Kwanini wapinzani wanapenda kutumia media za nje kuzungumzia mambo yetu ‘ya ndani’?

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
86,428
147,123
Sasa imekuwa kama imehalalishwa vile kwa viongozi wa upinzani kuvikacha vyombo vya habari vya ndani na kukimbilia media za nje na za washindani wetu wa kiuchumi.

Alianza Zitto na zile fedha za kusaidia elimu ya watoto wa kike lakini kwa bahati nzuri WB wakamshushua na kumpuuza. Zitto aliitumia BBC badala ya media za ndani.

Sasa Tundu Lissu naye anayarudia makosa yaleyale, hivi kwanini mnakwepa media zetu?

Inakera sana.

Maendeleo hayana vyama!
 
johnthebaptist,

Umeamua kupost hii ili kutusanifu au unamaanisha kweli?

Media gani Mkubwa ya ndani iliyo na guts za kumwendea Tundu Lissu na kufanya naye mahojiano kuelezea SERA na MIPANGO yake kama akiwa Rais?

Ni mwandishi gani wa "Tanzania ya Magufuli " wa TV ama Redio anaweza kuwa "hajipendi" amuulize Tundu Lissu maswali kama aliyoulizwa na KTN na Majibu take kisha chombo chake na yeye mwenyewe visiweze kula "ban" kwa "uchochezi?"
 
Wanataka attention ya mataifa ya nje...na wengi nje hawajui ukweli wa kinachoendelea Tanzania.
 
Anachofanya Tundu Lissu ndio kinamuondolea credit kwa mashabiki wake, anawatumia watu ambao wapo against Magufuli regime akiamini watasaidia kuleta impact ndani hiyo ni very wrong strategy, haitomsaidia kuwa urais anapoteza muda.


NB:Lissu ataondoka, Magu ataondoka, uchaguzi zitaisha Tanzania itaendelea kuwepo, ila kumbukumbu zitabaki.

TUIPENDE NCHI YETU.
 
Anachofanya lisu ndio kinamuondolea credit kwa mashabiki wake, anawatumia watu ambao wapo against magufuli regime akiamini watasaidia kuleta impact ndani hiyo ni very wrong strategy, haitomsaidia kuwa urais anapoteza muda.


NB:lisu ataondoka, magu ataondoka, uchaguzi zitaisha tanzania itaendelea kuwepo, hila kumbukumbu zitabaki.TUIPENDE NCHI YETU.
Nimekuelewa bwashee!
 
Back
Top Bottom