Kwanini wasimamizi wa mitihani hawavai "NAME TAGS" kama askari/watumishi wa banks? Do the candidates need to comment on misbehaving invigilators?

Infantry Soldier

JF-Expert Member
Feb 18, 2012
12,075
2,000
Shikamooni wakubwa zangu wote wa humu Jamiiforums. Mimi mdogo wenu (Last Born) Infantry Soldier nipo mzima kabisa wa afya. Thanks to God the Almighty. Eti ndugu zangu watanzania;

Kwanini wasimamizi wa mitihani hawavai "NAME TAGS" kama askari/watumishi wa banks? Do the candidates need to comment/report on misbehaving invigilators? Kwanini wasiweke pia suggestions box kwa wanafunzi kutoa dukuduku zao?

Nimeamua kuuliza hivi kwa maana kwamba leo nikiwa maeneo fulani wilaya ya Temeke nilikutana na rafiki yangu wa muda mrefu sana ambaye yeye pia ni miongoni mwa wasimamizi wa mitihani ya kidato cha sita.

Kwa kuwa tulikuwa hatujaonana kitambo, ilibidi ule muda wa lunch kabla ya wanafunzi kuanza kufanya mtihani wa pili nionane naye walau tusalimiane naye kwa dakila tatu tu.

Kweli, nilifanikiwa kuonana na jamaa tukapiga story kidogo ila nili notice kitu kimoja kutokana na macho pamoja na harufu iliyokuwa inatoka kinywani mwake. Jamaa alikuja amezimua kidogo kama sio K-Vant basi ile ni Valeur.

Sasa baada ya kuachana naye nikawa ninajiuliza, huyu jamaa anazimua alcohol muda huu wa kazi muhimu kama hii, anawezaje kufanya kazi yake kwa ufanisi?

Kwanini mifumo yetu ya usimamizi wa mitihani usibadilike na kuwapa wanafunzi/watahiniwa nafasi ya kutoa maoni yao juu ya hali nzima ya zoezi la usimamizi pamoja na tabia/mienendo ya wasimamizi wenyewe?

KUWA MZALENDO IPENDE TANZANIA. USTAWI WA NCHI YETU UNZAANZA NA WEWE. TIMIZA WAJIBU WAKO IPASAVYO.
 

Ncha Kali

JF-Expert Member
Sep 19, 2019
7,134
2,000
Mwanafunzi hana namna ya kuripoti, haruhusiwi kutumia simu... hata ikibidi kuripoti basi ataongea direct kwa ‘msaidizi’ wa karibu kwa kidole bila kujali name tags!

Like, yule msimamizi wa somo fulani kaingia amelewa.
 

jaranono

JF-Expert Member
Jun 24, 2015
1,655
2,000
Wewe ulitimiza wajibu wako wa kumpa ushauri wa namna bora ya kufanya kazi yake? Kama hukuongea nae hilo binfsi nashindwa kukutofautisha na mnafiki!!
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom