Kwanini wasomaji wengi wa Magazeti Tanzania wanazingatia habari za michezo pekee?

ZINDAGI

JF-Expert Member
Dec 5, 2015
1,117
1,424
Nipo sehemu nimekaa kuna idadi kubwa kidogo ya watu, nilichokigundua ni kwamba asilimia 98 wanaosoma magazeti wanapitia habari za michezo na burudani.

Hili linanipa maswali kidogo kwa nini ipo hivi?

Je, hii inawezekana watu wamepoteza focus katika mambo mengine, au magazeti hayana tashwishi kwa wasomaji kuhusu habari zingine?

Mwenye mawazo mengine please?
 
Ndio kitu cha kweli zaidi.
Ukisoma habari za siasa, uchumi n.k utaona mengi ni uongo wa kusifu upande fulani,lakini michezo ni kitu cha kweli na kinatugusa bila kupika pika mambo
 
MAMBO KIDIGITALI SIKU HIZI, HABARI ZA FRONT PAGE SIKU HIZI TUNAZIPATA KUPITIA MTANDAONI lakini hata za michezo pia

Idadi ya wasomaji magazeti inapungua, kwanza gazeti lenyewe siku hizi unaweza kulinunua mtandaoni ukalisoma lote kurasa zote

Pengine wameona habari za michezo zinawapa ahueni maana siku hizi siasa ikitoka hii inakuja hii hujakaa sawa ile, yaani vurugu vurugu mpaka unachoka

mfano: chanjo, bunge, gwajima, korosho, nida, mbowe,....n.k
 
Sababu zipo nyingi.
1.Magazeti mengi ya siasa kuripoti bila kufanya uchambuzi/kuingia kwa undani,bado yanaripoti kama vile tuko miaka ya mwanzoni mwa 2000 ambako hakukuwa na Facebook wala Instagram mf.gazeti linaandika mtu asiyejulikana ameua Polisi 3 bila maelezo ya ziada wao wanategemea vyanzo kutoka vyombo rasmi na hivyo vyombo rasmi vinaweza kutokutoa maelezo ya kina ya tukio au wakatoa kwa uchache,wakati mtandaoni wameandika jina la huyo mtu,anapoishi,kazi yake,sababu za kuua,picha mbali mbali za huyo mtu,wanaweka hadi video nk. Na hiyo habari unaipata muda huo huo wakati tukio linafanyika,habari kama hiyo gazeti linatoa kesho yake.Jiulize nani atanunua gazeti la namna hiyo.Tofauti na habari za michezo magazeti ya michezo yanafanya uchambuzi mfano juzi Yanga ilivyofungwa na Kelvin Kapumbu magazeti ya michezo hayakuandika habari za Kapumbu kuifunga Yanga bali yalichambua na kuandika kwa kina tamasha lilivyokuwa na jinsi mchezo ulivyochezwa habari ambazo huzipati mtandaoni.

2.Magazeti mengi ya Siasa yanaandika habari za kujipendekeza Serikalini, na hili lilianza wakati wa awamu ya tano.Hiyo pia ni sababu ya kukosa wasomaji.

3.Magazeti ya siasa kubanwa sana na sheria,kanuni nk.Na kwa sababu yenyewe yanaandika habari zinazoweza kuleta athari kwa wanasiasa/watawala na ni rahisi kuyadhibiti kwahiyo yanalazimika kuandika habari nyepesi nyepesi ambazo hazina mvuto tofauti na magazeti ya michezo ambayo habari zao hazina athari kwa watawala.

4.Wananchi kukata tamaa na habari za siasa/watawala,wanaona mambo ni yaleyale wanaongopewa kila siku mara uchumi umekua wakati wao mifukoni hakuna kitu.Wanaamua kusoma habari za michezo au kujihusisha zaidi na michezo ambako kunawapa faraja kwa kiasi fulani.
 
Nipo sehemu nimekaa kuna idadi kubwa kidogo ya watu, nilichokigundua ni kwamba asilimia 98 wanaosoma magazeti wanapitia habari za michezo na burudani.

Hili linanipa maswali kidogo kwa nini ipo hivi?

Je, hii inawezekana watu wamepoteza focus katika mambo mengine, au magazeti hayana tashwishi kwa wasomaji kuhusu habari zingine?

Mwenye mawazo mengine please?
Kuna shida kidogo kwenye utafiti wako,labda uliweke wazi hapa nikuelewe. Utafiti wako ulizingatia mazingira wanapotoka hao wasomaji? umri? jinsi? hali zao za elimu n.k?
 
Good umejibu vema
Huu ndio naweza kuuita ugreat thinker
 
Nipo sehemu nimekaa kuna idadi kubwa kidogo ya watu, nilichokigundua ni kwamba asilimia 98 wanaosoma magazeti wanapitia habari za michezo na burudani.

Hili linanipa maswali kidogo kwa nini ipo hivi?

Je, hii inawezekana watu wamepoteza focus katika mambo mengine, au magazeti hayana tashwishi kwa wasomaji kuhusu habari zingine?

Mwenye mawazo mengine please?
Wa TZ wazee wa..CONNECTION..

Hakuna Gazeti linaloandika habari za kisiasa,kiuchumi kwa uweledi sana hapa nchini,lakini pia Watanzania tuna kasumba fulani kuwa hili jambo ni la watu fulani sisi/mimi halinihusu(ndiyo maana kila uchwao bei ya mafuta,sukari inapanda wala huwasikii wakisema lolote wanaamini wapo watakaowapazia sauti)..

Bado tuna safari ndefu..
 
Nipo sehemu nimekaa kuna idadi kubwa kidogo ya watu, nilichokigundua ni kwamba asilimia 98 wanaosoma magazeti wanapitia habari za michezo na burudani.

Hili linanipa maswali kidogo kwa nini ipo hivi?

Je, hii inawezekana watu wamepoteza focus katika mambo mengine, au magazeti hayana tashwishi kwa wasomaji kuhusu habari zingine?

Mwenye mawazo mengine please?
Binafsi izo za michezo huwa sisomi hata heading. Afu magazeti siku hizi Kuna mtu ananunua kweli jamani.wameingia digital media.
Pia habari ujanja ujanja Sana. Kuna video ya Ile Hamza wadada wamerekodi wakiwa ghorofani Mara ghafula naiona kwa shigongo amepiga mhuri wake.

Binafsi ubongo wa binadamu unapenda raha aka pleasure kuliko Mambo ya maana. Na ndo Mana ni rahisi kunywa soda kuliko kutafuna tangawizi mbichi.
Ni rahisi mwili unapenda kupumzika kuliko kufanya kazi.
Ni rahisi kufungua mtandao wa kijamii kuliko kufungua kurasa za kukufundisha kitu ama skills Fulani.

Ni rahisi Sana kupiga umbeya na kuangalia tv kuliko kuupa mazoezi mwili wako. Tena na ubongo unatafuta reasons za kwa Nini umefanya hayo maamuzi.
Ni rahisi Sana kutaka sex bila kujua outcome ya sex ni Nini.

Ni rahisi kuangalia mafanikio ya mtu kuliko kuyatafuta ya kwako Mana ubongo tuliopewa sio rafiki kwetu kwa maisha ya Sasa ivi.
Ubongo wetu unaogopa Sana kesho ambayo haijulikani na ndo Mana ni rahisi Sana mtu kusoma ili aajiriwe Mana atakuwa na uhakika wa kipato chakula na kuishi kuliko kufanya biashara yake mwenyewe ambayo inaweza ikamfanya akawa millionaire in dolawise.
So ubongo unapenda nyeupe ama nyeusi basi sometime between haupendi.
Unataka kujua Kama ni 0% ama ni 100% Ila something in between hautaki.
Na huku in reality life haliko ivyo kabisa.
 
Back
Top Bottom