Kwanini waswahili hatupendi kuambiwa ukweli?

Sham777

JF-Expert Member
Aug 1, 2019
334
836
Nilicho gundua watu wengi ili urafiki, undugu, mahusiano yadumu kuna mambo hutakiwi kuyaongea hasa yanayo husiana na ukweli. Mfano ukimwambia mpenzi wako Umenenepa umepoteza mwonekano wako mzuri basi itakuwa ugomvi usio isha hata kama lengo lako lilikuwa ni zuri.

Nimeshuhudia ugomvi baada ya kijana mmoja kuambiwa ukweli ambao ungemsaidia katika maisha yake yote sio yeye tu bali na familia yake.. Kuna kijiwe chetu cha Bodaboda huwa tunapiga sana story hivyo hata watu ambao sio bodaboda wanapenda kushinda pale. kuna kijana Mmoja anaitwa Kidume ni bodaboda na ameoa na anawatoto watano. Jina la kidume ni jina la utani kutokana ana watoto wengi. Kudume anapenda utani kutania wenzake kuwa hata wakifa hawata acha chata kutokana wengi wao ndio kwanza wanaanza maisha na hawana familia wala watoto..

Juzi kuna kijana mpya alikuwa amekuja kijiweni kupiga stori mbili tatu, kama kawaida Kidume kuonesha umwamba akamuuliza vip kijana umeoa kijana akajibu bado, Anaendelea vip una mtoto, kijana akajibu bado sina nimemaliza chuo juzi tu ndio nimekuja anza maisha mtaani. Kijana pia akamuuliza kidume vip wew unawatoto kidume kama kawaida yake akajibu ndio akataja na idadi. Kijana akauliza tena kutokana na kazi ina risk je Una bima ya afya endapo likatokea la kutokea (ajari), Kidume akasema Sina. Kijana akamuuliza swali jingine ambalo lilileta ugomvi je ikatokea umekata Moto (kufa) Je Familia yako ina weza kuishi bila shida kwa muda gani?.

kulingana na saving acc yako? Kidume sura ilibadilika akajibu kwa kupaniki hata mwaka mzima wanaishi. Kijana akawambia Umeniambia Una watoto watano kwanini unafanya saving ya hela badala ya hiyo hela kufungua mradi na uwafundishe wanafamilia ili endapo ikatokea la kutokea waendeleze huo mradi/miradi iyo hela badala ya kula mwaka wale miaka yote watakayo kuwepo, Kidume alikuwa mkali na anamwambia kijana kuwa anamchulia maisha yake kwasabab kijana anaongelea mambo ya kufa kufa..

NB:
Kwanini tusikubali ukweli/ Fact na tuutumie in positive way pale tunapo ambiwa. Tumeona wengi wasio penda kuambiwa ukweli mwisho wake unavyo kuwa. Tuwe na tabia za kukubali tusiwaone maadaui watu wanao tuambia ukweli..
pia mnisamehe mimi sio mwandishi mzuri nimeona nishee tu na nyie hili jambo
 
Kutokujiamini, na kutotaka kuukubali uhalisia wa mambo hasa unachoamini na kujisifu kukifanya kwa ustadi, kinapoonekana kuwa na walakini. Haya mambo yako katika kila nyanja ya maisha yetu, maeneo ya kazi, biashara, dini na hata siasa (mfano awamu ya tano)
 
Hata Lisu alipoambiwa ukweli kwamba anasaliti nchi kwa kututisha tutashitakiwa MIGA alichukia sana.
 
Back
Top Bottom