Kwanini wapenzi na mashabiki wengi wa CHADEMA hawamuamini tena Zitto Kabwe?

Mwita wacha jazba Great Thinkers hawawi limited kwenye kuchambua ishu, kama CDM na wafuasi wake hawamuamini Zitto na bado ni kiongozi wao basi something is a miss hapo na huenda Zitto haiamini CDM pia so ni uhusiano wa kulindana mkuu yaani huko CDM ni Waarabu wa Pemba! Ha! Ha! Ha!
 
Mbowe, Dr Slaa na Zitto wamekifanya chama cha CDM kuwa maarufu kuliko wao wenyewe, na chama bado muasisi wake yupo na ana sauti kwenye chama kama Mwl Nyerere alivyokuwa na sauti kwenye CCM. Ni kweli hata mie nilikuwa naamini Zitto angekuja kuwa rais wa nchi hii kama angecheza siasa zake vizuri.

Zitto anaamini kuwa vijana wote bila kujali itikadi ya vyama vyao wakiungana wanaweza kulikomboa Taifa hili, na ndiyo maana hutumia muda mwingi kuwasupport vijana wenzake kuwainua kisiasa pasipo kujali wanatoka chama chake. Ukufuatilia kauli na hotuba zake huwasifia sana vijana mfano Serukamba, January, Nape n.k Mie siwezi kushanga kesho akimusupport Nape au Makamba mtoto na kumtekeleza mgombea wa CDM. Wakina Kafulila, Mkosamali na Machali ni mfano wa watu alio wasupport na kuwatekeleza wagombea wa CDM. Vijana hawa kesho wanapofanya ndivyo sivyo kama Wabunge hawa wa NCCR ambao wanaendeleza malumbano wenyewe kwa wenyewe badala ya kuwatumikia wananchi , kauli za Serukamba juu ya posho n.k wanamwangusha Zitto .

Binafsi nadhani siasa za namna hii zinamwangamiza kisiasa katika kipindi hiki ambacho CDM inaungwa mkono na watanzania wengi. Ni wazi wapo wabunge wa CDM wamepata ubunge kwa sababu ya kukubalika CDM kuliko wao wenyewe.
 
Zitto kawa mbinafsi sana,mi sasa hiv nakuambia nipo jimbon kwake,kigoma kask_kata ya mkigo,mi tena nakuambia kigoma kask kama atasimama kijana sio wazee,kupambana na zitto,safar ya siasa itaisha.mkitaka habar za kgm kask mniulize tu


Kaka/dada sijakusoma unamaaanisha nini vile, au macho yangu!!!!! kama sentensi zako hazieleweki.
 
Kama nakumbuka vizuri wakati wa maandamano ya Ars Zitto alikuwa India kwa ajili ya matibabu, na CDM walipoenda ikulu kwa ajili ya swala la katiba yeye alikuwa safarini nje ya nchi.
Pamoja na hayo, Zitto haburuzwi kwenye maswala ya kijinga, yeye sio 'ndio mzee', anajua anachokifanya

Mwanasiasa mahiri ni yule mwenye uwezo wa kuwashawishi wenzake wakubaliane na mawazo yake, ili katika utekelezaji muwe wote. Huwezi kuwa katika chama, tena ukawa kiongozi kama alivyo Zito, halafu walio wengi wanaamua, wewe ukaendelea kuwa na msimamo wako binafsi. Ukiwa kiongozi ni lazima usimamie maamuzi ya vikao siyo maamuzi yako binafsi. Kama Zito anang'ang'ania matakwa yake ambayo ni kinyume na maamuzi ya vikao, basi hastahili kuwa kiongozi.
 
Mtazunguka na maneno mengi..,ni kweli zito watu wengi wazee kwa vijana wameshapoteza imani naye. Sababu kubwa ni moja tu nayo ni kuwa zito alipendwa na watu wa lika zote kwa kutetea nchi na wananchi kwa dhati kbs.,baada ya muda zito akageuka kuwa rafiki na mtetezi wa aliokuwa akiwapinga kwa maovu yao kwa nchini na watu. Japo anajaribu kujiweka kwenye kivuli kuwa bado anatetea wananchi...watu wanaona mienendo yake na anachojifanya kutetea haviendani. Hiyo ndio sababu kubwa.


Kuhusu mtazamo wangu.

Zito ameingizwa chaka bila kujijua..,alidhani au bado anadhani urafiki wake na watu wa CCM ni kwa manufaa yake.Nionavyo mie ni kuwa CCM ilitafuta njia ya kummaliza zito maana asingepoteza umaarufu ilikua hatari kwa CCM. Walimu-win kwa kumsogeza awe rafiki wa CCM kwa kumkosha kama wana-mu appriciate sana hivi...rafiki yangu mmoja aliwahi kunidokeza dini pia ilitumika kumshawishi zito ili ainge kwenye mtego huo. Mtego umenasa..shv hana marafiki CDM bali anao wengi CCM..Je jiulize hajamalizwa bado?na je ulishawahi ona mtu anatoka chama cha upinzani na kuingia chama tawala bila kuanzia chama hicho tawala na kufikia level kubwa ya uongozi wa chama tawala..time will tell...wait,zito anakila sababu ya kujilaumu kwa kujichanganya kapoteza CV yake nzuri ambayo alianza kuijenga ambayo ingempelekea hadi hata kuwa rais wa nchi hii..mazingira ya zito sasa yanamtoa kuaminiwa tena na wananchi wengi kama iliyokuwa mwanzo. Have a look..January ambaye kwa muono wangu amepewa jukumu la kuwa karibu na zito sana siku hizi kama rafiki hv...Japo inaonekana na inasemwa sana mitaani na humu JF juu ya undumila kuwili wa makambaz family,kwa mfano alikuwa msaidizi wa JK baadae ikasomeka anapingana na JK na hata mwanae Riz1. Kwa kigezo hicho nashawishika kuona kuwa Zito anamalizwa kiaina pia na urafiki huu wa kasi na kisiasa kati yake na january sijui ulikuwa wapi zamani najiuliza pia?? utaona trend shv january popularty yake inakua lkn zito inashuka ndio maana hata watu wameanza kuweka post za kuhoji humu JF. Hamuoni kuwa mtego umenasa na zito kamalizwa kisiasa hapo????? sijui lkn ni muono wangu tuu katika intelegensia za mambo ya siasa.

zitto kama binadamu ana mapungufu yake sawa lakini kuna kundi la watu "maalum" waliowekwa kumuharibia! kuna hot issues ambazo zitto amezisimamia hao mnaowaamini wameshindwa.mfano hai ni issue ya posho,amesimamia alichoamini. kuna wengine wanasingiza ohh pesa zinawekwa moja kwa moja kwenye akaunti za wabunge, wanataka kutuaminisha kuwa zitto hana hiyo akaunti?zitto ameibua mijadala mingi pale bungeni na kwingineko ambayo imeleta tija kwa taifa hili.so mpeni heshima yake!
 
Ujue pro-Chadema wengi ni mateka wa Mbowe, sasa wanauona Zitto ni tishio kwa boss wao..

Kuanzia kipindi kile Zitto kutaka kugombea uenyekiti wa Chadema, ndio chuki ilianzia apo!

hivi wewe unawashwa au
 
Tukiachana na chuki za udini na ukanda kuna wakati msimamo wa mtu unaonekana ukibaki palepale au ukibadilika ni jambo rahisi sana kulijua

Hahitaji mwenyewe kukanusha au kukubali,wakati utaamua
 
Nachukia sana ufisadi na mafisadi wote. Nilikuwa nampenda sana rais wetu lakini baada ya kuonakashindwa kuwadhibiti mafisadi kweli nilikaa nikasema Tanzania hatuna rais. Rais anamwambia mwizi aliekapua mabilioni ya raia wako waliokuweka madarakani kuwa. Rudisheni pesa halafu kesi hakuna tena kwa kuwabembeleza na wengine hawakurudisha mpaka leo. Kweli utasema Tanzania kuna rais na kuna mahakama kuna serikali ya haki. Mie nimeiba kuku wakanikamata nikakubali kumrudisha hata ivyo selo nitalala na kipigo juu na kifungo. Kuhusu Zitto anakitu kimoja anapenda apendwe na kila upande hataki kuwaudhi ccm na chadema katika mambo yote ya maandamano, kunyanyaswa kwa chadema sijawai hata siku moja nikimsikia Zitto akiilaumu serikali na kuna kipindi anapinga hata maandamano ya chama chake. Sasa kama uwezi hata kumsema Mwema anavyowaonea kwa kumwogopa rais hapo utakuwa unawateteaje walalahoi wanakuamini? Tunampenda Zitto lakini masuala mengine yuko upande wa ccm sana inatakiwa awe mkweli asiogope kuwa atawekwa ndani au atawekwa kwenye hizo tume za bunge. Ukiwa mkweli utaongea tu hata wakikuziba mdomo. Awe mstari wa mbele katika chama chake asiwe na mawazo au tamaa ya kutaka makubwa muda wake bado ikifika atapata tu.
 
zitto kama binadamu ana mapungufu yake sawa lakini kuna kundi la watu "maalum" waliowekwa kumuharibia! kuna hot issues ambazo zitto amezisimamia hao mnaowaamini wameshindwa.mfano hai ni issue ya posho,amesimamia alichoamini. kuna wengine wanasingiza ohh pesa zinawekwa moja kwa moja kwenye akaunti za wabunge, wanataka kutuaminisha kuwa zitto hana hiyo akaunti?zitto ameibua mijadala mingi pale bungeni na kwingineko ambayo imeleta tija kwa taifa hili.so mpeni heshima yake!
Hakuna watu wanaomharibia Zitto anajiharibia mwenyewe umeona leo kahusishwa na yanayoendelea NCCR, tunaposema si kwamba tunamonea.
 
1. Aligeuka kuunga mkono Dowans/ Richmond ghafla kama ilivyotajwa.
2. Aliungana na Kafulila dhidi ya uongozi.
3. Aliamini ana umaarufu kuliko chama
4. Alikuwa na mazungumzo ya mara kwa mara na Mkurugenzi wa usalama wa Taifa na kuibua maswali.
5. Alijenga urafiki wa Ghafla na R.A
Baada ya hayo hapo juu kuaminika bila ufafanuzi wa kutosha ni vigumu,
 
Hakuna siri ktk UTANDAWAZI,, kuhusu Zitto ni kwamba aliteuriwa kuwa mwnykt wa kamati ya madini akaenda na wenzake kwenye migodi ya Buzwagi na Bulyanhulu huko Synyng wakagawana kazi yeye kaenda peke yake Buzwagi mgodi ulio na matatizo ya ufisadi hatimaye wakamtuliza kwa kumpa rushwa. Inaaminika alipewa KOLEO LA DHAHABU hii ni DHAHAMA make ni thamani kubwa ya mabilioni ya fedha. hatimaye akapunguza ukali dhidi ya ufisadi na mafisadi. Ndo kipindi hicho alianza kuwa na migogoro na viongozi wa CHADEMA na akawa anampongeza rais kwa kila alichofanya. Watu walijua habari hizi na ndiyo maana wakapoteza imani naye. Naomba tuwe wawazi tuache unafiki hili ni taifa letu wenyewe.........
 
Hakuna siri ktk UTANDAWAZI,, kuhusu Zitto ni kwamba aliteuriwa kuwa mwnykt wa kamati ya madini akaenda na wenzake kwenye migodi ya Buzwagi na Bulyanhulu huko Synyng wakagawana kazi yeye kaenda peke yake Buzwagi mgodi ulio na matatizo ya ufisadi hatimaye wakamtuliza kwa kumpa rushwa. Inaaminika alipewa KOLEO LA DHAHABU hii ni DHAHAMA make ni thamani kubwa ya mabilioni ya fedha. hatimaye akapunguza ukali dhidi ya ufisadi na mafisadi. Ndo kipindi hicho alianza kuwa na migogoro na viongozi wa CHADEMA na akawa anampongeza rais kwa kila alichofanya. Watu walijua habari hizi na ndiyo maana wakapoteza imani naye. Naomba tuwe wawazi tuache unafiki hili ni taifa letu wenyewe.........

JF sio sehemu ya porojo usilete maneno yako ya vijiweni Vingunguti...weka ushahidi wa maneno yako tuone!
 
ritz mbona wewe ndo mateka no 1 wa viongozi wa magamba,huwa unatetea vitu ambavyo hata mtoto anajua vipo wrong! Hatukushangai
 
Wanaompinga Zitto ni wachaga!. Wanahofia Zitto kuchukua madaraka kwenye taasisi yao.

Are you sure? Kama Jimboni kwake tu alimshinda mgombea wa CCM kwa kura 3000 kati ya kura 42,000 zilizopigwa, u-Chaga unaingiaje hapo?

Maswali kumhusu Zito ni mengi na majibu hatuyaoni: Hammer ya RA kugeuka ya kwake; Simu za Mkurugenzi wa Usalama wa Taifa; Utetezi wa kununua mitambo ya Dowans (soma mitambo ya RA); Kupigiwa chapuo na JK juu ya uenyekiti wa kamati ya Bunge; Sifa kwa Kikwete kujenga barabara ya lami ya kwenda Burundi huku wilaya za Kigoma, Kasulu na Kibondo zikikosa mawasiliano ya barabara kila msimu wa mvua; n.k., n.k.

Tabia ya ukinyonga wa Zito, kwa maoni yangu mimi ambaye siyo Mchaga wala Mrundi, (Kigoma kuna Warundi wengi), inanifanya niendelee kuwashangaa CHADEMA kutomfukuza uanachama Zito.

Maadam unaleta u-Chaga (soma ukabila), Zito ni kabila gani?
 
Uzuri wetu tuko wazi kiongozi akifanya vizuri tunamsifia mnafiki tunampa LIVE on the spot haijalishi ana influence kiasi gani kwa jamii.
Mkuu ujue we una point sana, na always una hit to the tagert, ila tu hiyo Avatar yako ndo inanichefua kila nikkiangalia Mkuu, Badilisha Mkuu, haindeni kabisa na points zako,some times nikkiangalia AVATAR Yako, najikuta na scrol down nikihisi utakuwa umeandika Upupu kama hiyo AVATAR yako, kumbe sio Mkuu, itoe Mkuu
 
Zitto Kabwe kiukweli hana mvuto tena kwa vijana na watu wote hata jimboni kwake hawana imani naye ndiyo mana uchaguzi uliopita alishinda kwa kura chache sana ukilinganisha na 2005 nadhani hata hilo yeye anakiri na kama yupo humu jamvini aongelee hili, Zitto Kabwe haamini tena ndani ya jamii hasa hasa jimbo lake mana alidiriki kumpigia kampeni kafulila aliyefukuzwa uanachama ndani ya Chadema kwa makosa yake yaliyodhirika na kuamua kwenda NCCR,sasa huyo huyo tena aliyekuwa anampigia kampeni za wazi wazi kupitia chama pinzani hata mwaka haujaisha kaleta migogoro mikubwa ndani ya NCCR Mageuzi kwa kutokuwa na imani na Mwenyekiti wake mbatia lakini baada ya kura kupigwa Mwenyekiti Mbatia kaibuka mshindi kwa asilimia 99% kwa kura zilizopigwa na wajumbe na kumfanya kafulila kuabika na kufukuzwa chama,huyu ni mtu aliyekuwa anapigiwa kampeni na Zitto jimboni kwake badala zito akisaidie chama chake anakwende kufanya uasi! Kamwe Zitto haaminiki tena na hili la kufukuzwa kwa Kafulila linazidi kumshushia hadhi Zitto kwa kile alichokuwa anamtetea Kafulila na kumpigia kampeni za ubunge! Zitto ni msaliti mkubwa kwa vijana wa nchi yake na chama chake!
 
Zitto sio msaliti wa chama pekee,ni msaliti kwa vijana wote waliomuamini...
 
Back
Top Bottom