Elius W Ndabila
JF-Expert Member
- Jul 17, 2019
- 322
- 645
Nimesoma maandiko mengi ya wadau wa vyama vya siasa na wafuasi wao bada ya CHADEMA NA ACT Wazalendo kujiondoa kwenye uchaguzi unaofanyika tr 24 ya mwezi huu. Hoja nyingi nilizosoma wengi wameandika CCM imejichimbia kaburi.
Nimesoma Twitter ya Jussa pia nimeona amenukuu hivyo hivyo kuwa CCM wamejichimbia kaburi. Msingi wa nukuu zao ni kuwa CCM inahusishwa na majina ya wagombea hao kuenguliwa kwenye mchakato kwa kukosa sifa zilizoainishwa kwenye kanuni za uchaguzi.
Nimejiuliza, kama lengo la upinzani ni kuhakikisha kuwa CCM inaondolewa madarakani, sasa hofu ni ya ni ya nini kwao kwa CCM kujichimbia kaburi? Ni nini kinawatisha kwa CCM kujichimbia kaburi? Wanataka CCM isijichimbie kaburi na iendelee kuwa imara kwa mapenzi yapi kwao?
With a simple arguent, nimetambua kuwa CCM haijichimbii kaburi bali huenda inazidi kukita mizizi yake chini zaidi. Nimekuja na assumptions hizo kwa kuwa ninatambua upinzani hawawezi kuishauri CCM kuendelea kusalia madarakani, labda iwe ni hatua ya juu zaidi ya udhaifu wa Upinzani. Upinzani imara unapaswa kuchekelea CCM inapokufa na siyo kuishauri kuokoka kwenye kifo.