Kwanini waswahili/ watanzania hatuna herufi zetu?

hidencode

Member
Nov 8, 2018
13
9
Nimefuatilia jamii nyingi duniani zina herufi na namba zao, mfano wachina, waarabu, wakorea, wazungu

Je nini chimbuko la herufi na namba hizi? Walifanikiwa vipi walio na herufi zao?

Msaada kwa mwenye ufahamu
 
Toa mfano nikuelewe mkuu
 
Kwani wewe kila siku ukiambiwa watanzania ndio wana IQ ndogo kuliko watu wote duniani huelewi
 
Nimefuatilia jamii nyingi duniani zina herufi na namba zao, mfano wachina, waarabu, wakorea, wazungu

Je nini chimbuko la herufi na namba hizi? Walifanikiwa vipi walio na herufi zao?

Msaada kwa mwenye ufahamu
Watu wenye haerufi zao waliunda mfumo wao wa uandishi, mfano wachina wao wanatumia mfumo wa picha. Wao walitumia muoneiano wa kitu na kuchora hicho kitu na baadae ndio herufi zenyewe. Mfano

mtu 人 (ren) hapo kuna picha ya kiwiliwili na miguu

Kubwa 大 (da) hapo kuna picha ya mtu akikumbatia kitu kikubwa

Moto 火 (huo) hapo ni picha ya mti ukiungua.

Mifano mingine ni

Chini 下 (xia)

Juu 上 (shang)

Wakolea na wachina asili ya uandishi ni moja ila kutokana na tofauti kijiographia imepelekea utofauti kidogo wa maumbo ya herufi zao.
Kwa upande wa waarabu, na wazungu nao kuna mifumo yao iliyopelekea kuibuka kwa hati zao.

Waswahili huenda tungedondokea kwenye mfumo wa wachina, michoro ya mapangoni ni ushahidi tosha kuwa baada ya miaka kadhaa huenda tungekuwa na mfumo ule wa uandishi.

Kutokana na kuingia kwa wageni karne ya 13 kulipelekea kuanzishwa kwa hati tofauti tofauti mpaka sasa tunatumia zilizokuja na wageni kwasababu hatukuwa na utamaduni wa kuandika na hata kama tungeandika bado tusingeweza kushindana nao, rejea kwenye viwanda na tamaduni za waswahili wa kale.
 
Shukrani sana kwa maelezo yako mazuri, vilevile ingekua vizuri ungetupa andiko au link ya kusoma kuhusiana na tamaduni za waswahili wa kale
 
Unataka mfano gani mkuu? Siunaona wachina wanaherufi zao kama hivi 你好, za kwetu si tunatumia za kingereza ( A -- Z)

Mkuu sisi hatutumii herufi za kiingereza, na hata wao hawana herufi zao, (A-Z) ni herufi za kilatini.

Hoja ni hii kwamba uwe na herufi zako ili iwe nini??, wazungu wanasema (na hilo ni sahihi) kwamba "necessity is mother of invention". Sasa wewe unayo mahitaji gani ili leo uwe na herufi zako, mbona huna kalamu, gari, kompyuta, cherehani, simu yako uliyoigundua wewe muafrika??!!.
 
Mahitaji yapo, ukiangalia lugha zetu za asili haziandikiki kwa hizi herufi ulosema ni za kilatini

Hata na hivyo nilitaka kujua kwanini wao waweze kuwa na herufi zao na sisi tushindwe! Na sio kwamba nilihitaji kujua umuhimu wa sisi kuwa na herufi zetu
 
kuna series moja ya kikorea kuna mfalme alitaka aondokane na kutumia lugha ya kijapani enzi hizo walipokuwa wakitawaliwa na wajapani hivyo akafanya jitihada akaaznza kuunda lugha yao badaye wakafanikisha.
kwa kujibu swali lako ni kuwa kwa sisi Tanzania na Afrika kiujumla hatuna herufi zetu binafsi sababu inaonekana kabla hatujatawaliwa mababu zetu walikuwa hawana huo utaratibu wa kuandika
 
"Kwanini wao wawe na herufi zao na sisi tushindwe???"-- umeuliza swali rahisi sana, ni kwamba sisi hatukuwa na "neccesity" ya kuwa na herufi yaani maisha yetu zama hizo hayakuhitaji tuwe na maandishi, lakini wewe leo unaweza kugundua herufi na ukazitangaza ili zitumike na utapata zawadi na heshima kubwa kwani utakuwa ni Mtz wa kwanza kufanya hivyo kama si mwafrika wa kwanza.
 
Kweli kabisa, naamini kuna umuhimu wa kufanya hivyo
 
kuna series moja ya kikorea kuna mfalme alitaka aondokane na kutumia lugha ya kijapani enzi hizo walipokuwa wakitawaliwa na wajapani hivyo akafanya jitihada akaaznza kuunda lugha yao badaye wakafanikisha.
kwa kujibu swali lako ni kuwa kwa sisi Tanzania na Afrika kiujumla hatuna herufi zetu binafsi sababu inaonekana kabla hatujatawaliwa mababu zetu walikuwa hawana huo utaratibu wa kuandika
Si kweli. Labda Tanzania.

Ethiopia wanazo na nchi zingine za Kiarabu za Afrika wanatumia herufi zao.
 
Nimefuatilia jamii nyingi duniani zina herufi na namba zao, mfano wachina, waarabu, wakorea, wazungu

Je nini chimbuko la herufi na namba hizi? Walifanikiwa vipi walio na herufi zao?

Msaada kwa mwenye ufahamu
Jibu ni kuwa, jamii yoyote isiyo na maandishi yake (own alphabet) ni ishara kuwa walikuwa hawajui kusoma au kuandika mpaka WAKOLONI walipowaletea ELIMU. Sisi babu zetu walichora picha tu mapangoni.
 
kuna series moja ya kikorea kuna mfalme alitaka aondokane na kutumia lugha ya kijapani enzi hizo walipokuwa wakitawaliwa na wajapani hivyo akafanya jitihada akaaznza kuunda lugha yao badaye wakafanikisha.
kwa kujibu swali lako ni kuwa kwa sisi Tanzania na Afrika kiujumla hatuna herufi zetu binafsi sababu inaonekana kabla hatujatawaliwa mababu zetu walikuwa hawana huo utaratibu wa kuandika
HIDDEN ROOTS
 
Askari_makumbusho_matini_Kiswahili_-_Kiarabu.png
 
Attachments

  • Askari_makumbusho_matini_Kiswahili_-_Kilatini.png
    Askari_makumbusho_matini_Kiswahili_-_Kilatini.png
    318.4 KB · Views: 36
Back
Top Bottom