Kwanini wasomi wengi wametekwa na michezo na kusahau mambo ya muhimu? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kwanini wasomi wengi wametekwa na michezo na kusahau mambo ya muhimu?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Gurti, Mar 24, 2011.

 1. G

  Gurti JF-Expert Member

  #1
  Mar 24, 2011
  Joined: Nov 19, 2010
  Messages: 211
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Ndugu zangu wa jf,

  Mimi huwa ninafuatilia sana uelewa watu kuhusu mambo ya msingi ya nchi hii. Kila mara kunapokuwa na mambo muhimu kwenye media asubuhi kwenye vituo vya magazeti, ktk daladala na maofisini ikiwepo ofisini kwetu mjadala unaoongoza bado ni wa michezo. Ninajitahidi kuanzisha mijadala iliyoko uk wa mbele wa gazeti - hawataki- Ni michezo tu. Hata kukiwa na hotuba za rais, Dowans, katiba mpya au uchaguzi bado watu wanajadili michezo kupita kiasi. Mimi inanisumbua sana. Mimi ni mshabiki wa Man U na Simba lakini michezo haipaswi kuwa zaidi ya katiba mpya na downs au siasa kwa ujumla. Kwanini wasomi hawabalance?

  Hivi karibuni nimeanza kufuatilia nyendo za great thinkers wa Jamii forums, mwendo ni ule ule. Ninapaandika makala hii, wafuatiliaji wa michezo magazetini ktk jf ni karibu 8000 wakati mambo ya downs na katiba mpya na mengine muhimu yahusuyo nchi wanacheza kati ya 0 hadi 250. Hii maana yake ni nini huko tuendako?

  Watu wengi hatujui kuwa siasa ndo inaamua kama sisi tuangalie/tufuatilie michezo kwa amani au tusiangalie kabisa kukitokea vurugu. Tunasahau kuwa hata soka yetu inauawa sana na wanasiasa. Kwa hiyo, kwa kuwa ninapenda sana michezo lazima nipende sana siasa na nifuatilie sana nyendo za siasa aka katiba mpya, uchaguzi, downs, mijadala bungeni ili sote tujue hatima ya upenzi wetu katika michezo pamoja na maeneo mengine katika maisha kama uchumi, afya nk.

  wakubwa nawasilisha.
   
 2. kweleakwelea

  kweleakwelea JF-Expert Member

  #2
  Mar 24, 2011
  Joined: Nov 29, 2010
  Messages: 2,419
  Likes Received: 435
  Trophy Points: 180
  hii nayo inabidi ipelekwe kule kwenye jukwaa la michezo waione!
   
 3. G

  Gurti JF-Expert Member

  #3
  Mar 24, 2011
  Joined: Nov 19, 2010
  Messages: 211
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Ahsante sana hoja nitaifanyia kazi
   
 4. S

  Smarty JF-Expert Member

  #4
  Mar 24, 2011
  Joined: Feb 25, 2011
  Messages: 729
  Likes Received: 149
  Trophy Points: 60
  Mi naona watu hawafuatilii sana kwa sababu wanasiasa wa Tanzania wako after their stomach and families. Kwa mfano zamani ubunge ulikuwa wito na watu walikuwa wanalipwa posho tu. leo hii ubunge ni ajira ambayo haisomewi na wala huitaji kuwa profecional. sasa mkuu hapo kuna siasa au usanii? kama mtu ana doctrate anashindwa kufanyia kazi profecional yake anakimbilia kwenye siasa hapo inakuwaje? ndo maana watu wameamua kujikita kwenye michezo na burudani nyingize ili kuondoa frustration za ugum wa maish maana ukufuatilia sana siasa unaweza kuchanganyikiwa bure
   
Loading...