Kwanini Wataalam wa Afya wamekumbwa na sakata la vyeti fake na Afya ni Sekta nyeti!!

MLAU

JF-Expert Member
Aug 23, 2007
4,726
3,358
Nimepatwa na maswali kiasi kuhusiana na baadhi ya watumishi ktk Sekta ya Afya kukumbwa ktk kashfa ya vyeti fake na kuondolewa ktk utumishi wa umma.

Hii Sekta ya Afya ni moja ya Sekta nyeti sana kwasababu inashughulika na Afya ya binadamu na kuwa na mtumishi mwenye elimu ya Mashaka nayo inatia shaka ktk huduma.

Nini kimepelekea kuwa na watumishi kama hawa ktk sekta vyeti kama hizi za Afya hapa Tanzania??

Na nini kifanyike kutokuwa na watumishi kama hawa??
 
Hawa watu ni kwamba tu form four hakufanya vizuri,lakini unakuta chuo kaenda na kasoma vizuri tu ila cheti kilichompeleka huko ndo cha kufoji.Na sio kwamba kwakua hawakua na vyeti original basi hata huduma yao haikukidhi viwango,NO.
 
Hujiulizi mbona wengine wanapata division one form four halafu form six wanazungusha?cha kushangaza wenye vyeti Feki ndo majembe ya kazi
Asante umenisaidia.Ni kwamba unaeza feli form four lakini ukafika chuo ukasoma vizuri.Kuna watu tuko nao mitaani hawakufanya vizuri sana lakini wameenda vyuo vya nursing na wakafanya vizuri.
 
  • Thanks
Reactions: SDG
Hujiulizi mbona wengine wanapata division one form four halafu form six wanazungusha?cha kushangaza wenye vyeti Feki ndo majembe ya kazi
Hapa iko hivi aliyezungusha form six anakuwa kuna sehemu alizembea, ila ukumbuke ambaye alifeli bado hajui na anahitaji knowledge ya nyuma kwenda mbele.
 
Kamanda Kova alikamata watu waliokuwa wanatengeneza vyeti fake Buguruni ile kesi yao ilifika wapi??

Na RPC Kigoma alikamata waliokuwa wanatengeneza vyeti fake tena mpaka masters nao kesi yao ilifika wapi??
 
Tena hao wa afya wengi waliofoji ni ngazi ya diploma na certificate...
Kuingia ngazi ya digrii kwa kufoji sio rahis sanaaaaa....
Acha utani wewe!Kwa nini iwe vigumu?Ninamjua mtu yupo had I sasa na ni muuguzi mkuu wilaya,alianzia ajira kama muhudumu wa afya,akanunua walimu wakafanya mbinu afanyiwe mtihani wa form 4,akapata Cheti,alisoma diploma,na kisha degree pale st John.Jinsi alivyofaulu chuo kikuu ni kununua tu paper.Na kwa watoto wa kike wengi wanahonga K.Ndio maana tuna watu wa vyuo vikuu huku ni mabomu mabomu yaani hata huwezi kuniambia kitu.
Natamani sana kuwe na mitihani inatolewa kuhusu kazi wafanye wrote,naamini wapo vimeo wengi na elimu fake ya digrii ingawa vyeti wanavyo
 
Sekta ya afya ilivamiwa wakati wa utekelezaji wa mpango kabambe wa kuongeza rasilimali watu.

Vyuo vya elimu ya afya vilianza kuwa ni biashara kubwa na inayolipa.
 
Sasa form four bios upate bashite afu utudanganye chuo unaweza fanya vyema?.

Miaka michache iliyopita sifa za kusoma uuguzi na uganga ngazi ya cheti ilikuwa ni elimu ya darasa la 7 na ngazi ya diploma ilikuwa ni elimu ya sekondari bila hata kuwa na D ya biology mama mdogo alitumia hiyo fulsa mwaka 2001
 
Hapa iko hivi aliyezungusha form six anakuwa kuna sehemu alizembea, ila ukumbuke ambaye alifeli bado hajui na anahitaji knowledge ya nyuma kwenda mbele.
Elimu gani ya Tz? Kukariri, ndio hao wasomi wameifikisha Tz hapo ilipo. Mikataba yote mibovu ni wao sio wale wa darasa la 7.
 
Asante umenisaidia.Ni kwamba unaeza feli form four lakini ukafika chuo ukasoma vizuri.Kuna watu tuko nao mitaani hawakufanya vizuri sana lakini wameenda vyuo vya nursing na wakafanya vizuri.


Madesa yanawatoa.
Mfumo wa Elimu ya chuo ni tofauti na Elimu ya sekondari.

Elimu ya sekondari inahitaji mtu mwenye akili na maarifa mana kila kitu unafanya mwenyewe mpaka siku ya mtihani ndani ya chumba cha mtihani. Haitakiwa uwe unapaniki paniki hovyo.

Na pia sekondari inahitaji mtu mwenye juhudi na malengo. Mtu analenga kuwa daktari au mwalimu au askari au Engineer au mhasibu au Rubani au Mwanasiasa. Kwa hiyo kuanzia Form lll mtu anaonekana kabisa kuwa amelenga wapi.

Sasa kwa nchi zetu tunaowaita madaktari feki eti majembe tunamchukua mtu aliyefeli mwenye cheti feki tunampa nafasi ya kusomea mambo ya afya halafu mwenye akili na maarifa anakosa ile nafasi halafu mtu anasema eti ni majembe.!!!
Mi hawa watu ninawafahamu wengi kwa sababu najua uelewa wa mtu anayesoma miaka minne halafu anashindwa kupata D nne kuwa uelewa wake ni mdogo sana. Mimi hua kwa kutumia Biology niliyoisoma O- Level mpaka leo nikifikaga hospitalini naona kuwa kuna ubabaishaji mkubwa sana sana.
Na hua kuna rafiki yangu mmoja namwambiaga siku hizi hakuna madaktari ni watu waliopewa ajira kwa vimemo wamejazana tu huko.
Wasomi halali wanatolewa kwenye hospitali kubwa wanahamishiwa huko vijijini kusiko na vitendea kazi wabaishaji wanabaki mijini mana wana ndugu waliowapa ajira kwa vyeti feki na ndio wanaopanga vituo vya kazi.

Eti leo ubabaishaji na uzembe wa madaktari feki unaitwa ni utendaji bora.!!!!!
Hebu mambo mengine tumuunge mkono mh. Rais kwa sababu ndiyo mabadiliko yanakoanzia.
Huwezi kuwa na watu walionunua vyeti ili wapate mishahara mikubwa ili hali uelewa na maarifa kichwani ni mdogo.
Watu wengine witakiwa wawe wasaidizi wa waganga wa kienyeji leo hii ni madaktari feki waliofoji vyeti ili tu nao wasiachwe nyuma na madaktari halisi waliokua na maono ya kuwa madaktari tangu shule ya msingi na wakawa wanafanya juhudi kwenye masomo na wanapopata maksi za chini wanarudia na kufaulu.

Baada ya mishahara ya madaktari kuboroshwa wakati wa mkapa ndipo manesi wa darasa la saba nao walipotaka kusoma na kuwa madaktari. Hapo watu walianza kufoji vyeti ili wakasomee udaktari mana sifa ya kusoma chuo cha udaktari kwa ngazi ya digrii ni lazima form four uwe umefaulu na kuwa na credit( alama ya C na kuendelea) kwenye masomo ya Hesabu, English, Biology, Chemistry na Physics.

Wengi wa wahudumu waliokuwepo hawakuwa na Sifa za kusoma digrii. Walipoona maslahi ya madokta yameboreshwa wakatamani mishahara minono na wakaona vijana waliopiga PCB zao za halali wanakuja kuchukua idara zote wakaanza kufoji vyeti ili wapate mishahara mizuri.
Wengi wanauzoefu kazini lakini sio kwa maana ya kufoji cheti.

Matokeo yake sasa ni kuwa hao hao waliofoji vyeti wakawa madaktari na kwa savabu ya kuwa kazini muda mrefu wakawa ndio wakuu wa idara mbalimbali.

Hao madaktari feki na wakuu wa idara feki wakawa wanawaajiri watoto wao feki kuwa manesi feki. Ndio wale wanaovaa visketi vifupi na mapaja nje nje na kutukana wakina mama wanaokuja kujifungua.
Akitukana ukienda kumtolelea taarifa kwa mkuu wa idara utakuta ni hawara yake au mjomba ake mgonjwa wako atakua hatarini.
Eti hao ndio leo wanaitwa Majembe.!!!!!

Kwa haya anayofanya Mh. Rais huko mitaani anapata sifa na heshma kubwa sana kwani anarudisha hadhi ya Elimu na kusababisha watu wasome kwa juhudi na kwa malengo.

Ukikimbia umande Sekondari ujue itakula kwako tu hakuna kufoji cheti.
Ule ujanja ujanja wa kukimbilia chuo kwa kufoji vyeti na kutegemea madesa na migongo ya group assignment itapungua. Unakuta mdada amejaza notes kitabu kizima kwenye mapaja .
Na wenye mapaja makubwa kama wale manesi waliofoji vyeti ndio utakuta ni notes na Ilustrative diagrams zake zote.

Ikumbukwe kuwa sina shida au tatizo na wale wahudumu waliobaki na elimu zao za darasa la saba au form four zao za div 4 au 3 wakawa hawajafoji ili wawe madokta.
Hawa nawaheshimu sana kwani huwa wanajituma kwa uaminifu kulingana na majukumu yao yanapoishia.
Hawajafanya udanganyifu na Jamii itaendelea kuwakubali na kuwaheshimu.
 
ndiyo maana watu wengi wanaumwa UtI COZ VIPIMO HAVISOMI INAONEKANA POA KUMBE SIO POA KABISA
Kabisa na Dar siku hizi kila MTU ana UTI na kama ilivyokuwa hapo nyuma kidogo kila MTU ana Typhoid fever wakati hana.

Na wengine wengi tu kuandikuwa kuwa wana malaria baada ya kupima wakati hawana hiyo malaria
 
Back
Top Bottom