

N:B
CELTA - Certifacte in English Language Teaching to Adult
TEFL - Teach English as a Foregn Language Certificate
TESOL - Teach English to Speaker of Other Language Certificate
TESL - Teaching English as a Second Language Certificate
ESL - English as a second language Certificate

Kati ya hizo certificate CELTA ni nzuri kwa nchi kama Japan kulingana na mahitaji yake

Parabora
Geneva - Switzerland

chukua hatua stahiki, Corona ipo na ni hatari
Una link hapo ya kuombea nafasi Japan??
 
Matatizo yetu sisi kama taifa ni makubwa mno. Mfumo wetu wa Elimu kwa namna na kiasi kikubwa hautuandai kukabiliana na changamoto za ulimwengu wa sasa. Hautuandai kushindana katika ngazi za kimataifa. Muda wetu mwingi, wengi wetu ni majungu, umbea, betting hatwendi zaidi ya hapo.
 
Katika nchi chache za Ulaya na USA nilipoishi Wakenya ndio wakalimani wa kiswahili, kuna siku nilienda mahali nikajifabya cjui English wakanipa dada mmoja wa Kikenya anitafasirie, yaani kilichokua kinasemwa na anachoniambia vilikuwa vitu tofauti. Nikamkataa then nikawaambia ukweli
 
Katika nchi chache za Ulaya na USA nilipoishi Wakenya ndio wakalimani wa kiswahili, kuna siku nilienda mahali nikajifabya cjui English wakanipa dada mmoja wa Kikenya anitafasirie, yaani kilichokua kinasemwa na anachoniambia vilikuwa vitu tofauti. Nikamkataa then nikawaambia ukweli
 
Shida sio lugha ya kiswahili,shida in lugha ya kiingereza huwezi amini hapa bongo hata MTU mwenye PhD kizungu kinamsumbua just imagine

MTU first degree stela maris university
Masters:mzumbe university
PhD:udsm
Hiyo mtu hajapata exposure yeyote kwenye lugha ya kingereza(kuishi na native speakers) hivi unazan MTU kama huyo abakubalika kimataifa au kuweza kushawishika kufundisha hicho kiswahili huko Japan amezrzika na salary yake ya 1.2ml
Kusoma hizoo course za kiingerza sio mchezo ada sio chini ya 500000 za kibongo

Wakenya na waganda kiingerza kibawabeba sana kwwnye soko la ajira,kuna mwaka Fulani nlikuwa hong Kong wakenya na waganda wamejaa mbaya na wanapata kazi za ndani n house boy sababu tu anajua kiingereza so atatoa msaada mkubw kwa mtot wake

Kuliko umuajiri mbongo mwenye degree ya kubabaisha asiyejua kingerza vizur bora umuajir mkenya au mganda aliyeishia shule ya msingi akulelee mtoto wako

Changamoto nyingine hatujui wapi pa kuanzia,yan hutujui hata hiyo passport mtu hajui anaipataje yan?

Cha mwisho kabisa ni mtaji ,ujue ukiwaza kwenda hata hapo Malaysia bila dollar 1000 unakuwa deported, hebu waza.

Passport 200000/=
Visa dollor120
Flight ticket 670
Accommodation per day50$
Health insurance 154$/3 month

Kibongo bongo sio rahisi kuyamudu hayo yote ukitarajua kuwa ndii umemaliza chuo



Sent using Jamii Forums mobile app
Mkuu PASSPORT ni 150,000/= je gharama zingine ni za kwensa nchi gani?

Pia umeongea ukweli mkuu kwenda bara jingine kutoka huku Tz, uende kupambania maisha nje nafikiri itakubidi usiwe na chini ya 2mil
 
Tuna kasumba hizi

1. Uvivu wa kusoma na kufutilia mambo mfano kwenye mitandao kuna fursa nyingi za ajira nje na free courses ila umakini na persistence ya kusoma all small details na kuapply hatuna. Kwa mfano uweke link hapo yenye page 7 tu bado mtu atauliza naomba nifanyie mchongo. Angalia hata mashirika ya kimataifa hapo Geneva watanzania ni wachache sana si kwamba hatuna elimu ila sijui elimu yetu imetulemaza hatu compete kivyetu vyetu sielewi.

2. Kuamini kuwa kila kazi ni connection: vijana wengi huamini hivi na kukata tamaa ya kusaka ajira nje

3. Fear of unknown. Yaani hujui unaogopa nini ila tunaogopa tu kwenda kufanya kazi mbali na nyumbani hatutaki mwenda nje ya comfort zone zetu.

4. Kubweteka na degree na masters zetu. Kuna course nyingi za soft skills zinazomuongezea mtu thamani mf presentation skills, team work, language etc ila tunabweteka na masters tunasahau kila mwaka thamani ya ulichosoma jana inapungua. Mfano fani ya Computer science huwezi kuwa umegraduate mwaka juzi ukasema umetosheka na programming languages za enzi zile lazima uwe unajinoa hapa na pale sasa vijana wa leo wanaringia vyeti na picha kubwa za graduation parties. Kumbuka pia interview za mashirika makubwa wana muassess mtu kwenye competencies nyingi haswa soft skills na upembuzi wake katika mambo kadha wa kadha nje ya fani yake.

5. Kutokuelekezana kwa waliofanikiwa. Mkuu nikupongeze kwa thread nzuri ila baadhi ya waliotoka na kufanikiwa hawatoi mrejesho chanya hata kuwapa moyo wadogo wajaribu. Kuna waliojaribu kufungua hadi blogs hao tunawapa sifa za jinsi ya kupata scholarships ila bado wengi wangeweza ku shed light kwa wenzao.

6. Kuogopa macho ya jamii. Katika jitihada hizi kijana anawaza dah sijui ntaonekanaje . Je nikifeli si ntachekwa na classmates wangu.

Sent using Jamii Forums mobile app
Umeongea madini tupu!! Vijana tuamke!
 
Back
Top Bottom