Kwanini Wapangaji Tulipe Witholding Tax Wakati Tunatakiwa Kukata Kutoka Kwenye Kodi Ya Pango

Cowman

JF-Expert Member
Feb 5, 2013
1,710
3,145
Unataka kufanya biashara, unaenda TRA kwa ajili ya kupata TIN, TRA wanakwambia lete mkataba wa pango, wanakufanyia assessment na wanakwambia unatakiwa ulipe Rent Income Tax na Stamp duty. Unawauliza ndio nini hizo, wanakwambia ni malipo ya kodi kutoka kwenye kodi ya pango. Unawauliza tena ni nani anatakiwa kulipa kati yangu na mwenye nyumba, wanakujibu ni mwenye nyumba. Unamrudia mwenye nyumba na kumueleza anakujibu 'Kijana hayo mambo wanalipaga wafanyabiashara, unatakiwa ulipe wewe mimi Kodi yangu ni Laki Sita kwa mwenzi, utaki acha. Khaa!

Unapaniki kidogo, unaingia kwenye website ya TRA unakuta;

Withholding tax is the amount of tax retained by one person when making payments to another person in respect of goods supplied or services rendered by the payee. Payment subject to Withholding Tax include Rent.

Unajiuliza je nitafanyaje?...Hamna namna tena unarudi TRA na unalipa TZS 720,000/=

Sasa nauliza hivi nyie mabosi kwanini hatamataki kulipa hii kitu? Mbona tunapunguziana mitaji ndugu.
 
Kodi nitakayolipa ni ile tu ambayo siwezi kuikwepa.
Hii ni ngum kukwepa kuna baadhi ya sehem TRA wameweka rates zao per square metre, na wakati mwingne wanakua wana mikataba ya nyuma ya hilo jengo.
 
Funga biashara nenda kalime .huku kwenye kilomo hatuna hizo kodi zenu za ajabu ajabu.yaani TRA wanaua biashara za watu.
 
Nilitaka kulima pamba ila nimesikia bei imeshuka toka TZS 1200 kwa kilo mwaka jana hadi TZS 1100 mwaka huu.
 
Hakuna sehemu yenye nafuu mkuu, hata huko wakulima wanalia pembejeo bei juu, mazao bei hazilipi, mbaya zaidi mazao yagongane kuvunwa utakuja kuuza debe la mahindi 2500.
 
Nilitaka kulima pamba ila nimesikia bei imeshuka toka TZS 1200 kwa kilo mwaka jana hadi TZS 1100 mwaka huu.
Si umesikia wafanyabiashara wa Tunduma wanachokifanya saa hizi? Wengi wanahamishia biashara zao Zambia kwaajili ya kukimbia msululu wa kodi, kodi kama hio ilikuwa inamhusu mwenye jengo inakuaje uilipe mpangaji??!!??!! Tra toeni majibu najua mpo humu.
 
Mkuu tunaumizana sana halafu wenyewe kila siku wanatuhubiria tujiajiri.
 
Unataka kufanya biashara, unaenda TRA kwa ajili ya kupata TIN, TRA wanakwambia lete mkataba wa pango, wanakufanyia assessment na wanakwambia unatakiwa ulipe Rent Income Tax na Stamp duty. Unawauliza ndio nini hizo, wanakwambia ni malipo ya kodi kutoka kwenye kodi ya pango. Unawauliza tena ni nani anatakiwa kulipa kati yangu na mwenye nyumba, wanakujibu ni mwenye nyumba. Unamrudia mwenye nyumba na kumueleza anakujibu 'Kijana hayo mambo wanalipaga wafanyabiashara, unatakiwa ulipe wewe mimi Kodi yangu ni Laki Sita kwa mwenzi, utaki acha. Khaa!

Unapaniki kidogo, unaingia kwenye website ya TRA unakuta;

Withholding tax is the amount of tax retained by one person when making payments to another person in respect of goods supplied or services rendered by the payee. Payment subject to Withholding Tax include Rent.

Unajiuliza je nitafanyaje?...Hamna namna tena unarudi TRA na unalipa TZS 720,000/=

Sasa nauliza hivi nyie mabosi kwanini hatamataki kulipa hii kitu? Mbona tunapunguziana mitaji ndugu.
Ki msingi Withhold Tax ni Kodi ambayo inakua paid by the source. Mfano Mishahara labda, muajiri anatakiwa yeye akukate wewe miajiriwa kisha yeye ndie apeleke TRA, wewe akupe Net salary ikiwa imeshakatwa hiyo kodi (PAYE).

Sasa kama Mwenyenyumba asipolipa kodi ni kosa lako wewe kutomkata hiyo tax wakati unampa pango lake. Same way as Mfanyakazi asipokatwa kodi na Mwajiri basi ni kosa la mwajiri anaempa mshahara mfanyakazi, na sio kosa la mfanyakazi anaepokea mshahara usiokatwa kodi.
 
Mkuu nimekuelewa sana ila tatizo ni hawa Landlords kama kodi yake kwa mwezi ni laki sita yeye anataka M7.2 kwa mwaka sasa ukianza kumwambia mambo ya witholding tax anageuka mbogo na atakwambia tu kama umeshindwa acha. Nadhani itegenezwe namna ya kuwabana hawa watu la sivyo wanatuachia mzigo mkubwa sana.
 
Back
Top Bottom